Exaud J. Makyao
JF-Expert Member
- Nov 30, 2008
- 1,518
- 22
CHADEMA imeamua kurahisisha maendeleo ya chama kwa kuingiza suala la teknolojia.
Sasa CHADEMA imeanzisha E-Membership.
Yaani Electronic Membership.
Mtu akitaka kujiunga na CHADEMA aweza kujiunga kupitia INTERNET.
Naona wanataka kuweka katika vitendo SERA YA CHADEMA YA ELIMU.
SEHEMU YA SERA HIYO INASEMA HIVI,
Hali ya Elimu yetu Tanzania ikoje?
Hii imekaaje wanajamii?
Sasa CHADEMA imeanzisha E-Membership.
Yaani Electronic Membership.
Mtu akitaka kujiunga na CHADEMA aweza kujiunga kupitia INTERNET.
Naona wanataka kuweka katika vitendo SERA YA CHADEMA YA ELIMU.
SEHEMU YA SERA HIYO INASEMA HIVI,
Hali ya Elimu yetu Tanzania ikoje?
- Elimu bado ni ya kikoloni inayozalisha watwana.
- Mitaala haiendani na hali halisi ya kidunia.
- Wanafunzi wanalazimishwa kusoma kila somo kupata vyeti wakati vipaji haviendelezwi.
- Mpango wa Elimu ya Msingi wa kudandia uliyogubikwa na rushwa – Maandalizi ya walimu ni duni na rasilimali hazifikii walengwa.
- Bajeti ya elimu finyu sana – asilimia 9 tu!
- Tanzania ni nchi ya tatu kutoka mwisho duniani ambayo kiuwiano na idadi yake ya watu, ina idadi ndogo ya wasomi wa sekondari na vyuo.
- Elimu inawezeshwa kwa fedha za mikopo na misaada ya wahisani wakati fedha itokanayo na kodi atozwayo mwananchi inafanyiwa anasa tu.
- Gharama za elimu bado ni mzigo mkubwa kwa familia masikini.
- Mazingira ya elimu ni duni – madarasa, nyumba za walimu, maabara na vitabu.
- Mfumo wa Elimu hauna mtazamo wa Kijinsia hivyo hauweki mazingira mazuri ya kupata maarifa kwa wanafunzi wa kike na pia wanafunzi wenye ulemavu.
- Mazingira ya shule haya kidhi haja na sio rafiki kwa watoto wenye ulemavu wa viungo,wasioona na viziwi.
- Elimu ya teknohama hususan sayansi ya kompyuta haijaanzishwa.
- Mfumo wa elimu unaochelewesha kuhitimu – kuchelewa kuanza (miaka 7+) na kuchelewa kumaliza (2,7,6,3+)
- Elimu ya Uraia ni finyu na potofu.
- Michezo mashuleni imefutwa na hivyo kuziba vipaji vya watoto mfano UMITASHUMTA na UMISETA.
Hii imekaaje wanajamii?
Last edited: