CHADEMA na Lowassa kwa Ushindi huu wa Raila Odinga mtaweka wapi sura zenu?

Nimeshangazwa na maandiko ya hawa ndgu zetu likiweko la Mtatiro. Mnachanganya sana, aliposhinda Kenyatta mlikuwa wa kwanza kupongeza wakati Nasa wanalalamika kuibiwa, tena mkasema Odinga hajaibiwa atulie, leo matokeo yametupiliwa mbali mmekuwa tena mle mle na kudai demokrasia imetumika hivi nyie mko upande gni? My take tukio la jana mi naliona kma lina +ve impact kwa upande wa ukawa ambayo inataka demokrasia ya ukweli na kule kuunga mkono kwa kwanza kubalini kuwa mlipotea..nawakilisha.
Hakuna kitu kibaya sana katika maisha ya binadamu kama kuwa VUGUVUGU. Ni bora mtu Uwe baridi au moto. WanaSiasa wanatupotezea muda wetu Watanzania.
 
Juzi Esther Bulaya ameshinda kesi ya ubunge dhidi ya Steven Wasira. Unasemaje hapo
kushinda kesi kwa Bulaya siyo sababu ya kusema mahakama ni huru.
tunapojadili haya mambo lazima tuangalie kwa undani mfumo mzima wa mahakama unapatikanaje. na kama unaweza kuwa na uhuru wa kutosha bila kushawishiwa na nguvu kutoka nje. hapa ni wenye akili tu wanaweza kuelewa hii.nyie magamba itakuwa ngumu
 
jaribu kufungua kidogo ubongo wako.kinachozungmzwa na chadema ni mfumo wa mahakama ya kenya kutoa maamuzi bila kushinikizwa na serikali iliyoko madarakani.na Chadema haija withdraw statement ya kumuunga mkono Kenyatta hata uchaguzi ukifanyika kesho na uhuru akashinda Chadema itampongeza na akishindwa watampa pole.
Hivi hizo shule mlienda kusomea Ujinga.? (FF)
Esther Bulaya kamgaragaza Wassira ( Mahakama zimetenda haki)
Lijualikali alishinda rufani yake ( Mahakama imetenda haki)
Ni wapi kuna shinikizo la serikali kwa Mahakama?
 
Esther Bulaya kamgaragaza Wassira ( Mahakama zimetenda haki)
Lijualikali alishinda rufani yake ( Mahakama imetenda haki)
Ni wapi kuna shinikizo la serikali kwa Mahakama?
Hata Lissu kufunguliwa mashtaka na kushinda kesi mahakama imetenda haki. lakini nakuuliza Je mahakama kumkingia kifua Prof Lipumba na kushindwa kusikiliza mashauri ya wabunge 9 wa CUF waliofukuzwa na Lipumba hapo kuna Haki.
 
Hata wakubwa wetu hawaongelei hilo zaidi ya matusi. Unajua upinzani wameridhika sana?

Upinzani wtu unapambana na mtu na si mfumo. Angalia wanavyolalamika badala ya kuongoza wanachotaka.

Odinga anapambana kwa hoja na sera si kuamka na matamko kila siku ya watu binafsi. Tunaua chama kwa kutotaka kufikiri.
Pamoja na usanii wa Chadema kama unavyodai jiulize kwanini chama cha wahuni na mafisadi wanaihofia katiba mpya ya rasimu ya Warioba na Tume huru ya uchaguzi!?
Jibu ni kwamba wanajua ndiyo itakuwa kiama chao kwenye anga za siasa nchini na hata katibu mwenezi wa chama cha wahuni na mafisadi anajua fika.

 
Korti ya kenya haijasema Uhuru ameiba wamesema tume haikufuata procedure. Na nina imani tu kuwa Uhuru bado atashinda kwani NASA ni timu tu ya wafanyi biashara waliounda NASA kwa nia ya kula nchi. Wakimchagua Kenya itapata hasara kubwa. Kenya wako mbele sasa kwenye democrasia kuliko nchi zote za Africa. Na Tz iko nyuma 50 yrs. Hata ukiwasikiliza waandishi wao na watu wao wanavyojadili mambo katika media utaona kuwa wako hatua nyingine.
 
Kutenguliwa kwa ushindi wa Uhuru ni ushindi kwa Africa nzima kwani ndiyo mwanzo wa democrasia Africa. CHADEMA walifurahia Uhuru ashinde kwa kuwa tu Odinga ni rafiki wa rais wetu. Inaeleweka. Lakini kumhusisha Lowassa na procedures za Kenya ni kukosa akili.
 
Chadema wawe na wasiwasi gani wakati Uhuru atashinda tena.Kwa ukomavu wa kisiasa aliouonyesha hata wale ambao hawakumpigia mwanzoni watampigia
 
Tatizo Lako ni ufinyu wa fikra! Tunaunga Jubilee kwa kuwa utawala wa Tanganyika unaunga NASA. Na tutaendelea kuiunga jubilee kwa kuwa Kenyatta ni mwanademokrasia na anajiamini. Tofauti na watawala wengine wa EA BAADA ya uchaguzi aliruhusu maandamano na mikutano kama katiba inavyotaka. Aluta kontinua Kenyatta.
kwa kweli ndugu hujielewi..siasa za hisia na mihemko mbele akili nyuma...tatizo chadema mnaenda na hisia sana kuliko akili....nyie mnaweza kunywa coca kisa tu mmemuona JPM kanywa pepsi yaani basi tu muoneshe upinzani tu ndio fahari yenu...hichi chama kuna watu wachache wamewashika mapembe na nyie bila kujielewa mnaenda tu...hii hii ccm mnayoipinga ndio leo imewapa watu wanowashika mapembe.....chadema ya kweli ni ile ya zamani sio hii ya sasa hivi
 
Post kama hizi zina-summarize mawazo yetu wabongo,sijasikia wanyarwanda waganda wala warundi wakshoboka na mambo ya uchaguzi ya Kenya,sina upande wowote lakini Ashinde odinga ashinde Kenyatta mimi muuza mahindi Manzese,yule fundi Tv kariakoo kunamsaidia nn...hizi tabia za Umbea ziko hadi chini huko majumbaNi kwetu,odinga hajashinda uchaguzi ameshinda rufaa,kenyatta hana kosa au kesi ya kujibu according to The Supreme court....tunachagua pande kama Timu za EpL bhana.......hebu tupambane na hali zetu...
Well said

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeleta ili muunganishe kwa mara ya tatu leo. Mnalinda ufuasi wa vyama!!!!

CHADEMA ilijipambanua wazi kuungana na mwizi Uhuru kwa keti dhaifu sana ya kumkomoa Raila.
Wengi walisema, imekosea. Imekosea kwa sababu wao ni wapinzani na si watawala.

Nasema CHADEMA ni aibu na wanatetea wezi kwa kiwango hiki. Tunawambia kila siku, chama kisiendeshwe na mtu ila sera za pamoja na zinazojisema zenyewe. Kitendo cha Lowassa kutaka kutumia chama kujitukuza matokeo yake ni kukosa mwelekeo.

Lowassa anatafuta utukufu wake binafsi na sasa matokeo yake tunaona.

Mfumo huu wa CHADEMA wa kutetea hata uovu iwe fundisho.

Mwenyekiti aamuke na kuendesha chama kama taasisi na si matamko ya watu au fikra zao.


Siamini kama yupo mwana chama wa ccm anayeweza kufurahia kile kilichotekea Kenya cha Urais kutenguliwa mahakamani wakati wao hawataki katiba mpya yenye kipengele cha kuhoji ushindi wowote ambao umetangazwa na tume ya uchaguzi kuhusu ushindi wa Rais.
Ni wao ambao wanaamini kuwa hupo muhimili mmoja wenye uwezo kuliko mingine yote na kukubaliana na JPM kupiga marufuku mikutano kinyume cha katiba ya nchi. Ni wao wanaomshangilia pale anapopinga maamuzi ya mahakama ya kuzuia bomoabomoa iliyo kinyume na sheria. Ni wao wanaofurahia ukandamizaji wa demokrasia nchini.

Sijui wataanzia wapi kufurahia kilichofanyika Kenya maana kimezaliwa na demokrasia wanayoikataa kila siku. Kimetokana na mahakama kuwa huru bila kuingiliwa na maagizo toka juu. Hivi wamejifunza nini wanachama wa ccm kuhusu umuhimu wa demokrasia kutamalaki ndani ya nchi.

Hata hivyo pongezi nyingi ziende kwa Uhuru anayejua maana ya utawala bora na sheria na ambaye ni mmoja wa viongozi wanaoheshimu katiba za nchi zao. Je ccm mpo tayari kumshauri JPM?
 
Akili za brn

Mwambie uchwara aige yafuatayo kutoka kenya

1. Asiingilie uhuru wa mahakama

2. Aheshimu na kuitii katiba

3. Afuate na kuziheshim sheria

Nakwamba yeye siyo Mungu..... Nimtumishi wetu...hivyo asivunje katiba atuheshimu kwakutenda haki.
Heshimu mamlaka iliyopo ndugu, hata vitabu vitakatifu vinatuasa hivyo.
 
Heshimu mamlaka iliyopo ndugu, hata vitabu vitakatifu vinatuasa hivyo.

Mamlaka ya haki huheshim katiba na watu wake

Sasa hivi tunahitaji

1. Katiba mpya ya warioba

2. Tume huru ya uchaguzi

3. Uhuru wa kuhoji mahakamani ushindi usiolidhisha wa rais

UTAIFA KWANZA.....katiba mpya msingi wa usawa, haki na umoja

Uzalendo, kwanza dai katiba mpya ya warioba
 
Screenshot_2017-09-01-18-07-39.png
Je waungwana hawa baada ya kuona upepo umebadilika je na wao watabadilika?

Naamini Chadema ilishinikizwa kuchukua upande wa Uhuru kwa kuwa Mnunuzi wa Chama alitaka iwe hivyo ...je baada ya upepo kubadilika je watajorudi na kuja na tamko jipya au watapotezea?
 
..kwani "mcha mungu" yuko upande gani?

..kama bado anaendelea kumuunga mkono Raila basi CDM watakuwa upande wa Uhuru.
 
Back
Top Bottom