MWONA MBALI
JF-Expert Member
- Oct 7, 2016
- 460
- 612
Ni katika uhuru wa mawazo natafakari hili, demokrasia katika Africa imekuwa na maigizo mengi sana, mara nyingi vyama tawala bila kujali kukubalika kwake na wananchi vimekuwa vikitumia dola na fursa ya utawala kujihakikishia utawala wa milele. uhuru wa kidemocrasia wa vyama pinzani umekuwa ukibanwa pasipo sababu za msingi.
Ili vyama vya upinzani viweze kwenda mbele vinahitaji watu makini wenye weledi na ujanja wa kisiasa kutumia fursa ndogo wanazozipata kujitangaza na kujenga hoja madhubuti na kufanya chama tawala "kihahe".
Ni miezi michache iliyopita shughuli za kisiasa za vyama ni kama ilikuwa imepigwa marufuku kabisa, sasa angalau mikutano ya ndani imeruhusiwa.
nilitegemea fursa hii ya kuruhusiwa mikusanyiko ya ndani kwa chama kikubwa kama CHADEMA ingeitumia vizuri ili kuhalalisha madai yao ya kubanwa kisiasa. na kwa kuwa chama kina mtandao wa nchi nzima pengine zingeibuliwa hoja mbalimbali zenye kuonyesha mapungufu ya kiutendaji ya serikali na pengine kushauri maeneo ya kuboresha, yote ni katika kuletea maendeleo taifa letu.
ACT wazalendo pengine ni chama kinacho onekana kidogo kilicho na mbunge mmoja tu, wao wameiona fursa hii jana walikuwa na mkutano wa kidemocrasia uliokuwa na waliikwa mbalimbali, sitajikita sana ya nini kilijadiliwa ila kitendo cha ACT kufanya mkutano ule wa ndani kwa ufanisi, kinafanikiwa zaidi kujitangaza na wameonesha kuwa wanaweza kutumia fursa ndogo zilizopo kufanya mambo makubwa.
Idara za uenezi/habari/na propaganda za vyama vya siasa hasa vya upinzani zinapaswa kuwekwa watu wenye akili nyingi na wanaojua kutumia kila fursa inayojitokeza ili kuimarisha uhai wa chama.
CHADEMA ni chama kikubwa zaidi ya ACT ila idara yao ya PROPAGANDA NA UENEZI ina watu wasio na AKILI KUBWA wakati ACT WAZALENDO ni chama kidogo kuliko CHADEMA ila idara yao ya PROPAGANDA NA UENEZI ina watu makini na wenye akili nyingi.
Najiuliza CHADEMA wana hoja gani kwa wananchi? je hiyo hoja yao itatoka kwa mikutano ya hadhara na maandamano pekee?