CHADEMA na mawasiliano kwa umma

CHADEMA na mawasiliano kwa umma

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,065
Reaction score
136,448
Miezi miwili iliyopita niliwasihi CHADEMA wabadilishe kauli mbiu yao ya ‘no reforms, no elections’ na waache kusema [hususan mwenyekiti wao mpya] watauzuia uchaguzi kufanyika endapo hakutakuwepo mabadiliko ya namna chaguzi zetu zinavyofanyika.

Kusema mtauzuia uchaguzi kufanyika endapo hakutakuwepo na mabadiliko ni rahisi sana kutafsiriwa kivingine na mtu yeyote yule. Na hicho ndo kimepelekea Lisu kukamatwa na kuwekwa kizuizini.

Kutoa kauli za namna hiyo [zenye kutafsirika kwa namna mbalimbali] kunairahisishia kazi CCM na serikali yake, ya kuwabana kuwa mnachochea vurugu.

Kwenye harakati kama hizi za kisiasa, moja ya kanuni kubwa zaidi ni kutokumrahisishia kazi mpinzani wako.

Kwa kutumia mfano wa mchezo wa mpira wa miguu, usijifunge magoli wewe mwenyewe au usicheze rafu kwenye eneo la penati au kwenye eneo la mita kumi na nane.

Sasa, CCM na serikali yake huwezi kuihusisha sana na matumizi ya akili kwa namna wanavyoiendesha nchi.

Lakini, hiyo isiwe sababu ya kuirahisishia kazi yao ya unyanyasaji.

Itakuwa vyema endapo huu uongozi mpya wa CHADEMA utaliangalia kwa maanani stahilifu hili suala la mawasiliano kwa umma.

Sijui idara yao ya mawasiliano ina watu gani na wenye sifa zipi.

Ila kwa kinachoendelea mpaka sasa naweza kusema idara hiyo bado ina nafasi kubwa na pana ya uboreshwaji.

Wataalamu wa mawasiliano kwa umma tupo. Just reach out and we’ll offer our helping hand in your messaging.

Happy Easter.
 
Mkuu hujatoa ushauri Nini kingepaswa kufanyika,umekosoa tu kilichofanyika, approach nzuri ni ipi ili mamlaka zielewe kua upinzani wamechoka wizi??
 
Mbona nimeshasema kuwa hiyo kauli ilipaswa kubadilishwa.

Au hujaelewa nilichokiandika?
 
Miezi miwili iliyopita niliwasihi CHADEMA wabadilishe kauli mbiu yao ya ‘no reforms, no elections’ na waache kusema [hususan mwenyekiti wao mpya] watauzuia uchaguzi kufanyika endapo hakutakuwepo mabadiliko ya namna chaguzi zetu zinavyofanyika.

Kusema mtauzuia uchaguzi kufanyika endapo hakutakuwepo na mabadiliko ni rahisi sana kutafsiriwa kivingine na mtu yeyote yule. Na hicho ndo kimepelekea Lisu kukamatwa na kuwekwa kizuizini.

Kutoa kauli za namna hiyo [zenye kutafsirika kwa namna mbalimbali] kunairahisishia kazi CCM na serikali yake, ya kuwabana kuwa mnachochea vurugu.

Kwenye harakati kama hizi za kisiasa, moja ya kanuni kubwa zaidi ni kutokumrahisishia kazi mpinzani wako.

Kwa kutumia mfano wa mchezo wa mpira wa miguu, usijifunge magoli wewe mwenyewe au usicheze rafu kwenye eneo la penati au kwenye eneo la mita kumi na nane.

Sasa, CCM na serikali yake huwezi kuihusisha sana na matumizi ya akili kwa namna wanavyoiendesha nchi.

Lakini, hiyo isiwe sababu ya kuirahisishia kazi yao ya unyanyasaji.

Itakuwa vyema endapo huu uongozi mpya wa CHADEMA utaliangalia kwa maanani stahilifu hili suala la mawasiliano kwa umma.

Sijui idara yao ya mawasiliano ina watu gani na wenye sifa zipi.

Ila kwa kinachoendelea mpaka sasa naweza kusema idara hiyo bado ina nafasi kubwa na pana ya uboreshwaji.

Wataalamu wa mawasiliano kwa umma tupo. Just reach out and we’ll offer our helping hand in your messaging.

Happy Easter.
uongozi mpya wa chadema umejaa makhalakhancha tupu, hawana maono kabisaa, ni kanyaga twende tu bora liende 🐒
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Mbona No Reforms, No Election imeeleweka kwa wengi, Hakuna lugha laini wala ya kistaarabu kwa dhlumati, wao wakiamua kuteka na kuua hawaui kwa ustaarabu wanaua kabisa.

Lugha hiyo imefanya wasikae ofisini kwa amani wakafikiri kumkamata Lissu watapunguza joto kumbe ndio wamemwaga mafuta juu ya moto.

Bila hii lugha CCM wangeendelea ku relax.
 
No reform no election elewa

Mwaka huu Kama hakuna Sheria nzuri za uchaguzi hakuna uchaguzi

Mwezi wa 6 tunaanza maandamano yasiyo na kikomo kila kata nchi nzima !!
Mtauzuiaje uchaguzi kutokufanyika?
 
Kuzuia huwezi, maana ni haki ya kikatiba, ila kwa mtu mwenye akili timamu sidhani kama kuna haja ya kwenda kupanga foleni unachomwa jua eti unapiga kula
 
No reform no election elewa

Mwaka huu Kama hakuna Sheria nzuri za uchaguzi hakuna uchaguzi

Mwezi wa 6 tunaanza maandamano yasiyo na kikomo kila kata nchi nzima !!
Mimi naunga mkono hiyo no reform no election, lakini kiamini watanzania wataandamana kwa wingi hilo siamini naona muda bado sana wa muamko wa namna hiyo. Yakiwezekana kipindi hiki ntastaajabu kwa mshangao mkubwa
 
Back
Top Bottom