CHADEMA na muhuri wa damu katika Taifa lao

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,940
Hakuna chama ambacho kimewahi kuumizwa, kuteswa na kutoa gharama kubwa kwaajili ya ustawi wa Tanzania kama CHADEMA.

Sikuwahi kusikia kama Mwingereza aliwahi kuua viongozi wa TANU wakati wa harakati za kupigania uhuru.

CHADEMA, wakati wa utawala wa Kikwete, walirushiwa bomu lililoua watu wengi kule Arusha. Polisi waliwahi kumwua mwanachama wa CHADEMA kule Morogoro. Kiongozi wa CHADEMA kule Arusha alikatwa shingo kwa chainsew. Alphonce Mawazo, Mwenyekiti wa CHADEMA wa mkoa kule Geita, aliuawa kwa mapanga, na Serikali ya CCM ikawazuia watu wasitoe heshima za mwisho kwa Mawazo.

Pamoja na uovu wote huo, ambao hata TANU haikuwahi kufanyiwa na mkoloni mzungu, CHADEMA hawakukata tamaa, japo kwa majonzi makubwa, waliendelea na mapambano ya kutafuta haki zinazogandamizwa na watawala.

Wakati wa Utawala wa Magufuli, viongozi wa CHADEMA, magereza yakageuzwa kuwa nyumba zao, na mahakama kuwa ndiyo sebule zao. Wengine wakapotezwa mpaka leo. Kiongozi wa CHADEMA akamiminiwa risasi zaidi ya hata ngiri anavyoweza kushambuliwa, Ben Sanane akapotea, madiwani wakauawa.

Ni unyama ambao hata Mwarabu hakuwafanyia watumwa alionunua, ni ushenzi ambao hata mkoloni Mwingereza hakuwahi kuutenda, lakini CHADEMA wamefanyiwa. Ni nani katika hali ya kawaida, angeweza kuyamudu mateso na misiba hii? CHADEMA, kwa sababu ya upendo wao kwa Taifa, japo kwa taabu sana, walisonga mbele.

Wakati wa utawala wa Samia, kuingia tu, alichoona ni muhimu na cha haraka, ilikuwa ni kuwakamata na kuwasweka mahabusu mbalimbali viongozi na wanachama wa CHADEMA. Kisha wakaanza kuwatoa mahabusu taratibu. Mwishoni wakambakiza walitemtaka, Mh. Freeman Mbowe (Mungu amjalie afya njema, maisha marefu, moyo mkuu na ujasiri usiokoma), yeye wakambandika na kesi ya ugaidi. Wanaendelea naye mpaka siku watakapokuwa wameridhika.

Ni chama gani ambacho kimeipigania Tanzania ya demokrasia, haki, uhuru wa maoni na uhuru wa habari, uhuru wa Bunge, na haki ya maendeleo kwa Watanzania, kwa gharama kubwa zaidi ya CHADEMA? Hakika hakuna.

CHADEMA, wanachama na wapenzi wake wametoa damu, na maisha yao kwaajili ya Watanzania. Damu hii na maisha ya wenzetu hao, yasiende bure. Katiba mpya ni lazima, Tanzania ya haki, uhuru na demokrasia ni lazima.
 
CUF ina historia ndefu ya harakati za siasa za upinzani katika nchi hii kuliko chama chochote kingine.

Wewe unalinganisha mateso ya utumwa utadhani ulikuwepo.

Tuonyeshe picha moja tu ya wanachadema wakiwa wamefungwa na minyororo shingoni na miguuni wakipelekwa gerezani wakiwa nusu uchi?

Matukio mengi ya chadema ni orchestra kuliko uhalisia wake.

Mengi yana walakini, na ni yana chain ya kutengenezwa na chadema yenyewe.

Ndio maana mfano, Lissu alishambuliwa ndio.

Hilo halina ubishi.....lakini chadema wametumia gharama zao kumtunza dereva wa Lissu nje ya nchi ili tu asihojiwe au kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola nchini.
Je kwa nini hili linatokea?

Kama anayo siri mnayohofia uhai wake, mbona Lissu hampeleki kwenye taasisi muhimu huko ughaibuni akatowe maelezo?

Amezunguka Dunia nzima na Media zote kubwa, lakini huwa hagusii hili la kukimbia na shahidi muhimu kwenye tukio lake?

Time Will Tell....ndio maana sishangai Mbowe kuwa jela.

Hatujui hao Makomandoo wake ameanza kuwatumia tangia lini?

Huenda wakawa sehemu ya mengi ambayo hatuyajui huku mkichafua serikali.
 
Mkuu umeandika kweli tupu! Tena hayo ni baadhi tu, kuna yaliyofanywa nyuma ya pazia kuhakikisha chadema kinaangamia lakini kiliumia na baadae kikapona!

Mungu ni fundi, nina hakika kuna mabadiliko yatakujatokea ambayo CCM itashindwa kabisa kuyazuia kwa namna yoyote ile!

Itakuwa ni kama mabadiliko ya serikali yaliyotokea mwaka 2021 na kuleta rais wa kwanza Mwanamke ambaye hakuna aliyemtarajia katika hali iliyokuwepo ndani ya CCM! Zipo taarifa kuwa CCM ilijaribu kuhaha huku na kule kutaka kuzuia mabadiliko yale au kuyapindisha lakini kote walikwama, Hatimaye mama akaapishwa kuwa Rais wa JMT!

Hivi ndivyo maono yangu yanavyonionyesha, kuna muda unakuja CHADEMA itaunda serikali ya JMT, na huo utakuwa ni mwisho au kifo cha moja kwa moja cha CCM!

Chama hiki lazima kitakufa kwasababu kimezoea kufanya siasa katika mazingira mepesi huku kikisaidiwa na majeshi na vyombo vyote vya serikali !

Kitakufa haraka kwasababu vyombo hivi vyote vitakata mrija ! na zaidi hakitapata tena fursa na misaada ya kiuchumi kinaypewa na serikali.

Hivyo wapambanaji msikate tamaa kuna saa ya ukombozi inakuja ni muda tu utaamua!
 
CUF ina historia ndefu ya harakati za siasa za upinzani katika nchi hii kuliko chama chochote kingine.

Wewe unalinganisha mateso ya utumwa utadhani ulikuwepo.

Tuonyeshe picha moja tu ya wanachadema wakiwa wamefungwa na minyororo shingoni na miguuni wakipelekwa gerezani wakiwa nusu uchi?

Matukio mengi ya chadema ni orchestra kuliko uhalisia wake.

Mengi yana walakini, na ni yana chain ya kutengenezwa na chadema yenyewe.

Ndio maana mfano, Lissu alishambuliwa ndio.

Hilo halina ubishi.....lakini chadema wametumia gharama zao kumtunza dereva wa Lissu nje ya nchi ili tu asihojiwe au kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola nchini.
Je kwa nini hili linatokea?

Kama anayo siri mnayohofia uhai wake, mbona Lissu hampeleki kwenye taasisi muhimu huko ughaibuni akatowe maelezo?

Amezunguka Dunia nzima na Media zote kubwa, lakini huwa hagusii hili la kukimbia na shahidi muhimu kwenye tukio lake?

Time Will Tell....ndio maana sishangai Mbowe kuwa jela.

Hatujui hao Makomandoo wake ameanza kuwatumia tangia lini?

Huenda wakawa sehemu ya mengi ambayo hatuyajui huku mkichafua serikali.
Haya nenda kachukue buku 7 za lumumba ukalewe kimpumu
 
CHADEMA kitabaki kuwa genge la mhuni Mbowe anayetumia fedha kujijenga kwa mamluki wachache kwa njia mbalimbali kama kushinda mitandaoni. CHADEMA ingekuwa na support ya watanzania kwa kiasi fulani tu kinachoeleweka ingechukua nchi.
Lakini uroho wa madaraka wa Mbowe hauwezi kuipa ushindi CHADEMA, aidha wa kura au mioyo ya watanzania.
Ukiangalia historia ya CHADEMA imejengwa na two pillars;
  1. Imani (trust) ya watanzania kwa baadhi ya watu walioiongoza CHADEMA. Ukiangalia historia Mbowe kagombea urais mara mbili akaishia kupata kura asilimia 0. au chini ya 2! CHADEMA kilipata umaarufu kupitia viongozi wengine kama Zitto lakini kwa kiasi kikubwa sana Dr Slaa. Huyu watu walimtrust wengi na hivyo kuisupport CHADEMA. Lakini cha ziada alichofanya Dr Slaa ni kujenga mifumo ya CHADEMA na kutojijenga yeye binafsi. Ndiyo mana kwenye mgogoro uliopelekea kuondoka CHADEMA aliondoka peke yake bila kutaka kukibomoa chama, lkn leo hii Mbowe huwezi mtoa sababu kajijenga binafsi na kapanga watu wanaomtumikia yeye na siyo chama. Vilevile sababu Dr Slaa aliamini katika kujenga mifumo ndiyo sababu mojawapo iliyofanya CHADEMA ipate angalau kura ilizozipata kwenye uchaguzi wa 2015 na siyo kwamba Lowasa ndiyo alichangia sana kama ambavyo wanadanganya umma.
  2. Chuki iliyopitiliza ya watanzania kwa viongozi na serikali ya CCM ya wakati ule. Ni kweli kweli kwamba viongozi na serikali walikuwa mbali na watanzania sababu walishindwa kutatua kero sugu za watanzania. Rushwa zavwaziwazi, ufisadi, kupeana vyeo kindugu, huduma mbovu za jamii kama afya na elimu, bei za vitu kuwa juu, ukosefu wa ajira, ujambazi uliokithiri, uporaji na utapeli wa wazi mfano watu kuporwa nyumba ilikuwa jambo la kawaida, ubovu wa miundombinu kama barabara na umeme, nk. Kwa kuwabserikali ilionekana dhahiri kushindwa kutatua kero na kukosa dhamira yabwazi, wananchi waliichukia na kiurahisi kugeukia upinzani kupata faraja. Na ukikumbuka vizuri hizi ndiyo zilikuwa sera za upinzani zilizoibeba sana kwa sababu ziligusa mahitaji ya watu(maanake walio wengi).
Sasa baada ya CHADEMA hasa Mbowe kushawishiwa na kununuliwa na fisadi Lowasa, wakazitupa hizo sera zinazogusa mass, kwa tamaa ya kuingia ikulu. Kumbuka walivyodanganywa na Lowasa kuwa eti suala la kura wamuachie yeye, ila ana uhakika wanaingia ikulu.

Baada ya hapo CHADEMA ilibadilika na kukomaa kuwa chama cha ‘kihuni’. Angalia tu hata hapa JF manazi wengi wa CHADEMA ni ‘wahuni’ wanaoamini kwenye kutukana matusi na kudhalilisha kama njia ya kuzima hoja zenye nguvu. Uhuni wa CHADEMA unadhihirika maeneo mengi;
  1. Kuminya demokrasia ndani ya chama. Mbowe ni mwenyekiti wa kudumu kwenye chama cha ‘kidemokrasia’. Kiongozi anayetakiwa na Mbowe ndiye anayepitishwa kugombea iwe kwenye baraza la wanawake, vijana au kokote. Kumbuka ubabe wa bila majadiliano wa kulazimisha wabunge kutohudhuria bunge sababu ya COVID 19.
  2. Kufanya vitendo vya kihuni kisiri na kusingizia ni serikali ilimkuipaka matope. Hata mabomu ya Arusha inaaminika na wengi ni mpango wa wachache CHADEMA, vinginevyo mwambieni Mbowe atoe mkanda wa video uliorekodi tukio zima! Kumbuka wakati wa uchaguzi wa 2020 ofisi za CHADEMA zilikuwa zinatolewa kwanza documents muhimu alafu ndiyo zinachomwa! Au ule uhuninwa kuchapa karatasi feki za kura Dsm na kutangaza tumekamata kura za kughushi za CCM! Wanaita waandihi wa habari, wanawaonyesha kwa mbali hizo kura na kisha wanaenda kuzichoma kisiri. Walijua wakiziacha watu waziangalie kiundani itajulikana wamefoji sababu zilikuwa tofauti. Lakini kilele cha uhuni na kuumbuka ni kesi ya Mbowe ya ugaidi. Hii ndiyo imedhihirisha wazi CHADEMA ilikuwa inatumia mbinu gani katika maisha yake hasa baada ya kuishiwa sera kuanzia 2015 na Magufuli kuwa karibu na wananchi kwa kutatua kwa kasi na kuonyesha nia thabiti ya kuendelea kutatua kero za wananch.
 
CHADEMA kitabaki kuwa genge la mhuni Mbowe anayetumia fedha kujijenga kwa mamluki wachache kwa njia mbalimbali kama kushinda mitandaoni. CHADEMA ingekuwa na support ya watanzania kwa kiasi fulani tu kinachoeleweka ingechukua nchi.
Lakini uroho wa madaraka wa Mbowe hauwezi kuipa ushindi CHADEMA, aidha wa kura au mioyo ya watanzania.
Ukiangalia historia ya CHADEMA imejengwa na two pillars;
  1. Imani (trust) ya watanzania kwa baadhi ya watu walioiongoza CHADEMA. Ukiangalia historia Mbowe kagombea urais mara mbili akaishia kupata kura asilimia 0. au chini ya 2! CHADEMA kilipata umaarufu kupitia viongozi wengine kama Zitto lakini kwa kiasi kikubwa sana Dr Slaa. Huyu watu walimtrust wengi na hivyo kuisupport CHADEMA. Lakini cha ziada alichofanya Dr Slaa ni kujenga mifumo ya CHADEMA na kutojijenga yeye binafsi. Ndiyo mana kwenye mgogoro uliopelekea kuondoka CHADEMA aliondoka peke yake bila kutaka kukibomoa chama, lkn leo hii Mbowe huwezi mtoa sababu kajijenga binafsi na kapanga watu wanaomtumikia yeye na siyo chama. Vilevile sababu Dr Slaa aliamini katika kujenga mifumo ndiyo sababu mojawapo iliyofanya CHADEMA ipate angalau kura ilizozipata kwenye uchaguzi wa 2015 na siyo kwamba Lowasa ndiyo alichangia sana kama ambavyo wanadanganya umma.
  2. Chuki iliyopitiliza ya watanzania kwa viongozi na serikali ya CCM ya wakati ule. Ni kweli kweli kwamba viongozi na serikali walikuwa mbali na watanzania sababu walishindwa kutatua kero sugu za watanzania. Rushwa zavwaziwazi, ufisadi, kupeana vyeo kindugu, huduma mbovu za jamii kama afya na elimu, bei za vitu kuwa juu, ukosefu wa ajira, ujambazi uliokithiri, uporaji na utapeli wa wazi mfano watu kuporwa nyumba ilikuwa jambo la kawaida, ubovu wa miundombinu kama barabara na umeme, nk. Kwa kuwabserikali ilionekana dhahiri kushindwa kutatua kero na kukosa dhamira yabwazi, wananchi waliichukia na kiurahisi kugeukia upinzani kupata faraja. Na ukikumbuka vizuri hizi ndiyo zilikuwa sera za upinzani zilizoibeba sana kwa sababu ziligusa mahitaji ya watu(maanake walio wengi).
Sasa baada ya CHADEMA hasa Mbowe kushawishiwa na kununuliwa na fisadi Lowasa, wakazitupa hizo sera zinazogusa mass, kwa tamaa ya kuingia ikulu. Kumbuka walivyodanganywa na Lowasa kuwa eti suala la kura wamuachie yeye, ila ana uhakika wanaingia ikulu.

Baada ya hapo CHADEMA ilibadilika na kukomaa kuwa chama cha ‘kihuni’. Angalia tu hata hapa JF manazi wengi wa CHADEMA ni ‘wahuni’ wanaoamini kwenye kutukana matusi na kudhalilisha kama njia ya kuzima hoja zenye nguvu. Uhuni wa CHADEMA unadhihirika maeneo mengi;
  1. Kuminya demokrasia ndani ya chama. Mbowe ni mwenyekiti wa kudumu kwenye chama cha ‘kidemokrasia’. Kiongozi anayetakiwa na Mbowe ndiye anayepitishwa kugombea iwe kwenye baraza la wanawake, vijana au kokote. Kumbuka ubabe wa bila majadiliano wa kulazimisha wabunge kutohudhuria bunge sababu ya COVUD 19.
  2. Kufanya vitendo vya kihuni kisiri na kusingizia ni serikali ilimkuipaka matope. Hata mabomu ya Arusha inaaminika na wengi ni mpango wa wachache CHADEMA, vinginevyo mwambieni Mbowe atoe mkanda wa video uliorekodi tukio zima! Kumbuka wakati wa uchaguzi wa 2020 ofisi za CHADEMA zilikuwa zinatolewa kwanza documents muhimu alafu ndiyo zinachomwa! Au ule uhuninwa kuchapa karatasi feki za kura Dsm na kutangaza tumekamata kura za kughushi za CCM! Wanaita waandihi wa habari, wanawaonyesha kwa mbali hizo kura na kisha wanaenda kuzichoma kisiri. Walijua wakiziacha watu waziangalie kiundani itajulikana wamefoji sababu zilikuwa tofauti. Lakini kilele cha uhuni na kuumbuka ni kesi ya Mbowe ya ugaidi. Hii ndiyo imedhihirisha wazi CHADEMA ilikuwa inatumia mbinu gani katika maisha yake hasa baada ya kuishiwa sera kuanzia 2015 na Magufuli kuwa karibu na wananchi kwa kutatua kwa kasi na kuonyesha nia thabiti ya kuendelea kutatua kero za wananch.
Maelezo mengii alafu yote upupu.Mtaunga unga sana stori ila lazima ujue ndo zama zinawakimbia hivyo.
 
CUF ina historia ndefu ya harakati za siasa za upinzani katika nchi hii kuliko chama chochote kingine.

Wewe unalinganisha mateso ya utumwa utadhani ulikuwepo.

Tuonyeshe picha moja tu ya wanachadema wakiwa wamefungwa na minyororo shingoni na miguuni wakipelekwa gerezani wakiwa nusu uchi?

Matukio mengi ya chadema ni orchestra kuliko uhalisia wake.

Mengi yana walakini, na ni yana chain ya kutengenezwa na chadema yenyewe.

Ndio maana mfano, Lissu alishambuliwa ndio.

Hilo halina ubishi.....lakini chadema wametumia gharama zao kumtunza dereva wa Lissu nje ya nchi ili tu asihojiwe au kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola nchini.
Je kwa nini hili linatokea?

Kama anayo siri mnayohofia uhai wake, mbona Lissu hampeleki kwenye taasisi muhimu huko ughaibuni akatowe maelezo?

Amezunguka Dunia nzima na Media zote kubwa, lakini huwa hagusii hili la kukimbia na shahidi muhimu kwenye tukio lake?

Time Will Tell....ndio maana sishangai Mbowe kuwa jela.

Hatujui hao Makomandoo wake ameanza kuwatumia tangia lini?

Huenda wakawa sehemu ya mengi ambayo hatuyajui huku mkichafua serikali.
Hujui lolote wewe,zaidi yakupiga porojo tu.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Chadema;
wameteswa
wameonewa
wamebakiziwa makesi
wameumizwa
wamedhulumiwa 'maisha yao'
Lakini waliowafanyiwa hivi wako wapi leo? na walio hai wako ktk nmateso ya laana mbaya sana
 
Back
Top Bottom