CHADEMA ndani ya Morogoro!!

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,973
Taarifa za uhakika nilizonazo kutoka Morogoro, ni kuwa viongozi wa Baraza la vijana Taifa (Bavicha), Bw. John Heche(mwenyekiti) na Bw. Deogratius Munishi(Katibu Mkuu) wapo mjini humo katika harakati za kukiimarisha chama.

Wataanza kwa kufungua tawi la vijana Nanenane, kisha watafungua tawi jengine Kilakala na mwisho watafungua matawi mawili kata ya Kichangani.

Baada ya kukamilisha shughuli ya ufunguzi wa matawi, watamalizia kwa kuhutubia mkutano wa hadhara eneo la Kichangani.

Wananchi wa Morogoro kazi kwenu ugeni ndio huo, vijana wako kazini na ujumbe wa ukombozi wa kweli toka kwa mkoloni mweusi.

Naomba kuwasilisha.
 
Shime wana morogoro mjini,hususan vijana hudhurieni kwa wingi na kwa umoja wenu ukombozi wa kweli kutoka kwa mkoloni mweusi utapatikana.
 
tupo pamoja, nimeona na matawi yatakayofunguliwa,watu waamke sasa maana kila siku twadanganyiwa lifti za bure za mabasi mekundu
 
tupo pamoja, nimeona na matawi yatakayofunguliwa,watu waamke sasa maana kila siku twadanganyiwa lifti za bure za mabasi mekundu
Labda ni washabiki wa simba leo si AZAM na Simba...lol
 
john heche kwa kupenda posho hajambo anaanda vi ziara visivyo na maana ilimradi apate posho tu amakweli njaa mbaya
 
john heche kwa kupenda posho hajambo anaanda vi ziara visivyo na maana ilimradi apate posho tu amakweli njaa mbaya

Imeandikwa asiyefanya kazi na asile. Maadam Heche anafanya kazi basi ni haki yake kula posho.

Mbona wabunge wanakula posho kwa kusinzia mjengoni!
 
john heche kwa kupenda posho hajambo anaanda vi ziara visivyo na maana ilimradi apate posho tu amakweli njaa mbaya
BORA KUPENDA POSHO YA CHAMA CHAKO KULIKO RUSHWA YA MAFISADI! Heche kanyaga kamanda ht huku upande wa mashekh tunakukubali ungependa posho ungeenda kukaa uzini ukisaini kila siku karibu sana hata huku madrasa wewe (Xvi )tulia unyolewe cheo kimepata jembe
 
Back
Top Bottom