Mamlaka makubwa ya MTU mmoja kwenye nchi ni tatizo kubwa sana la Kikatiba katika nchi hizi maskini sana .
Nchi ambazo kila kitu kinategemea maamuzi na huruma ya mtu mmoja tuu na hakuna wa kuweza kumpinga iwe kisheria.
Hali hii inasababisha kila mtu kutafuta Uhuru na maisha yake binafsi kwa kuwa karibu na ua la waridi, yaani kuwa karibu na mwenye riziki mkononi.
Viongozi wa Dini ,wazee , wafanyabiashara waliozoea kubebwa na Chama na vijana wasaka madaraka; wote hawa wanakua na kazi moja tu ya kupigania maslahi yao bila kujali lipi ni haki na lipi sio haki.! Lipi limefanywa kutokana na siasa za Chuki na lipi limefanywa kwa sababu ya visasi .
Dunia itakua mahali salama kama tutasimama kweli kwenye misingi imara ya manabii wetu wa zamani sio hawa manabiii wa kutangaza nia kupitia vyama vyenye nguvu ya kidola.
Manabii wa zamani wametufundisha jambo moja kubwa sana; USIMTENDEE MWENZAKO JAMBO AMBALO WEWE MWENYEWE HUPENDI KULITENDEWA.
CCM na viongozi wa Dini mnaoshangilia kila jambo hata lile ambalo msingependa kamwe nyie mlitendewe tubuni murejee kwenye maandiko ya Dini na hata maadili ya wazee wetu wa zamani.
Tumesahau kuwa Misikiti mingi ,makanisa mengi makubwa na madogo na hata mabango mengi ya Waganga wa asili yalipata kuwa na mafanikio makubwa wakati na kufikia yalipofikia kutokana na utawala wa awamu ya JK. Huruma yake na utu wake ndivyo vilivyosababisha watu wakaanza kumtukana na kuona hajafanya kitu chochote. Vijana wetu walipata ajira na nafasi nyingi za kusoma ndani na nje ya nchi huku biashata zikishamiri ndani na nje ya nchi .
Watu wengi vijijini walijenga majumba ya vigae na mabati ya msauzi kila kona ya nchi. Viongozi wa Dini kama akina Gwajima ndipo walipojipatia utajiri mkubwa na kujitangaza ndani na nje ya nchi wakati wa JK. Makanisa yakajenga vyuo vikuu vingi na majengo makubwa makubwa kila kona ya nchi ,Misikiti ya kisasa ikajengwa nchi nzima na visima vya maji .Cha ajabu Leo wale wale waliokaa mezani kwa Mh. JK rais wa awamu ya NNE ndio hao hao wanaokaa na kusahau mema yaliyotokana na Uhuru wa kuabudu,Uhuru wa kujieleza,Uhuru vyombo vya habari,Uhuru wa kisiasa,utu,uzalendo wa kweli ,umoja, upendo n.k.
Naogopa sana ninapoona taifa lenye watu wasiothamini wema wa mtu kwa sababu tu ya kusaka madaraka na vyeo.
Ni vema tukakumbuka kuwa awamu ya tano isingekua na uwezo wa kukusanya kodi kama awamu ya NNE isingekua imewajenga wafanyabiashara kuwa na uwezo wa kiuchumi. Awamu ya NNE ilinunua mpaka EFD machine kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya kukusanya kodi.
Hali kadhalika Chadema na Mgombea wao wasibeze maendeleo yanayofanywa na awamu ya tano. Hata wakiingia madarakani watapata sehemu nzuri zaidi ya kuanzia kutokana na awamu hii ya tano.
Waombe kura lakini wasikejeli juhudi za awamu ya tano. Wapinzani wayakubali yale mazuri ndipo waonyesha mabaya na kusema wao watafanya mazuri zaidi kwa namna gani.!
Reli na ndege ni muhimu hilo halina ubishi . Kinachopaswa kupiganiawa ni namna ya kuzijenga bila kuathiri sekta nyingine.
Kuwabana mafisadi ni muhimu sana lakini cha muhimu ni kuwabana bila kumbambika mtu kesi au kumdhulumu Mali zake kwa sababu tu hakuungi mkoni kisiasa.
Kuwadhibiti Mabeberu wa ndani na nje ni lazima na muhimu lakini cha msingi ni kutuambia mtawadhibiti vipi bila kuvunja sheria.
Kudhibiti siasa uchwara za kupakana matope ni muhimu lakini cha msingi mtuambie nyie mtadhibiti vipi bila kuvunja katiba ya nchi.