CHADEMA na Polisi wakubaliana kusitisha maandamano ya Machi 25

Hata Mh. Lema naye ameanza kuwa mjasilimali wa michango ya wanaCHADEMA. Nafikiri anajifunza kutoka kwa Mh. Mbowe. Sijui ile chopper bado iko kwenye meli au bandarini?. Mbona yuko kimya sana!!.

Huyu Chris Lukosi lazima atakuwa anafahamu kwa sababu yeye ndiye alimpeleka kwenda kupiga picha kwa ma-dealer wa used chopper.
Mkuu ile ilikuwa ni kanya boya na nilifanya hivyo kwa maagizo ya boss Lema
Chilisosi akarusha hewani, si unajua tena siasa za chadema ni kanyaboya tu!
 
Hapa ndio nakubali mageuzi yataletwa na sisi raia na si wanasiasa! wengine tunapiga kelele huku mtaani hadi tumeonekana majuha!

Mkuu wangu sasa naona tunapoteza muelekeo wa kuitoa CCM madarakani live!!!

Sikuangalia TV zingine. Kama Source ya taarifa ni Channel 10 tu, nina mashaka na authenticity ya taarifa hiyo.
Hii inawezekana habari ya kupotosha jambo.
 
Mkuu uwe na adabu
Ina maana hata babu nae alisafiri mpaka mbeya?
Nasikia unaishi Uingereza,lakini posts zako hazina tofauti na Mtanzania ambaye hakufuta ujinga na hajawahi kutembea na kuishi ktk jamii iliyoendelea! Hata wewe ni mzee mtarajiwa, hivi karibuni utaitwa babu au bibi. Ningetarajia kwa kuishi kwako nje,tena nchi iliyoendelea,ungekmfano kwa mijadala yenye hoja za msingi,siyo hii mipasho ya kijinga!
 
Ndo shida ya kuposti kishabiki, kwa taarifa yako Mwema kang'amua ukweli kwamba kesho watu wanafanya kweli na hizi

porojo na matangazo yake yamekwa na njia ya kufikia amani ni moja tu kumuangukia Kamanda mbowe ili aturejeshe

nyuma kwa muda tukisubili ufumbuzi. Mapatano ni jambo la msingi na zuri lakini ujuwe na ifahamike kwamba popote

duniani hakuna kilichoshinda nguvu ya umma.

Mwisho Tutafikia muafaka nao nikuona kawambwa na Mulugo wanatoswa 90% failure ni upuuzi mkubwa,

nikutudhalilisha watanzania, nikulidharirisha Taifa na kutowatendea haki watoto wetu na viizazi vyetu hapo baadaye.

Wewe muache mtoto wako ashinde na facebook na whatsup halafu tegemea atafaulu na sms usiku kucha anawasiliana na honey na darling halafu subiri kawamba ajiuzulu ha ha haa wabongo bwana kazi kweli kweli
 
Lets wait and see wale wafuata upepo, hongera sana Mbowe na IGP kwa kuweka utaifa mbele, maana wewe kama m/kiti wa chadema unge lazimisha maandamano hayo uliopanga yangetia doa fursa ya kuvutia wawekezaji kutokana ujio wa rais wa china kwa maana kama Rais wao anakuja hapa TZ alafu watanzania wanaandamana itaonekana hatuja ona faida yake ya kuja hapa Tanzania.
 
Nasikia unaishi Uingereza,lakini posts zako hazina tofauti na Mtanzania ambaye hakufuta ujinga na hajawahi kutembea na kuishi ktk jamii iliyoendelea! Hata wewe ni mzee mtarajiwa, hivi karibuni utaitwa babu au bibi. Ningetarajia kwa kuishi kwako nje,tena nchi iliyoendelea,ungekmfano kwa mijadala yenye hoja za msingi,siyo hii mipasho ya kijinga!
Amepewa jukumu maalum la kupambana na CHADEMA kwenye mitandao ya kijamii hususan humu JF, lakini kwa mipasho hii anajisumbua sanasana wanajiongezea mikosi kwa kuwa na wanamikakati feki kama hawa.
 
.
Hata kama chadema wameyaahirisha maandamano mimi binafsi nitaandamana kuizunguka nyumba yangu mara saba nikilaani uzembe wa wizara ya elimu na zaidi sana waziri. Hilo pekee ndilo litakaloweza kupoozesha kwa kuahirisha hasira zangu.
.
hata mimi nitaandamana kuizunguka meza ya hapa ofisini
 
Wengine wamechukia kuahirishwa maandamano na wengine wamefurahia lakini mimi nimejifunza kitu, viongozi wa Afrika hawana ustaarabu wa kuwajibika kwa kuwa wapo wanaowatetea hata pale wanapovurunda.
 
Jamani pro-CCM hebu acheni basi hioz kejeli zenu kwani unaboa sana, tangu jana usiku hamjalala kupiga majungu, sio fair kabisa.
 
hata CUF hawakuanziwa mbali sana kidogokidogo polepole leo wako wapi washaingia mkataba wa serikali ya kitaifa ili hali wao ndo walikuwa ni washindi mara zote sasa hivi wamegutuka kujifunika shuka akati kushakucha muelewe ccm hutumia pesa nyingi kusomesha watu wake political science na si technolojia au science yote hayo ni namna ya kutawala wa Tz ninaamini upo wakati utafika na watang'oka madarakani ila kwa vyama madhubuti haswa pengine hata isiwe CDM au CUF
 
CDM na viongozi wake ni lazima kuwa na msimamo, vinginevyo watu wataanza kukosa imani na nyinyi.

Hii kukaa na kusema mmekubaliana na mnaowaita kila siku kuwa ni watesi wenu, policcm, bila kubainisha misingi ya makubaliano yenu haileti picha nzuri kwa wapenzi na wadau wenu wa siasa.

Nimeweka hojaji chache za kujiuliza:-

1. Mmekubaliana nini? Kwa sababu zipi?

2. Huo uovu mnaodai kufanyiwa nao wamekubali kuuacha?

3. Mnaziamini ahadi zao?

4. Hii ni mara ya ngapi kuwataka muache kufanya maandamano? Wanaheshimu ahadi zao? Je, zile sababu za upotoshaji walizozitoa awali wamezifuta? kwa nini walizitoa?

5. Ni kweli uamuzi unatokana na majadiliano au hakukuwa na nia ya dhati kwa viongozi ku-risk na kufanya maandamano hayo?

6.Maaandamo hufanyika wakati gani? Misingi ya kuahirisha ni nini? Makubaliano? Kulinda maslahi?Uoga?

7. Je, baada ya muda huo kupita mantiki ya maandamano bado itakuwepo? Wakikataa tena kuwaruhusu?

8. Ile mikutano iliyoishia Iringa na baadaye ikasimama, sababu zake ni zipi?

9. Hawa watu wanaowamini, wataendelea kuonyesha imani yenu kwao iwapo hii ndio inakuwa style ya maamuzi yenu? Dakika za mwisho mnarudi nyuma?

10. Kwa nini mpaka sasa, pamoja na wadau wengi kuonyesha nia ya kuwasaidia, hamjatoa mkakati wa wazi wa uhakika wa kuwa na vyombo vyenu wa habari? Mfano, taarifa hii ya kuahirisha, itawafikiaje wadau wenu kwa haraka?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimekubalina na jeshi la Polisi Tanzania kusitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike kesho tarehe 25/03 kushinikiza kujiuzulu kwa Mawaziri wa Elimu

Upande wa Chadema kwenye mazungumzo hayo umewakilishwa na Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe na ule wa polisi umewakilishwa na IGP Said Mwema. Pande mbili zimeafikiana kukutana tena ndani ya siku 14 kwa ajili ya kuboresha mahusiano ya pande mbili.

Source: Chennel Ten

Hongera sana Mbowe na IGP huo ndio uongozi makini wa kujali maslahi ya taifa, haipendezi mgeni anakuja anakuta sisi wenyewe tunagombana au kupingana katika suala ambalo linaweza kujadiliwa kwa pande zote mbili na kufikia muafaka bila ya vurugu wala bugudha na hivyo kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
 
Nilitarajia haya kwani hivi juzi tu walioitwa wafuasi wa sheikh Ponda (ambao nataka waitwe waislam) walifanya kitu hicho hicho walichotaka kufanya chadema wameishia jala miaka mitatu hata wanaoua wananchi kwa ufisadi hawajawahi kufungwa.nasema nilitarajia kwani njia ambayo igp ameitumia kwa chadema haiwezekani kwa waislam?ila kwao mazungumzo yamewezekana ila ingekuwa waislam wasingeitwa wangeshia virungu na sasa ni staili mpya ya jela tambueni malalamiko ya waislam yanafanana na wana jamii wengi wa nchi hii sasa nadhani serikali iongeze magereza maana njia waliyobaki nayo watanzania ni hiyo tu kwani wamepuuzwa muda mrefu.IGP simamia uadilifu
 
Jamani tuache ushabiki wa vyama na siasa hayo maamuzi ni ya busara na hekima Mbowe katanguliza Tanzania kwanza,Kusitisha maandamano hakubadilishi msimamo wa chadema!
 
Tangu saa 12 alfajri niko barabarani na bango langu chaajabu hamna mtu anae nisapot au ndio kusema mwenyekiti ame tusaliti?
 
Back
Top Bottom