CHADEMA naomba ufafanuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA naomba ufafanuzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nduka, Jun 4, 2012.

 1. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Waungwana tangu chama hiki kipate nguvu ya uungwaji mkono na ruzuku kimeanzisha mapambano ambayo kimsingi sioni kama ni muhimu kwa chama cha siasa. Natumbua lengo la chama cha siasa ni kushika dola hivyo inaeleweka zaidi kwa mapambano ya CDM kuelekezwa CCM ila hainiingii akilini pale mapambano yanapoelekezwa kwa vyama vyenzake vya upinzani. Kwa mfano CDM ipo kwenye mapambano ya kila siku na CUF na NCCR hivi mapambano haya yanalenga kupata nini? Na ni kwa nini CUF na NCCR?
   
 2. I

  Iramba Junior Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka jibu ni dogo sana, katika vita hakuna adui mkubwa wala mdogo,adui ni adui tu, na kwa sababu kama ulivyosema CDM inataka kushika dola ni lazima kuakikisha kwamba mashambulizi ni kwa kila ajae mbele.
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Iramba nakubaliana na wewe kwa upande mmoja lakini sioni kama haya mapambano ni strategic maana yanapunguza focus kwenye lengo kuu lakini pia kuharibu kujenga uadui na adui wa adui yako ni kupoteza nguvu bure maana yeye alipaswa kushughulikiwa na adui yako. Hii haipunguzi gharama tu bali pia hupunguza nguvu za adui.
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  huwezi kuwa na vita na mtu bado ukaamini mke na watoto wake ni salama sana hata ukanywe nao chai.
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Edmund kinachowafanya NCCR na CUF kuwa mke na mtoto wa CCM ni kipi na kinachowafanya CHADEMA wasiwe ni kipi?
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mkuu hivyo vyama ni wakala wa chama tawala. CCM imewapa jukumu la kuivuruga CDM. Sasa CDM baada ya kushtukia dili lao wameamua kujizatiti kupambana nao yaani 3 in 1.
   
 7. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Kila siku CHADEMA, CHADEMA, CHADEMA. Hivi hii chadema itazuia msife? au itawaokoa na moto wa milele?.
  SIASA ZITAPITA BALI NENO LA MUNGU LITADUMU MILELE.
   
 8. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,827
  Trophy Points: 280
  Kumbe ndauka wa bongo movie.
   
 9. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We don't get U.

  Sidhani kama una ushahidi kwa hayo uliyosema? Thibitisha hilo kabla hujaandika.
   
 10. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu hebu tuondolee wokovu kwenye jukwaa la siasa nenda kwenye jukwaa husika
   
 11. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mbona hilo avatar lako linafanana na marehemu CCM na CUF?
   
 12. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Mzee wa njaa, unataka uthibitisho upi? Wa Wenje kumkebehi mwenyekiti wa NCCR au Halima Mdee kumtusi kabisa? Au kauli za Mbowe alipoeleza kwa nini kambi rasmi bungeni haihusishi wabunge wa vyama vingine vya upinzani?
   
 13. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kauli yako haina facts ndio maana nakuambia thibitisha ndugu....
   
 14. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  NCCR na CUF vilikuwa na nguvu zamani kabla ya CDM labda CDM ndio inatumiwa kuvivuruga.
   
 15. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Mzee wa njaa, fact zipi unataka? Au wewe unajua uhusiano mzuri wa CUF na CDM?
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  CUF wapo kwenye serikali ya umoja wa kitaifa
  NCCR nao hivyo hivyo, angalia Mbatia na manjonjo yake
   
 17. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wewe Nduka , ni mwana Gamba na ndio maana unaumia sana tunapowasema NCCR na CUF kwani unatimiza kiapo cha ndoa,kwamba ntakupenda kwenye shida na raha.swali dogo tu kwako ambalo ndio litakua jibu la swali lako. NI JE WEWE KAMA MWANA CCM UNAUMIA NINI NA KUPUNGUKIWA NINI SISI CHADEMA TUNAPOWASEMA CUF NA NCCR?
   
 18. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Hivi hadi leo tunaushamba wa demokrasia kiasi hicho au ni makusudi? Aina ya muafaka wa Zanzibar sio mgeni duniani na nilidhani kwa hali hyo CDM ingejinasibisha kwa CUF ili kujifunza kwa maslahi ya wananchi. Ni ubinafsi tu ndio unaweza kukusukuma uendeleze migogoro kwa maslahi ya chama. Hivi baada ya uchaguzi CDM walimtambua rais? Na msimamo wa CDM kwenye rasimu ya katiba je? Hii ni mifano ya makubaliano yenye maslahi kwa wananchi na taifa. Siku zote unaanza na maslahi ya taifa halafu chama baadaye.
   
 19. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Safi sana mkuu kwani kwenye msako wa nyani ngedere hawezi kusalimika!
   
 20. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Hivi kila mtu CDM hata hiyo demokrasia kwenye jina la CDM itakuwa na maana? Naumia kama mtanzania kuona taasisi inayoendeshwa kwa kodi za wananchi inafanya kazi kinyume na malengo yake.
   
Loading...