CHADEMA na tishio la Tendwa kukifuta Chama kisa Maandamano/M4C

Hellow wanajamii, hivi majuzi nimesoma gazeti moja hv likisema kwamba "CCM yasema yaweza kukifuta chama cha democrasia"...Hivi inawezekana aje chama kimoja kukifungia chama kingine?
 
Chadema ni chaguo la mungu kwani ni sauti ya wengi. Chadema ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo. CCM hawana ubavu wa kuifuta Chadema, CCM inapotea katika sura na mioyo ya watanzania muda si mrefu. R.I.P CCM
 
Hellow wanajamii, hivi majuzi nimesoma gazeti moja hv likisema kwamba "CCM yasema yaweza kukifuta chama cha democrasia"...Hivi inawezekana aje chama kimoja kukifungia chama kingine?

.
Nnachofahamu mimi kwa sasa ni kwamba Chadema ina uwezo wa kuifuta sisiemu kwenye sanduku la kura.
.
 
Andaa mazishi ya nyinyiemuu mkuu,watu kama akina tendwa,nepi,mkama six,kilango,lusinde aaagh!!hawataisha kuwataja wote ndio wanaimalizia kuinyonga.
 
hellow wanajamii, hivi majuzi nimesoma gazeti moja hv likisema kwamba "ccm yasema yaweza kukifuta chama cha democrasia"...hivi inawezekana aje chama kimoja kukifungia chama kingine?

kwa fitina, kuwaundia kesi, kuwachafua kwa mbinu kama alizofanyiwa mwangosi, ally na ulimboka na mbinu nyingine chafu ambazo mtu asiye na macho na akili atasema ni chadema wameyanya hayo, lakini mwenye akili atashtukia janja ya mabwepande
 
Mbona anahangaika hangaika tu si akifute aone moto wake? kutishia nyau mtu mzima this is too much, he should action upon bana kha!
 
hicho kijamaa kimelewa madaraka ndo maana kinaongea mambo yanayolingana na ufupi wake, ngoja nianze kukigonga makwenzi ili kizidi kudidimia. keep on chadema, keep on m4c!!
 
Sijui kama hawa jamaa wa chama tawala wanajiona jinsi wanavyopwaya katika swala zima la demokrasia. Bado hawajafahamu maana yake au wanajifanya kutishia watu? Nashindwa kuamini kuwa wanaelewa maana ya demokrasia yaa vyama vingi nchini. Bado wanamatamshi yenye virusi "zidumu-fikra". Hili ni tatizo kubwa sana maana ingeeleweka kama ingekuwa ile miaka mitano ya mwanzo tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi.
 
Kama upeo wa akili za Tendwa, au Mabwana zake wanaomtuma, ni kutaka kukifuta Chadema au kuzuia M4C kwa sababu watu wanauliwa kwenye mikutano yake, basi ili asikifute, asizuie tu M4C, bali akikataze pia kisishiriki chaguzi ndogo, maana huko pia watu wake wanauliwa kinyama kama tulivyoshuhudia Igunga na Arumeru. Au haoni kuwa Polisi na Majambazi wengine wa CCM waliofundishwa kwenye makambi maalum wanaua watu kwa makusudi ili wapate sababu za kipumbavu za kuikwamisha CDM? Kwanini asitoe tamko dhidi ya wanaoua badili ya kuwasakama wanaouliwa? Hivi ni kweli Tendwa anaweza kuwa So Low kiasi cha kuamini kuwa nchi itakuwa na amani kwa kukifuta Chadema? Au ndio Kicks of A Dying Horse?
 
Kumekuwana matamshi mbalimbali kutoka ccm na taasisi zake kama uvcc, uwt na msajiri wa vyama vya siasa.dha hii ilianzia kwa waziri wa uratibu na sera mh.wasira kuwa chadema ni chanzo cha vifo kwenye mikutano yake hivyo ni vyema chama hicho kikafutwa kwa mujibu wa sheria.hata kabla ya kifo cha mwandishi wa habari mwangosi wassira alishatoa tamko hili.Jana pia katika maazimio ya mkutano mkuu wa uwt , kumetoka tamko hilo hilo.Hii inathibitisha kuwa dhana ya chadema kuwa tishio kwa chama tawala, imejadiliwa na kuwekewa mkakati kukifuta chadema kwa hila ya uchochezi , kusababisha vifo,kusababisha vurugu, hivyo kuwa chama kinachositahili kufutwa.haiji akilini huku tatizo la vurugu , vifo , na vikwazo vya ukuaji wa shughuli za kisiasa za chadema ni dhahiri zinavyudumazwa na vyombo vya dola.Hivyo basi kwa matamshi haya mbalimbali ya taasisi za ccm, mkakati ambao umepangwa mahususi na tendwa kushirikishwa kuwa mtekelezaji
CHANZO:TAARIFA ZA HABARI TV JANA
 
Back
Top Bottom