Wewe na Chakubanga ndio mmechanyikiwa! Subirini muziki wa watu wenye hasira na fedha zao,mtajificha uvunguni!Si siri tena kuwa CHADEMA inajichanganya na imechanganyikiwa.
Uchaguzi mdogo wa Songea, Longido na Singida umesusiwa na CHADEMA. Uchaguzi wa Kinondoni na Siha wanakaa vikao vya kusimamisha wagombea. Unaweza uliza nini kimebadilika mpaka sasa?
Acha kuonekana ndumila kuwili. Ina maana viongozi wetu hawajui wapi washike?
Kuhusu Lowassa inachekesha sana. Lowassa alipokwenda Ikulu kila kiongozi alimpinga kwa uwazi sana. Lema, viongozi wa BAVICHA, Mbowe na Lissu walionyesha Lowassa kutofanya vema kwenda Ikulu.
baada ya siku mbili Mbowe anasema wote waliokejeli Lowassa wamuombe radhi kwa kumtukana hadharani huku ikisema chama kina wasemaji wake wanaojulikana. Kwani tumesema mara ngapi juu ya chama kukosa msemaji ambaye tunaweza sema chama kimesema?
Kwa maana nyingine Lowassa ameonyesha hakuna wa kumsimamia tena huko. Atafanya kama anavyotaka bila wa kumkemea tena.
Hebu chama kisema msimamo juu ya uchaguzi mdogo Kinondoni na Siha, nini kimebadilika mpaka sasa?
Updates:
View attachment 679645