Ni ukweli usiopingika kuwa wapo vijana wanaojitoa katika ujenzi wa CHADEMA kwa gharama zao na muda wao pasipo kutegemea kulipwa.
Moja kati ya vijana hawa ni Nicholaus Ngowi wengi tukimfaham kama mtoto wa seremala.Huyu ni yule ambaye Lukuvi alimwita Lema alipomuuliza maswali live star tv akitokea Dodoma.
Mpambanaji huyu alijitolea mwenyewe kwa gharama zake kutoka Dodoma kwenda Muleba kusaidia campain za uchaguzi wa vijiji na vitongoji lakini kabla ya kwenda Muleba alifanya mkutano mkubwa sana wa hadhara kata ya kitangiri kwa kushirikiana na Alphonce Mawazo.
Siku moja kabla ya safari yao kwenda Muleba alipata ajali mbaya sana na kiukweli aliumia sana mguu wake wa kushoto na kulazwa hospitali ya Bugando na baadae Mwananchi hapa Mwanza.
Kiukweli nimemtembelea hospilini Mwananchi hali yake ni mbaya sana na anahitaji msaada wa haraka ili kuokoa mguu wake na maisha yake kwa ujumla.
Nilitaka nimpige picha ila alikataa. CHADEMA msaidieni kamanda huyu.namba yake ni 0713014400