Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Binafsi nashangazwa sana na ukimya wa watanzania kuhusu haya makato ambayo kwakweli ni makubwa mno kulinganisha na vipato halisi vya watanzania walio wengi.
Waajiriwa wengi wa nchi hii hasa watumishi wa umma wana mishahara midogo sana huku wakikabiliwa na msururu wa makato ya kisheria katika mishahara yao kuanzia PAYE, BIMA, makato kwa ajili ya mifuko ya hifadhi ya jamii,n.k.
Inasikitisha sana katika mlolongo huu mfanyakazi anaongezewa makato mengine ya kisheria ya asilimia 15 ya basic salary yake huku wengine teyari wakiwa na mikopo ya mabenki.
Kuna taasisi iliahidi kwenda mahakamani kupinga makato haya lakini mpaka sasa hatusiki chochote kinachoendelea huku watu wakiendelea kuumia na makato haya makubwa.
Mimi nawashsuri CHADEMA, ACT,na vyama vingine pamoja na wadau wengine kwenda mahakamani kupinga makato hayo iwapo kisheria inawezakana au kutoa mawakili kwa gharama za vyama kusimamia kesi hizi iwapo vyama vya siasa havina haki hiyo kisheria.
Japo Bodi inaruhusiwa kuongeza makato wakati wowote sidhani kama kisheria ni sahihi mabadiliko hayo kuathiri wale waliongia mkataba na Bodi kabla ya sheria kufanyiwa mabadilko.
Vile vile sidhani kama ni sahihi kubadili sheria bila kuhusisha wadau na kama sheria inairuhusu Bodi kubadili kiwango cha makato bila kushirikisha wanufaikaji na wadau wengine,basi sheria hii itakuwa ni sheria mbaya na inastahili kupingwa mahakani.
Mapungufu mengine ya wazi ya sheria hii
Grace period ya mwaka mmoja
Pia sheria hii inatoa grace period ya mwaka mmoja kwa mnufaika tangu amalize chuo na baada ya kipindi hicho kuisha, mnufaika huyu anatakiwa kuanza kulipa deni lake.
Lakini sheria hii haitambui ukweli kuwa kwa watumishi wa umma inaweza kuwachukua hata miaka miwili tangu wawasilishe vyeti kwa waajiri wao ndio wabadilishiwe mishahara yao(wapandishwe vyeo).
Sasa kumkata hiyo asilimia mtu mwenye mshahara wa Diploma kama ya ualimu sijui unategemea mtumishishi aishije na aweze kuleta tija mahala pake pa kazi..
Mimi nashauri grace period iwe ni angalau miaka miwili ilo hata makato yakianza basi mtumishi huyu awe na ahueni japo kidogo.
Utaratibu wa kuzingatia moja ya tatu ya mshahara.
Ni serikali yenyewe ndio iliweka utaratibu huu ili kumlinda mfanya kazi wake kuhakikisha anabaki na moja ya tatu ya mshahara wake baada ya makayo yote ya kisheria na yasiyo ya kisheriai lakini sina uhakika kama Bodi huu utaratibu unawahusu au laa .
Nachoshauri hapa ni kuwa,kama kweli huu utaratibu wa moja ya tatu Bodi hauwahusu au hawauzingati kama nilivyowa sikia(wenye uhakika watusaidie), basi ni wakati wa Bodi nao kuzingatia utaratibu huu ambao nao sijui kama uko kisheria au ni utaratibu tu usio na nguvu ya kisheria(sina uhakika kuhusu hili).
Wapinzani kama watu mnaotaka kushika madaraka ya nchi, nawashauri haya ndio mambo ya kupigania wananchi sambamba na mambo mengine kwani yanagusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
Na hata muswaada wa kuunganisha mufiko ya hifadhi ya jamii nao kama utapitishwa kama ulivyo ni vizuri nao muupinge mahamani kama utathiri utoaji wa mafao na haki zingine za wanachama ambao walijunga na mifuko hii kabla ya mabadiliko yanayotarajiwa hayajafanywa.
Tatizo kubwa la sisi watanzania ni kuwa na reaction ya muda tu na baada ya hapo tunasahau wakati nchi za wenzetu hata bei tu ya mkate ikipanda ni maandamano nchi nzima.
Nachojiuliza hivi kesho na kesho kutwa wakiamua kuongeza asilimia na kufikia asilimia 20 tutakuwa na haki ya kulalamika au kuhoji kama leo hii hatujachukua hatua yoyote?
Binafsi niliwahi pendekeza vyanzo hivi vya mapato kwa Bodi hii ya Mikopo kupitia huu uzi hapa chini.
Hivi vinaweza kuwa vyanzo mahususi vya mapato kwa ajili ya Bodi ya Mikopo