CHADEMA na tathmini ya Uchaguzi jimbo la Uzini

Ni vizuri ku share ni kipi mmejifunza kutokana na siasa za Znz? Tusiwe wachoyo ni vizuri kutathimini na sio kujificha na kufa kibudu.

Sijawahi kusikia au kuona jitihada za kushirikiana na mpumbavu zina tija.
 
Mwita,
Siasa za Znz ni zaidi ya unavyyozijua. Ndio maana hukumuona Jussa, maalim Seif hata mtatiro na Mh Juma Duni kuweka kambi kule. Kwani lile jimbo kwa vyovyote vile ni mali ya CCM.
Nikubainishie kidogo hata kama CCM wangeamua kuweka mgombea wake awe Jiwe au Pake na nyie wengine wekeni Bin'Adam basi juwa yule wa CCM laazima ashinde. Ndio maana CUF na vyama vingine hawakutumia nguvu kubwa kutafuta kiti hicho.

Chadema nafikiri utakubaliana na mimi kuwa Dr Padre Slaa aliweka kambi huko akiwemo na yule ndugu yetu Waitara na Heche na vijana wenziwe kwa takriban siku zote za uchaguzi ndio wameangukia pabaya zaidi ya ule uchaguzi wa 2010. Kwani 2010 walipata 7% na leo wamepata 4%.
Sasa nafikiri Chadema wajiulize je wamekuwa au ndio wamedebweda?
Huko ni kufaulu au kufeli ukilinganisha na nguvu walizotumia?
Nafikiri siku nyingine lazima wasome alama za nyakati kabla kukurupuka.

mkuu kumbuka kuwa CHADEMA hawakuwa na mgombea wa kiti cha uwakilishi 2010 kama unavyo kutudanya sasa hapa CDM wamepanda from 0% to 4% ila CUF ni dhadhili watu wa Uzini wanasema hata kwenye serikali ya mseto hakitakiwi kwa matokeo

Kuhusu report chama makini lazima kitatoa ndiyo maana hadi sasa hujasikia wakuu wakiongelea labda sema 4% ni ndogo na tutakuuliza vigezo
 
Nafikiri CUF kama wana akili waanze kujifunza kutokana na kumfukuza HAMAD RASHID, kwa mawazo yangu hili limechangia matokeo hayo. Kwa tathmini ya haraka haraka inaonyesha kuwa kwa sasa CUF inazidiwa au inalingana nguvu na CHADEMA kisiwani unguja.
 
Back
Top Bottom