jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,141
- 29,670
Wasalaamu kwa GTs na Makapuku kama mnavyotaka kuitwa.
CHADEMA ILIPIGA HATUA TATU MBELE NA SASA IMERUDI HATUA KUMI NYUMA....Ni masikitiko kwa wanasiasa wote iwe ni ndani ya CCM au nje ya CCM.
CHADEMA iliogopwa na Mwalimu Nyerere pindi ilivyoanzishwa kiasi cha kuonekana kuwa kinaweza kuwa chama chenye sera bora ndani ya upinzani(hapa simaanishi ubora wa kushika dola hapana bali ni ubora wa kuwa wapinzani wenye kuleta hoja mbadala za kimaendeleo na kiustawi katika taifa)
Hii ilikuwa ni hatua ya kwanza mbele.
CHADEMA ilikuwa ni Chama chenye uvumilivu na kinachoamini kwenye kujipanga zaidi.kwa miaka kadhaa kilikuwa kinajipanga kwa kufanya siasa za utulivu na kilianza kuwekeza katika kupata wanachama wasomi watakaokipeleka chama mbele na kukiimarisha.hili lilifanyika kimya kimya bila vurugu za maandamano vyuoni ...kina John Mnyika,Zitto kabwe na wengine ndivyo walivyoweza kuibuliwa kwa utaratibu huu.
CHADEMA ilijitahidi kuwekeza kwa kundi la wasomi zaidi ukilinganisha na NCCR iliyokuwa imejikita kwa vibaka,mama ntilie,wamachinga na wahuni wa mijini.Pia hapa tunaiona CHADEMA ikiibuka na agenda muhimu kama Chama yaani "VITA DHIDI YA UFISADI" Hapa ndipo vichwa vitano bungeni akiwemo Zitto,Mnyika,Slaa,Wangwe waliposumbua serikali bila kususa bungeni au kupayuka mambo wasiyokuwa na ushahidi bungeni.
Hii ilikuwa ni hatua ya pili mbele!!
Uwekezaji mkubwa wa CHADEMA kwenye siasa za mitaani na vijijini ulikuja baada ya uchaguzi wa 2010.kwani somo walilolisoma la kwamba kura hazipo kwenye propaganda za mitandaoni ai magazetini bali zipo kwenye level ya nyumba kumi kumi.
Hapa ndipo unaweza kuuona weledi wa katibu mkuu aliyepumzika siasa Dr Slaa alivyoanza kuwa tishio la dhahiri dhidi ya mfumo wa CCM.Dr Slaa alianza kuijenga CHADEMA kama vile anaeneza kanisa katoliki duniani...alianza kujenga matawi mitaani na vijijini
yaani lilipo tawi la CCM basi pembeni lipo la CHADEMA...kiukweli hii ndio iliyokuwa hatari kubwa kwa CCM kiasi Cha Kinana kuitwa na kuja kuandaa operesheni ya kisiasa iliyotukuka.
Hii Ilikuwa ni hatua ya tatu Mbele...!.###############$#
CHADEMA NA KIZUNGUZUNGU /KIHINDI HINDI
Ama kweli ngoma ya kitoto haikeshi..
CHADEMA ikaanza kurudi hatua zaidi ya tatu nyuma !!
CHADEMA ikaacha kuenenda na katiba yake au sera zake wakati inaaanzishwa.
CHADEMA ikaacha kujadili hoja badala yake ikawa ni mtaalamu wa kutengeneza vihoja bungeni na mitaani ili tu isikike.
CHADEMA ikakosa uvumilivu wa kisiasa na kujipanga .
CHADEMA ikaanza kupeleka siasa vyuoni badala ya kuchukua wasomi kutoka vyuoni ili waje kukijenga Chama.
CHADEMA ikaachana na wasomi na wafanyakazi badala yake ikaanza kuwekeza kwa masela na wanywa viroba wanaoweza kununuliwa na kufagia barabara.
CHADEMA IKAPOTEZA AJENDA YA MSINGI WA CHAMA yaani vita dhidi ya ufisadi kwa kumpokea waliyemtuhumu kuwa ni fisadi na kuanza kumtetea kwa nguvu zote.
CHADEMA ikafuta list of shame kwenye website yao...
CHADEMA ikaanza kumpinga hata Rais anayepambana na ufisadi.
CHADEMA ikaanza kuwatetea wafanyabiashara wasiolipa kodi.
CHADEMA ikaanza kuwaunga mkono wafanyabiashara wa sukari wanaohujumu uchumi
CHADEMA ikaanza kuweweseka kwa kurukia kila hoja.
CHADEMA ikaanza kuingiza bungeni wabunge wa viti maalum kwa kufuata uswahiba .
CHADEMA ikkakosa hoja na badala yake ikaanza kudususa kikekike...yaani siku wakimshutikia Tulia Ackson yuko ndani ya ndege na ndege ipo angani basi wataomba kushuka.
CHADEMA ikawa Chama cha kambale yaani kila mtu ana sharubu...haijulikani katibu mkuu ni Lowassa au Mwalimu au Mbatia au Silinde kila mmoja anatoa maelekezo tu.
Hebu niishie hapa na niwakaribishe muendelee kutaja hatua kumi zaidi walizopiga CHADEMA kuelekea reverse.
TUWASAIDIE WAPINZANI WASIFE KWA AFYA YA TAIFA