CHADEMA na hatua tatu mbele hatua kumi nyuma

CHADEMA na hatua tatu mbele hatua kumi nyuma

Hata
Wasalaamu kwa GTs na Makapuku kama mnavyotaka kuitwa.

CHADEMA ILIPIGA HATUA TATU MBELE NA SASA IMERUDI HATUA KUMI NYUMA....Ni masikitiko kwa wanasiasa wote iwe ni ndani ya CCM au nje ya CCM.

CHADEMA iliogopwa na Mwalimu Nyerere pindi ilivyoanzishwa kiasi cha kuonekana kuwa kinaweza kuwa chama chenye sera bora ndani ya upinzani(hapa simaanishi ubora wa kushika dola hapana bali ni ubora wa kuwa wapinzani wenye kuleta hoja mbadala za kimaendeleo na kiustawi katika taifa)

Hii ilikuwa ni hatua ya kwanza mbele.

CHADEMA ilikuwa ni Chama chenye uvumilivu na kinachoamini kwenye kujipanga zaidi.kwa miaka kadhaa kilikuwa kinajipanga kwa kufanya siasa za utulivu na kilianza kuwekeza katika kupata wanachama wasomi watakaokipeleka chama mbele na kukiimarisha.hili lilifanyika kimya kimya bila vurugu za maandamano vyuoni ...kina John Mnyika,Zitto kabwe na wengine ndivyo walivyoweza kuibuliwa kwa utaratibu huu.

CHADEMA ilijitahidi kuwekeza kwa kundi la wasomi zaidi ukilinganisha na NCCR iliyokuwa imejikita kwa vibaka,mama ntilie,wamachinga na wahuni wa mijini.Pia hapa tunaiona CHADEMA ikiibuka na agenda muhimu kama Chama yaani "VITA DHIDI YA UFISADI" Hapa ndipo vichwa vitano bungeni akiwemo Zitto,Mnyika,Slaa,Wangwe waliposumbua serikali bila kususa bungeni au kupayuka mambo wasiyokuwa na ushahidi bungeni.

Hii ilikuwa ni hatua ya pili mbele!!

Uwekezaji mkubwa wa CHADEMA kwenye siasa za mitaani na vijijini ulikuja baada ya uchaguzi wa 2010.kwani somo walilolisoma la kwamba kura hazipo kwenye propaganda za mitandaoni ai magazetini bali zipo kwenye level ya nyumba kumi kumi.

Hapa ndipo unaweza kuuona weledi wa katibu mkuu aliyepumzika siasa Dr Slaa alivyoanza kuwa tishio la dhahiri dhidi ya mfumo wa CCM.Dr Slaa alianza kuijenga CHADEMA kama vile anaeneza kanisa katoliki duniani...alianza kujenga matawi mitaani na vijijini

yaani lilipo tawi la CCM basi pembeni lipo la CHADEMA...kiukweli hii ndio iliyokuwa hatari kubwa kwa CCM kiasi Cha Kinana kuitwa na kuja kuandaa operesheni ya kisiasa iliyotukuka.

Hii Ilikuwa ni hatua ya tatu Mbele...!.###############$#

CHADEMA NA KIZUNGUZUNGU /KIHINDI HINDI

Ama kweli ngoma ya kitoto haikeshi..
CHADEMA ikaanza kurudi hatua zaidi ya tatu nyuma !!
CHADEMA ikaacha kuenenda na katiba yake au sera zake wakati inaaanzishwa.
CHADEMA ikaacha kujadili hoja badala yake ikawa ni mtaalamu wa kutengeneza vihoja bungeni na mitaani ili tu isikike.

CHADEMA ikakosa uvumilivu wa kisiasa na kujipanga .
CHADEMA ikaanza kupeleka siasa vyuoni badala ya kuchukua wasomi kutoka vyuoni ili waje kukijenga Chama.
CHADEMA ikaachana na wasomi na wafanyakazi badala yake ikaanza kuwekeza kwa masela na wanywa viroba wanaoweza kununuliwa na kufagia barabara.

CHADEMA IKAPOTEZA AJENDA YA MSINGI WA CHAMA yaani vita dhidi ya ufisadi kwa kumpokea waliyemtuhumu kuwa ni fisadi na kuanza kumtetea kwa nguvu zote.
CHADEMA ikafuta list of shame kwenye website yao...
CHADEMA ikaanza kumpinga hata Rais anayepambana na ufisadi.
CHADEMA ikaanza kuwatetea wafanyabiashara wasiolipa kodi.

CHADEMA ikaanza kuwaunga mkono wafanyabiashara wa sukari wanaohujumu uchumi
CHADEMA ikaanza kuweweseka kwa kurukia kila hoja.
CHADEMA ikaanza kuingiza bungeni wabunge wa viti maalum kwa kufuata uswahiba .

CHADEMA ikkakosa hoja na badala yake ikaanza kudususa kikekike...yaani siku wakimshutikia Tulia Ackson yuko ndani ya ndege na ndege ipo angani basi wataomba kushuka.
CHADEMA ikawa Chama cha kambale yaani kila mtu ana sharubu...haijulikani katibu mkuu ni Lowassa au Mwalimu au Mbatia au Silinde kila mmoja anatoa maelekezo tu.

Hebu niishie hapa na niwakaribishe muendelee kutaja hatua kumi zaidi walizopiga CHADEMA kuelekea reverse.

TUWASAIDIE WAPINZANI WASIFE KWA AFYA YA TAIFA
Hata viongozi wako wa ccm walisema haya haya miaka ya nyuma na wasira kutabiri cdm haitafika 2013 leo wanashangaa madiwani, wabunge na halmashauri zilizo chini ya cdm zinaingezeka sasa wameamua kusigina demokrasia
 
Hata

Hata viongozi wako wa ccm walisema haya haya miaka ya nyuma na wasira kutabiri cdm haitafika 2013 leo wanashangaa madiwani, wabunge na halmashauri zilizo chini ya cdm zinaingezeka sasa wameamua kusigina demokrasia
Walisema viongozi ....lakini mimi kama GT sikuwahi kusema na sasa nimeamua kusema...
 
Jesc@ au mwendokasi katika ubora wako!
Hapo ni blah blah,hakuna hoja kabisa!itabidi ujibiwe hivyo hivyo kiblablah!
Cdm ina uwakilishi mkubwa bungeni kuliko wakati wowote kwenye historia ya chama,mpaka hapo hoja yako ni mufilisi.Mwisho wa kujadili
 
Chadema kimepoteza dira , wamelamba matapishi wakengeukaji . hatutawaamini tena . bye bye ufipa
 
Tujadili hoja...nipinge kwa kupangua hoja na sio vihoja...hivi vihoja ndizo hatua kumi za rivasi nilizozisema ...yaani hata watetezi wa CHADEMA mitandaoni ndio style hii ya kivituko vituko aka wazee wa special diploma
Nimeipenda hiyo wazee wa diploma
 
Hesabu kwako ni shida sana, hivi kati ya cdm na ccm nani anazidi kurudi nyuma kila kukicha?tangu chadema imeanzishwa inazidi kuongeza idadi ya wabunge kila uchaguzi na ccm inapoteza kila wabunge kila uchaguzi, hapo nani anarudi nyuma?

Tatizo mmepokea matapishi na kunyofoa ile list of shame.
 
Jesc@ au mwendokasi katika ubora wako!
Hapo ni blah blah,hakuna hoja kabisa!itabidi ujibiwe hivyo hivyo kiblablah!
Cdm ina uwakilishi mkubwa bungeni kuliko wakati wowote kwenye historia ya chama,mpaka hapo hoja yako ni mufilisi.Mwisho wa kujadili
Hoja yangu imegusia maeneo mengi sana ...pangua hoja kwa kila eneo husika.......

Uwakilishi huu unaouita mkubwa ni uwakilishi dhaifu sana kulinganisha na uwakilishi wa 2005 uliomuondoa Lowassa 2008.
 
Hoja yangu imegusia maeneo mengi sana ...pangua hoja kwa kila eneo husika.......

Uwakilishi huu unaouita mkubwa ni uwakilishi dhaifu sana kulinganisha na uwakilishi wa 2005 uliomuondoa Lowassa 2008.
KUJUMLISHA NA KUTOA KWAKO NI SHIDA SANA!, gamba wewe
 
sasa mnaendelea kuchukua oil chafu
 
umetaja CHADEMA mara 25. kwelii chadema inakufanya uweweseke na kukunyima usingizi.
polee ila chunga CHADEMA isije ikakuletea magonjwa ya HIGH BP Na KISUKARI
 
Back
Top Bottom