CHADEMA mpo tayari kumpokea LOWASSA??

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,101
6,027
Lowassa ajiandaa kuaga...!! nanukuu

''Taarifa zaidi zimeeleza kuwa endapo Lowassa atatangaza kuachana mojakwamoja na CCM na kujiunga kambi ya upinzani, hatataja moja kwa moja chama anachotarajiwa kujiunga nacho ikiwa moja ya mbinu za kujiwinda na wapinzani wake katika azma yake ya kuwania urais mwaka 2015'' mwisho wa kunukuu.

Hii nikadri ya uchambuzi mrefu wa Gazeti la Dira la jana!! Hatua ya Lowassa kung'atuka ina lengo la kumdhoofisha Rais
Kikwete ili aonekane hajafanya lolote katika falsafa yake ya kujivua gamba mbinu ambayo pia imetumiwa na RA.

Je CDM mpo tayari kumpokea huyu EL endapo atajivua gamba CCM??
 
lowassa ajiandaa kuaga...!! Nanukuu

''taarifa zaidi zimeeleza kuwa endapo lowassa atatangaza kuachana mojakwamoja na ccm na kujiunga kambi ya upinzani, hatataja moja kwa moja chama anachotarajiwa kujiunga nacho ikiwa moja ya mbinu za kujiwinda na wapinzani wake katika azma yake ya kuwania urais mwaka 2015'' mwisho wa kunukuu.

Hii nikadri ya uchambuzi mrefu wa gazeti la dira la jana!!

Je cdm mpo tayari kumpokea huyu el endapo atajivua gamba ccm??

mimi naunga mkono chadema 100%
lowassa akipokelewa chadema itakuwa ndio mwanzo wa mimi kurudi ccm
 
Mi nadhani anaweza kuwa mwanachama wa kawaida na sidhani kama CDM inachagua wanachama ila inachagua viongozi kuwaweka kwenye nafasi mabalimbali na kama yeye anataka kuongoza atakuwa chini ya uangalizi maalum na sio aje na ndoto zake kuu za kutaka madaraka ya urais
 
Lowassa hawezi kuondoka CCm ladba JK aanze kwanza yy kutoka.
Pia lowasa ni tishio sana zaidi unavyofikiri ndani ya nchi mtandao wake ni mkubwa sana.
Hivyo CCm wanamgwaya sana, na pale bungeni anasupport kuliko Serikali pia kweny chama ana support
kubwa kuliko Rais. thas why jamaaalivunja sekretariet la yangemkuta ya thabo mbeki.
 
Lowassa kama anatuhumiwa na kukawa na ushahidi hastahili kujadiliwa kwa mtazamo wa kuhamia chama chochote cha siasa bali kuhama gereza moja kwenda jingine.....

Vinginevyo, kwa chama chochote cha siasa ambacho Lowasa atahamia basi chama hicho kinahitaji kumkumbusha juu ya maadili na values zake ambazo Lowassa atatakiwa kuzifuata.Kama itaonekana lowassa kaonewa au katolewa kafara basi ni jukumu la chama chochote cha siasa baada ya kujiridhisha kumpokea na kumtumia kama mtaji wake wa kisiasa ili kujiandalia mazingira mazuri ya kuwajibisha watuhumiwa,wezi na wale wote walioligharimu taifa kwa muda wote ambao CCM imekuwa madarakani na kuwalinda watuhumiwa/wahalifu hao

Chama makini cha siasa kinahitaji kufanya kazi ya kuwafanya hata wale Raia ambao si waadilifu kwa kuwaponya na kuwaonyesha njia ya kuwa raia wema,wawajibikaji na hilo litawafanya wawe na manufaa kwa Taifa letu.Natoa wito kwamba,tusiwatenge waliohisiwa au wafungwa waliomaliza vifungo vyao,bali tuweke mikakati ya kuwafanya kuwa raia wema na kuwatumia kwa maslahi ya taifa letu kama tunapata fursa hiyo
 
Lowassa kaa hukohuko CCM umshughulikie ****** katufikisha pabaya sana.Na sasa yuko mtegoni ya Jairo ni trailor picha inakuja.Jakaya hajui kuwa wewe ndiyo uko nyuma ya shughuli ya kukwamisha bajeti ya ngeleja.CCM watajuta kukufahamu
 
Lowassa ajiandaa kuaga...!! nanukuu

''Taarifa zaidi zimeeleza kuwa endapo Lowassa atatangaza kuachana mojakwamoja na CCM na kujiunga kambi ya upinzani, hatataja moja kwa moja chama anachotarajiwa kujiunga nacho ikiwa moja ya mbinu za kujiwinda na wapinzani wake katika azma yake ya kuwania urais mwaka 2015'' mwisho wa kunukuu.

Hii nikadri ya uchambuzi mrefu wa Gazeti la Dira la jana!! Hatua ya Lowassa kung'atuka ina lengo la kumdhoofisha Rais
Kikwete ili aonekane hajafanya lolote katika falsafa yake ya kujivua gamba mbinu ambayo pia imetumiwa na RA.

Je CDM mpo tayari kumpokea huyu EL endapo atajivua gamba CCM??

Hatuko tayari
 
CCM ni Lowassa,na Lowassa ni CCM hivyo usikae ukafikiria kuwa Lowassa anaweza kutoka CCM hata siku moja Ng'o kwa akitaka kufilsika niyeye kung'oka CCM ila akijiudhuru nyazifa awezi kuacha Ubunge wa CCM Monduli kwani atasingizia mimi siwezikuacha wananchi wangu wa Monduli watawaliwe na mwingine!Hivyo yeye sirahisi kuachia ubunge na uanchama CCM.
 
ina maana nguvu ya Lowassa ndani ya CCM imedhoofu kiasi cha yeye kufikiri kukihama chama? kirahisi namna hii? Mimi nafikiri anapambana mumo kwa mumo mpaka mwisho ujulikane. Bado sijawapa kina CCJ ushindi, mziki bado mzito na pevu tusubiri wakati zoezi la kukoboana magamba likiendelea.

Namkumbusha rafiki yangu NAPE Kwamba tayari gamba lingine limeibukia jana wizara na nishati ya madini naomba aliweke kwenye list ya kukobolewa.
 
Katibu mwenezi mwenyewe CCJ,sasa atamkoboa nani?

Sasa hivi CCM = CCJ vs chadema vs ccm dhaifu !
 
Ushauri wa bure kwa Lowasa, akitoka sisiem asilete fujo kwenye chama chochote cha siasa.
Walau asije CDM. Mchango aliotoa kwa taifa kama upo unatosha, kama haupo, hataweza kutoa tena.
Akasimamie miradi yake kwa njia ya halali zaidi, sio za kifisadifisadi.
Yeye atakumbukwa sio lazima kwa kung'ang'ania kuwa kiongozi ndani ya chama au/na serikali.
 
CCM ni Lowassa,na Lowassa ni CCM hivyo usikae ukafikiria kuwa Lowassa anaweza kutoka CCM hata siku moja Ng'o kwa akitaka kufilsika niyeye kung'oka CCM ila akijiudhuru nyazifa awezi kuacha Ubunge wa CCM Monduli kwani atasingizia mimi siwezikuacha wananchi wangu wa Monduli watawaliwe na mwingine!Hivyo yeye sirahisi kuachia ubunge na uanchama CCM.

unasikia KK, kwa dari ya uchambuzi huo ni kwamba atatacha nyadhifazake zote ikiwepo ubunge, halafu ataingia chama kingine cha siasa na atagombea tena ubunge Monduli....so its possible pia
 
Katibu mwenezi mwenyewe CCJ,sasa atamkoboa nani?

Sasa hivi CCM = CCJ vs chadema vs ccm dhaifu !

Unasikia Ben, hapa hatumuhuku!! Lets say kaingia CDM na keshajadiliwa na vikao vya chama kaoneka ni msafi na atakuwa under control, vp akiingiza ile falsafa ya kugombea urais 2015 huoni kutakuwa na mpasuko na mgawanyiko ndani ya Chama??
Hii ilitokea kwa Nape Jimbo la Ubungo lakini CDM walihandle it proper lakini huyu EL ana nguvu mno!!
 
ina maana nguvu ya Lowassa ndani ya CCM imedhoofu kiasi cha yeye kufikiri kukihama chama? kirahisi namna hii? Mimi nafikiri anapambana mumo kwa mumo mpaka mwisho ujulikane. Bado sijawapa kina CCJ ushindi, mziki bado mzito na pevu tusubiri wakati zoezi la kukoboana magamba likiendelea.

Namkumbusha rafiki yangu NAPE Kwamba tayari gamba lingine limeibukia jana wizara na nishati ya madini naomba aliweke kwenye list ya kukobolewa.

Ujue ukisoma hii stori ya EL kuaga, imeenda mbali zaidi kwa kuwaandaa watu sehemu zote atakazopita,alie na wengine wazimie, wasukuma gari, n.k!! Yaani ni kama mchezo wa kuigiza vile, atapita mikoa ya Dodoma, Morogoro,Pwani,Arusha, tanga, Kilimanjaro na atamalizia jimboni kwake Monduli ambako ndiko rasmi atajivua gamba kwa hotuba ndefu ya kumchafulia JK.
 
Unasikia Ben, hapa hatumuhuku!! Lets say kaingia CDM na keshajadiliwa na vikao vya chama kaoneka ni msafi na atakuwa under control, vp akiingiza ile falsafa ya kugombea urais 2015 huoni kutakuwa na mpasuko na mgawanyiko ndani ya Chama??
Hii ilitokea kwa Nape Jimbo la Ubungo lakini CDM walihandle it proper lakini huyu EL ana nguvu mno!!

Nape asingeweza kuwa mtaji wa CHADEMA ndani ya jimbo la Ubungo na wala hatawahi kuwa threat within or outside Chadema katika sanduku la kura.Najua,nina uhakika,niamini !

Kuhusu nguvu ya EL: Lowassa ana nguvu ndani ya chama chake tu,si nje ya chama.Samaki anajua kuogelea akiwa majini tu nje ya hapo utamuonea huruma,atasaidiwa!

Nilimshauri Nape na Chama chake,wakitaka kuweka mpinzani atakayetoa changamoto kwa chadema basi awe mtu ambaye amefanikiwa kuwahadaa watanzania angalao hadi sasa hivi kama Magufuli,Sitta,Membe tofauti na hapo wakizembea basi nguvu ya Lowassa ndani ya chama chao watampitisha mgombea ambaye ni popular ndanii ya chama lakini nje ya chama hatakiwi,hapendwi na hana jipya.Kwa hiyo ili kuepuka kipigo cha aibu 2015 hawana budi kuhakisha angalao wanashindwa kwa staha kwa kumzuia Lowassa kwa njia halali au yoyote ile kisiasa but technically and tactically ! ! 1 ushauri wa bure kwa watani!

Lowassa ajiandaa kuaga...!! nanukuu

''Taarifa zaidi zimeeleza kuwa endapo Lowassa atatangaza kuachana mojakwamoja na CCM na kujiunga kambi ya upinzani, hatataja moja kwa moja chama anachotarajiwa kujiunga nacho ikiwa moja ya mbinu za kujiwinda na wapinzani wake katika azma yake ya kuwania urais mwaka 2015'' mwisho wa kunukuu.

Hii nikadri ya uchambuzi mrefu wa Gazeti la Dira la jana!! Hatua ya Lowassa kung'atuka ina lengo la kumdhoofisha Rais
Kikwete ili aonekane hajafanya lolote katika falsafa yake ya kujivua gamba mbinu ambayo pia imetumiwa na RA.

Je CDM mpo tayari kumpokea huyu EL endapo atajivua gamba CCM??

Nadhani CHADEMA wameshajifunza kutokana na ngarambe zinazofanywa na Shibuda hivyo sidhani kama watafanya kosa kama hilo tena la kuruhusu magarasa kutoka magamba ndani ya chama chao.
 
Back
Top Bottom