THE COMMISSIONER
JF-Expert Member
- Dec 3, 2012
- 267
- 111
Huku Jeshi la polisi nchini likiamua kutumika vibaya na Chama cha Mapinduzi na Serikali yake kwa kupiga marufuku maandamano kwenye mikoa yote yalikopangwa kufanyika, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeendelea kusisitiza na kulitaka jeshi la polisi kutambua hivyo kuwa maandamano yako pale pale.
Taarifa iliyotelewa kwa vyombo vya habari na jeshi la polisi kwa jiji la Dar es salaam zinadai kuwa haliwezi kuruhusu maandamano hayo kwa kuwa kuna ugeni wa rais wa China siku hiyo lakini CHADEMA wamedai kuwa Rais wa china yuko hapa nchini kwa maslahi ya nchi yake na wao CHADEMA wako kwenye shughuli zao kwa maslahi ya nchi ambazo hazina mausiano yoyote na rais huyo wa china.
Kwa upande wa Arusha Jeshi la polisi linadai kuwa haliwezi kuruhusu maandamano hayo kwa kuwa CCM nao wameomba kufanya maandamano siku hiyo kwenye barabara hizo hizo walizoomba CHADEMA kwa nia ya kuipinga CHADEMA na msimamo wao wa kumtaka waziri ajiuzulu. Taarifa zinaendela kusema kuwa CHADEMA wameliambia Jeshi la polis mkoani huo kuwa hakitatetereka katika msimamo wake na kwamba ni jukumu la jeshi la polisi kupanga barabara tofauti zitakazotumika na vyama hivyo na kwamba wao CHADEMA wataendelea na maandamano yao katika barabara zile walizozipanga na kama wanawahusudu sana CCM basi wawapangie barabara tofauti.
Jijini Mbeya hali insemekana kuwa tete kwani kila mmoja yaani polisi na CHADEMA wameonyesha misimamo mikali na tayari taarifa zinadai kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ameamua kufanya kikao na wachungaji na maaskofu ili kuwaomba wawatangazie watu kwenye ibada za kesho kuwa wasijitokeze kwenye maandamano hayo kwani yataatarisha amani. Kwa upande wa CHADEMA wameendelea kulieleza jeshi la polisi kuwa adhma ya maandamano ya kuomngo'oa Kawambwa iko pale pale iwe mvua ama jua.
Pia taarifa kutoka makao makuu zilizosambazwa kwa vyombo vya habari leo hii na zimeeonyesha vikosi vitakavyoongza maandamano hayo ambapo kwa upande a Jiji la Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CHADEMA Tiafa Freeman Mbowe akisindikizwa na wabunge wote wa Dar es salaam watawaongoza wananchi kuelekea kwa waziri mkuu.
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Slaa, Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi na Mbunge Sugu watakuwa jijini Mbeya, wakati Mwenyekiti wa BAVICHA Tifa John Heche, Tundu Lisu, na Godbless Lema watakuwa jijini Arusha na kwa upande wa Mwanza Mwenyekiti wa Wazee Taifa Nyangaki Shilungushela na Ezekeia Wenje Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.
Hata hivyo taarifa zinasema Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema anatarajia kukutana na uongozi wa CHADEMA Taifa ili kuwaangukia kusitisha nia yao hiyo kwa kuwa nchi iko kwenye ugeni mzito jambo ambalo linasemekana kuwa CHADEMA hawako tayari kusikia chochote juu ya hilo.​