Nimepita Rwamishenye mida ya saa tano ilikuwa balaaa.
Yaani utadhani wanazindua kampeni za Ubunge Kati ya Rwakatare na Kataraiya. Jana Rwakatare alifanya mahojiano na Redion Vision yahapa Bukoba. Mtaani hii ndo ilikuwa gumzo. Mwamko na ari ya Wananchi iko juu sana.
Kwa hapa, baada ya maandamano na mkutano, CHADEMA inaweza kujikuta imefanikisha mambo mengi sana ikiwemo kuvunjavunja nguvu za ccm. Agenda kuu waliyoiweka mbele (UGUMU WA MAISHA na DOWANS) zimewakamata vilivyo wananchi wa hapa. Hata wiki iliyopita Kagasheki alipofanya Mkutano, wananchi walimweleza bayana msimamo wao juu ya mambo hayo. Kagasheki alikuj ghafla kuwahi KIMBUNGA cha ujio wa Dr. Slaa