CHADEMA muacheni Lowassa apumzike, uchokonozi utawaponza

Jamaa wanateseka sana...Sema hawakutegemea kama mzee angerudi ghafla..
 
Siri gani zilizoko Chadema ambazo zitakuwa hatari kwa nchi? Je, ni ugaidi?
 
Siri gani ambazo Lowassa atakuwa nazo ambazo akina Zitto, Arfi, Dr Kaboru, Dr Slaa n.k hawakuwa nazo? Naona hoja zako zimejikita katika kutoa vitisho visivyokuwapo
 
Usipangie watu cha kuchangia, maana ametukanwa sana na wanaccm na hukuwahi kuwaonya zaidi ya kuona sawa kisa Slaa alihukumiwa nafasi. Acha unafikia maana haulipi.
Povuuu ! Hapo Mtazamo amesema ukweli ulio wazi , kuna watu wenye matusi vinywani mwao kuliko wana ufipa?
 
 
Ukweli ni kwamba hadhi kidogo aliyonayo EL ni kwa sababu ya kujiunga na Chadema. CCM ilimchafua kwa kiasi kikubwa sana hadi kuuaminisha umma kwamba wanaanzisha mahakama ya mafisadi ilikuwa ni kwa ajili yake mwenyewe. Kumbuka CCM hao hao walisema chama chao kimesafishika kwa kuondoka EL. Mtakumbuka Polepole alivyomshambulia EL kwamba ndiye alikuwa kikwazo hata cha kupatikana kwa katiba mpya. Polepole alitamka wazi kabisa kwamba amejiunga rasmi kwenye ulingo wa siasa za CCM baada ya chama hicho kuondokewa na mafisadi akina EL.

Dr. Slaa naye alisema amekimbia Chadema kwa sababu ya EL na sasa DR Slaa ni MwanaCCM na balozi wa Sweden. Sasa tunasubiri kuona kama kweli Dr. Slaa alimkimbia Lowassa tuone kama ataachia na huo ubalozi aliopewa na mwenyekiti wa CCM
 
Acha hizo maneno zako.
Wakati Dr. Slaa anaondoka mlisema sio chochote na hana athari yoyote.
Bado tunakumbuka sana.
Lowassa naye katoka bado mnarudia makosa yale yale.
Siku jamaa akimwaga mboga mtatafuta pa kujificha.
 
CCM wanazidi kuudhihirishia umma sura yao halisi. Yaani viongozi wote wa chama na serikali wanafunga ofisi zao wasiwahudumie watanzania kisa tu kwenda kumpokea Lowassa! Hivi Polepole wewe na wenzako, hamuoni aibu kwa jinsi mlivyopiga hata push up kumdhihaki Lowassa?
 
Kumkubali Mzee Lowassa kurudi CCM hiyo ndio picha kamili ya Demokrasia iliyotukuka ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Chadema imeathirika vibaya sana kuondoka kwa EL...muda utaongea katika hili.
 
Siku ile Mzee Lowassa alipotua Ufipa ilikuwaje!?
 
Siku ile Mzee Lowassa alipotua Ufipa ilikuwaje!?
Jibu swali. Mtaendelea kujenga mahakama ya mafisadi? Mlisema CCM imekuwa safi kwa Lowassa kuondoka. Leo mnatwambia nini? Mlisema Chadema imempokea fisadi. Leo mnatwambia nini?
 
Na kwasababu hakukuwa na risiti ya mauziano pia ni rahisi tu kukana, EL amejishushia heshima sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jibu swali. Mtaendelea kujenga mahakama ya mafisadi? Mlisema CCM imekuwa safi kwa Lowassa kuondoka. Leo mnatwambia nini? Mlisema Chadema imempokea fisadi. Leo mnatwambia nini?
Unapotumia neno "Mlisema" unamaanisha nini!? Ni wapi niliposema hayo uliyoainisha hapo juu!? Hao waliosema ni kina nani?
 
Kumkubali Mzee Lowassa kurudi CCM hiyo ndio picha kamili ya Demokrasia iliyotukuka ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Chadema imeathirika vibaya sana kuondoka kwa EL...muda utaongea katika hili.
Mbona haikua Demokrasia alipohamia CDM!!
Mkuu hakuna athari yoyote, Muda utasema 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…