Chadema msimsahau mzee Kingunge.

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Mzee Kingunge atelekezwa na _CHADEMA_ .

Nakumbuka maneno ya aliyekuwa mwenyekiti wa BAVICHA, Mh Katambi alisema ndani ya CHADEMA watu wengi ni sawa na makarai yaani wanatumika wakati wa ujenzi wa nyumba lakini nyumba ikikamilika karai halina thamani tena.

Wengi walimpinga kumdhihaki na kumtukana na wengine walidiriki kusema amenunuliwa lakini Katambi aliongea maneno mazito sana. Leo tumeshuhudia maneno aliyoyaongea katambi kwa Mwanasiasa mkongwe sana Mh kingunge.

Wote tunajua ni jinsi gani kingunge alivyopigana kuijenga cdm wakati wa uchaguzi.
Leo kingunge sio wa kuachwa kujuliwa hali na hata mwenyekiti wa shina wa cdm.Leo cdm hawajali thamani ya Kingunge. Si Lowasa, Mbowe, Mnyika, Mashinji waliomtembelea mzee Kingunge!!!

Yanayotokea kwa Kingunge ni somo kubwa sana kwa vijana wanaojiita wafia CHADEMA. CHADEMA ni chama cha watu wachache leo nimegundua kwanini mrembo Wema Sepetu alisema anakosa furaha ndani ya CHADEMA.

Vijana kataeni kuwa makarai
 
Back
Top Bottom