Uchaguzi 2020 CHADEMA mnarudia Makosa ya 2015

Msulibasi

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
5,836
7,492
Nakumbuka Maxine Mello akitoa tathmini juu ya mchango wa media katika uchaguzi 2015 aliweka wazi kuwa CCM Ilitawala media na kusambaratisha wapinzani. Kuelekea October 2020 sijaona juhudi za dhati za chadema Kukamata kiungo yaani media.

Japo ilionekana kuzidiwa na CCM Chadema walikuwa na nguvu kwenye mitandao mara dufu au zaidi ya sasa.. Ukitazama Facebook ambayo wapiga kura wengi hutumia huoni Amsha Amsha ya Chadema.

CCM Kupitia matawi yao kuanzia kata wilaya MIKOA na jumuiya zao wanafanya juhudi kumjenga mwenyekiti na mgombea wao pamoja na wagombea ubunge kwa kupitia makundi ya mtandaoni. Inawezekana CCM ikawa na utatibu na ugharamiaji wa vijana wao wanaopambana kwenye media.

Chadema bado wana mawazo ya kutumia press conference kitu ambacho hakiwasaidii sana. Press conference zinaingiliwa na Vyombo vya dola na hazidumu kwenye mijadala. Chadema ikishindwa dimba la kati itakuja Lia .
 
Nakumbuka Maxence Melo akitoa tathmini juu ya mchango wa media katika uchaguzi 2015 aliweka wazi kuwa CCM Ilitawala media na kusambaratisha wapinzani. Kuelekea Oktoba 2020 sijaona juhudi za dhati za CHADEMA Kukamata kiungo yaani media.

Japo ilionekana kuzidiwa na CCM, CHADEMA walikuwa na nguvu kwenye mitandao mara dufu au zaidi ya sasa.. Ukitazama Facebook ambayo wapiga kura wengi hutumia huoni Amsha Amsha ya CHADEMA .

CCM kupitia matawi yao kuanzia kata wilaya mikoa na jumuiya zao wanafanya juhudi kumjenga mwenyekiti na mgombea wao pamoja na wagombea ubunge kwa kupitia makundi ya mtandaoni. Inawezekana CCM ikawa na utatibu na ugharamiaji wa vijana wao wanaopambana kwenye media.

CHADEMA bado wana mawazo ya kutumia press conference, kitu ambacho hakiwasaidii sana. Press conference zinaingiliwa na Vyombo vya dola na hazidumu kwenye mijadala. CHADEMA ikishindwa dimba la kati itakuja lia na kusababisha meno.
 
Media zipi unasema wakati ccm nichama cha watu wakijijini wasiojuwa kusoma na kuandika. ..hapa Tz hakuna chama chenye watu wajinga kama ccm ...Hata Nyalali hilo miaka ya 1990+
 
Mkuu sio kwamba Chadema imelala

Ila Chadema imekufa, vijana Wengi wameridhishwa na uchapakazi wa Magufuli ndio maana huoni bla bla mtandaoni

Vijana hawa wasio na kazi wasio na mbele wala nyuma???? Hili ni bomu ambalo akitokea mtu akawagawia AK 47 moto wake hautazimika leo wala kesho.
 
Kwa hiyo Chadema haijafa mkuu?
Chadema haijafa bali itakufa kama isipojitibu. Inatakiwa kuimarisha propaganda kwenye media badala ya kutegemea tweet za Lema Hilda Newton hao kina Mdude na Halima. Lazima kuwe na mifumo ya content na direction.

Kwamba wiki hii tunapost kulenga jambo gani, tunaandikaje,nk .Chadema isije tegemea Kigogo atawajeuka. Pia makosa ya Kigogo yasijekuigharimu Chadema kama chama.
 
CHADEMA shida yao huwa wanakubali kucheza miziki ya CCM.

CCM wako vizuri sana kuunda ajenda na kuzitumia kwa manufaa yao, ni propagandists wazuri hawa jamaa.

CHADEMA ni wadandiaji wa ngoma ya watu.

Bado hawajachelewa muda ndo huu, wadau tupo hapa with full bundle.
 
Chadema hakina mvuto kimebaki na wajinga wachache hasa humu jf,hakina sera kimekuwa genge la wahuni,kimebaki kufanya fujo na kuvunja sheria tu hakuna mwanainchi mwenye akili zake timamu atakae wapa kura

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Media zipi unasema wakati ccm nichama cha watu wakijijini wasiojuwa kusoma na kuandika. ..hapa Tz hakuna chama chenye watu wajinga kama ccm ...Hata Nyalali hilo miaka ya 1990+
CCM wananufaika sana na uwepo wa hao munaowaita wajinga ambao mtandao wao ni facebook. Kura ya Professor ni sawa na kura ya mjinga au mpumbavu mmoja huko Tandale Manyoni Newala au Ngarenaro. Chadema wagharamie.

Badala ya kuzozana na spika au polisi muda huu ni mzuri kuandaa Ilani ,kushawishi wagombea na kutengeneza mtandao wa media.

CCM wao wana watu wengi wenye influence ambao si wagombea mfano wastaafu. Mbowe anabanwa Hai huyohuyo amnadi mgombea uraisi?
 
Chadema wanae kigogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna wakati hata kigogo anapigana vita ya kiharakati na sio CHADEMA.

Maana CHADEMA huwa hawawezi kushikiria jambo moja na kusimama nalo kama ajenda.

Wao wanafuata sera ya upinzani hivyo wamekaa nje ya kinywa cha watawala wakisubiri kupinga.

Hapo ndo kufeli kwao kunapokuja.
 
Chadema haijafa bali itakufa kama isipojitibu. Inatakiwa kuimarisha propaganda kwenye media badala ya kutegemea tweet za Lema Hilda Newton hao kina Mdude na Halima. Lazima kuwe na mifumo ya content na direction.Kwamba wiki hii tunapost kulenga jambo gani, tunaandikaje,nk .Chadema isije tegemea Kigogo atawajeuka. Pia makosa ya Kigogo yasijekuigharimu Chadema kama chama.
Kwani kigogo ni mwanachama au kiongozi wa chadema? Sasa anahisikaje na CDM?
Mmeishiwa hoja au mmefilisika hoja?
 
Back
Top Bottom