CHADEMA na orodha mpya ya mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA na orodha mpya ya mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Indume Yene, Jan 12, 2009.

 1. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inakusudia kuja na orodha mpya ya mafisadi kama ilivyoandikwa katika gazeti la Nipashe (Jumatatu). Tunaelewa serikali ya SISIEMU bado inajikongoja kuwashughulikia mafisadi waliowahi kutajwa na chama hicho juu ya ufisadi.

  Swali, je serikali kipindi hiki imejiandaa vipi na hii orodha ya AIBU. Kwa habari zaidi soma hapo chini:-


  CHADEMA waibua orodha mpya ya mafisadi

  2009-01-11 16:03:15
  Na Mashaka Mgeta


  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeibuka na orodha mpya ya aibu, yenye majina ya watu wanaojihusisha na kashfa za ufisadi, hivyo kuhujumu uchumi na kulitia hasara Taifa.

  Hatua hiyo imebainika jana, ikiwa ni siku moja kabla ya kuanza kwa kampeni ya operesheni sangara Jijini Dar es Salaam, itakayozinduliwa kesho.

  Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto aliliambia NipasheJumapili jana kuwa, majina ya watuhumiwa hao wa ufisadi yanaendelea kushughulikiwa na chama hicho, kwa kushirikiana na vyanzo mbalimbali katika vita dhidi ya vitendo hivyo.

  Hata hivyo, Zitto hakutaja majina wala nyadhifa za wahusika katika kadhia hiyo ya ufisadi, kwa madai kuwa uchunguzi wa kina unaendelea ili kupata uhakika wa kuyaweka hadharani.

  ``Itachukuwa muda kidogo kuwataja, kwa sababu tunaendelea na uchunguzi wa kina, ili kujiridhisha na ukweli uliopo kuhusu tuhuma zinazowakabili, ndipo tuwataje,`` alisema.

  Taarifa za awali zilizolifikia gazeti hili, zilidai kuwa katika mikutano yake ya operesheni sangara Jijini Dar es Salaam, Chadema itataja majina mapya ya mafisadi, wakiwemo wamiliki wa kampuni ya Kagoda Agricultural Limited.

  ``Tunaendelea kuwashughulikia, hivyo hatutawataja kwa sasa, lakini huenda tukawatoa wengine pindi tutakapojiridhisha dhidi ya vitendo vya ufisadi walivyovifanya,`` alisema.

  Zitto, alisema uchunguzi wa tuhuma dhidi ya majina ya mafisadi wanayoyafanyia kazi utakapokamilika, watatumia jukwaa la siasa kuwataja hadharani, na si kuwasilisha majina kwa Tume ya Kupambana na Kudhibiti Rushwa (TAKUKURU).

  ``Sisi Chadema ni wanasiasa na TAKUKURU wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria inayowangoza, hivyo tutatumia majukwaa ya siasa kuwataja na si kupeleka majina hayo TAKUKURU,`` alisema.

  Kuhusu kutajwa majina ya wamiliki wa kampuni ya Kagoda, Zitto alisema kwa ufupi, ``Mkurugenzi wetu wa kampeni na uchaguzi ameshasema kupitia Alasiri (gazeti dada la Nipashe), hivyo tunasimama katika maneno yake.``

  Akitoa maoni yake kuhusu Chadema kuibua orodha mpya ya mafisadi, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Chiligati, alisema hatua hiyo inapaswa kuungwa mkono kwa kuwa inasaidia jitihada za Rais Jakaya Kikwete kupambana na uovu nchini.

  ``Hawa Chadema wanachokifanya siyo kitu chenye maslahi kwa chama hicho, hiyo ni vita yetu sote, sasa kama wanawajua wao wawataje tu na vyombo vya dola vitafanya kazi zake,`` alisema.

  Chiligati, alisema ni dhana potofu kwa chama kimoja cha siasa kuichukua ajenda ya vita ya ufisadi kama `miliki` yake, kwa kuwa athari zake zinaiathiri jamii nzima.

  Mwaka jana, Chadema katika mkutano uliohudhuriwa na vyama kadhaa vya upinzani, ilitaja majina yaliyopo kwenye orodha ya aibu ya watu wanaojihusisha na vitendo vya ufisadi.

  Hata hivyo, hatua hiyo iliwafanya watu waliotajwa, kujitokeza hadharani na kutaka waombwe radhi, vinginevyo wangemshtaki `kinara` wa kutaja majina hayo, Katibu Mkuu wa Chadema, Wilbroad Slaa.

  Licha ya karipio hilo, Dk. Slaa hakuwahi kuomba radhi, badala yake aliwataka wahusika katika kashfa hiyo, kwenda mahakamani, mahali ambapo ukweli ungejulikana.

  Katika mchakato wa matukio yanayohusiana na vitendo vya ufisadi, mawaziri kadhaa walijiuzulu na baadhi ya watu waliotajwa katika kadhia hiyo, wameshafikishwa mahakamani wakituhumiwa kuhusika katika makosa mbalimbali yenye kuhujumu uchumi na kulitia hasara Taifa.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  CHADEMA wasitishwe tupo nyuma yao!!Tutawasapoti kwa kila jambo!!
   
 3. Kahise

  Kahise Senior Member

  #3
  Jan 12, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 144
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  CHADEMA mwendelee hivyo hivyo kwa kuwa sasa umma wa watanzania wanaelewa mnachokifanya; ufisadi umewaathiri watanzania wengi mno na vita yake itaungwa mkono na kila mmoja wao.

  Darubini ya CHADEMA itakapomaliza kuchunguza kada ya juu, ninaiomba igeukie hata ma-wilayani kwa kuwa mambo yanayofanyika huku nayo ni mchafu.

  Hongera sana CHADEMA!
   
 4. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Chadema endeleeni kuwataja watanzania wanawaunga mkono,watafurahi kuwafahamu wezi zaidi wa rasilimali za TZ.Ikiwezekana muwataja na mali walijilimbikizia ili TAKUKURU wasisingizie kukosa ushahidi.Maana inashanga watu vipato vyao vinajulikana na havilingani na mali walizonazo eti wanataka ushahidi.Chadema juu juu zaidi.
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Mkuu umenena ukweli. Mpaka leo nashangaa kwanini watu hawa-querry uhlali wa mafedha ya mafisadi wa EPA hasa waliokuwa waajiriwa serikalini? Ukiangalia mishahara na marupurupu yote ya waheshimiwa watatu wa EPA aliofikishwa Ukonga utagundua kuwa hata kama wangefanya kazi kwa miaka 100, bado wasingekuwa na mabilioni hayo. Lakini EPA inasema hakuna ushahidi.
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nashauri baada ya kuwataja, uandaliwe utaratibu wa kuwafungulia mashitaka kupitia taratibu za mwendesha mashitaka binafsi. pamoja na kuwa njia hii ina vikwazo vingi sana, lakini itaonyesha dhamira ya dhati waliyokuwa nayo wananchi ya kupambana na ufisadi nchini
   
 7. AbdulKensington

  AbdulKensington Member

  #7
  Jan 12, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo sio kutajwa...tatizo ni kuchukuliwa hatua!
   
 8. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2009
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuwataja ni hatua moja katika kuwachukulia hatua! Kama kweli unadhani tatizo si kuwataja basi nenda kamtaje RA kuwa ndiye mmilika wa Kagoda na dowans pale Jangwani uone kama hakutakuwa na tatizo! Kubenea anapata mataizo sana kwa sababu tu ya kutaja!
   
 9. M

  Masatu JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hii itakuwa "sera" mpya nashauri waitie kwenye ilani yao ya uchaguzi
   
 10. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Nathani bado wanaamini inafanya kazi..
   
 11. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #11
  Jan 12, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hivi chadema hawana mpya zaidi ya neno ufisadi ufisadi ? Huyo zitto hivi mwaka ukiisha atawaeleza nini waliomchagua kama mbunge wao na slaa je ? Chadema angalieni alama za nyakati watu tunataka mabadiliko mambo ya ufisadi ni kazi ya serikali na vyombo vyombo vyake vya sheria sisi tunataka mambo mapya
   
 12. RR

  RR JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo kama ufisadi upo wafunge midomo yao?
  Wana haki ya kusema....wana haki ya kusemea jambo lolote wanaloona ni baya kwa nchi yao!
   
 13. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Mpya ya nini wakati iliyopo haijazeeka??????
   
 14. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwani la ufisadi lina kukera nini wewe..au ndo tuseme umekwisha? Kwamba atawaeleza nini wanachama wake waachie wenyewe pengine wanaridgishwa na utendaji wake...
   
 15. B

  Baba Lao Member

  #15
  Jan 12, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  We dogo angalia sana.watu hatulali kuhakikisha ufisadi unaisha wewe unakuja kuupaka mafuta? Kwanza huna unachoambulia kwa hao mafisadi ,then unapiga makelele tu ili wajue unawasaport.WATANZANIA SI WAJINGA TENA!
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  SHY aka Yona Maro

  1.Mtaalam wa plagiarism

  2. Mtaalam vi-blog

  3. Mtaalam wa kuboa

  4. Mtaalam wa spinning

  Nachelea kuandika 'kibaraka wa CCM'maana nashindwa kuelewa katumwa na nani kati ya wezi/wabadhirifu wa nchi yetu na wale wachovu wa kazi wanaojiita UT Vyovyote ilivyo, nia yake kwa Jambo forums sio nzuri, Mwendapole, 2008
   
 17. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu hapa ninakuunga mguu kwa asilimia 700. Hatujui ni ushahidi gani TAKUKURU wanaohitaji. Ni kiasi cha kumuita mtuhumiwa na kumuuliza jinsi anavyojipatia mali zake hizo. Na mtuhumiwa anatakiwa kutoa documents halisi kuhusu kipato na mali zake, mfano paystub, kodi anazolipa n.k
   
 18. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Haya ndiyo mambo. Tumekuwa tukisikia tu kuwa baadhi ya viongozi wa Upinzani pamoja na wanasheria watamfungulia mashitaka fisadi BWM kama hatafunguliwa mashitaka na serikali. Imekuwa ni lonolongo tu. Hayo mashitaka yamefikia wapi??? Fisadiz wanantakiwa kusogezwa lupango wanakostahili.
   
 19. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Naamini serikali bado ina kigugumizi kwa kushindwa kuwafuatilia wale sangara na badala yake inawafuatilia dagaa. Kama si CHADEMA na viongozi wake kuwataja hawa mafisadi, serikali ingekuwa bado inapiga danadana tu. Hivyo naamini kama kutakuwa na orodha nyingine mpya, wananchi na Taifa kwa ujumla itawajua zaidi wale wanaochangia Taifa hili kuendelea kuwa maskini.
   
 20. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Tanzania tunaoneana haya kuwa wawazi especially kama ni mambo yenye athari kwa PUBLIC. Kwa nini tukae tunaoneana haya au kufumbia macho mambo ambayo yana athari kwa jamii? Kila kitu ooh uchunguzi haujakamilika. Uchunguzi huku unaendelea huku wengine wakizidi kupoteza au kuweka nyongeza katika mafaili. Tuacheni huu uhuni, Taifa linaangamia kwa umaskini. Taifisha mali za fisadiz kisha gawanya kwa wananchi ili nao wafaidi kodi zao.
   
Loading...