Kuelekea 2025 Hongera CHADEMA kwa uchaguzi huru na haki, sijasikia tukio la wizi wa kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
17,727
27,212
Salaam, shalom!!

Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu uchaguzi unaendelea wa Kanda, mchuano ni mkali na leo tumeshuhudia Mh Sugu akiibuka mshindi Kwa tofauti ya kura mbili pekee.

Jambo jingine, sijasikia kura kuharibika, hili linaonesha kuwa uelewa wa wapiga kura CHADEMA ni WA kiwango Cha juu.

Nimefurahishwa pia na kauli ya Makamo Mwenyekiti wa CHADEMA ndugu TUNDU Lisu kukemea hadharani matumizi ya pesa chafu katika mchakato mzima wa uchaguzi wa chama chake.

Jambo lingine zuri ni kuwa, sijasikia matukio ya wizi wa kura, kura kuzidi idadi ya wapiga kura, Wala sijaona polisi wakisimamia masanduku ya kura Kwa mitutu ya bunduki.

NEC ijifunze DEMOKRASIA na uhuru wa uchaguzi uliooonyeshwa na CHADEMA. Kwa waliotegemea mkono uanguke kama fisi, pole Yao.

Kwa kilichotokea katika chaguzi hizi zinazoendelea za CDM, wananchi wanatakiwa KUIAMINI pasi na shaka CDM katika chaguzi zijazo Kwa kuwa wameonyesha matumaini ya kuheshimu SANDUKU LA KURA ambalo likiheshimiwa, hutoa viongozi Bora.

Mungu ibariki CHADEMA ✊

Mungu Ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

PIA SOMA:
- Kuelekea 2025 - Joseph Mbilinyi (Sugu) ashinda uchaguzi Kanda ya Nyasa, amgaragaza Mchungaji Msigwa
 
Ila kuna mtu kapewa lifti mpaka makambako ndio zile kura 2!
Hujaelewa,

Kule CCM, wanaweza kupiga kura watu 2000, Cha kushangaza, zikihesabiwa kura, mgombea mmoja akapata kura 1500, akafuatiwa na mshindi wa pili mwenye kura 800, na zikaharibika kura 50.

Na pamoja na Kutokea mshangao huo, Bado hawawezi kufuta uchaguzi.
 
Huko ccm unakuta watu wazima na elimu zao eti mtu anapata kura 100% bila hata kura Moja ya hapana Wala kuharibika! Na watu wanachekacheka kuwa ni ushindi wa kishindo. Huu ndio uchaguzi wa kweli, umejaa ubora na matokeo yanayoakisi uhalisia
Kuharibika Kwa kura pia ni kiashiria kuwa,

Chama hakijatoa Elimu ya kutosha ya Uraia Kwa wapiga kura.
 
Salaam, shalom!!

Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu uchaguzi unaendelea wa Kanda, mchuano ni mkali na Leo tumeshuhudia Mh Sugu akiibuka mshindi Kwa tofauti ya kura mbili pekee.

Jambo jingine, sijasikia kura kuharibika, hili linaonesha kuwa uelewa wa wapiga kura CHADEMA ni WA kiwango Cha juu.

Jambo lingine zuri ni kuwa, sijasikia matukio ya wizi wa kura, kura kuzidi idadi ya wapiga kura, Wala sijaona polisi wakisimamia masanduku ya kura Kwa mitutu ya bunduki.

NEC ijifunze DEMOKRASIA na uhuru wa uchaguzi uliooonyeshwa na CHADEMA. Kwa waliotegemea mkono uanguke kama fisi, pole Yao.

Mungu ibariki CHADEMA

Mungu Ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Watu wamechapana sana iringa ulikuwa nje ya nchi ndg ,hawa jamaa hawaaminiani hata wenyewe ,vitasa vimetembea sana
 
Back
Top Bottom