CHADEMA mnampuuza Mbowe!

any way...... ngoja ninywe kinana bariiidi tatu then nikalale umeshaniharibia siku......
 
Nape ( mnyiramba aliyeharibiwa ) nafikiri ushauri wa mahengela umeupata vema. Harakati hazimaanishi ugaidi, siasa za ugomvi, na mambo mengine mabaya. Please wewe ni kijana sana kuliko mimi, yamkini waweza kusoma sana hata yale magumu ukayajua vema.
Ona mawazo yako yanavyokudhalilisha: Hebu tuyape majina mawazo yako.
Uana harakati = a
ugaidi = b
mwanzilishi wa uanaharakati = c

haya tuje kwenye logic sequencia
: Uanaharakati ulianza zamani tangu enzi za kutafuta uhuru wa tanganyika (a)
:ugaidi ni sawa na uanaharakati
:mwalimu nyerere alikuwa mmojawapo wa waanzilishi wa uanaharakati wa kudai uhuru hapa tanganyika
hitimisho: (therefore) nyerere alikuwa mwanzilishi wa ugaidi.
Anayependa kuongezea ama kurekebisha aje afanye.
 
(Mhe. Mbowe akiwa Mbeya alikiri wazi kuwa CHADEMA kwa miaka yote tangu kuanzishwa kwake kimekuwa ni chama cha HARAKATI... Lakini nilifurahi kusikia akiwaomba wenzake kuwa sasa ni wakati wa kukibadili Chama chao kutoka chama cha harakati na kuwa sasa chama cha SIASA.)

NDUGU NAPE, KWANI SIASA SIO HARAKATI? JE! HAMSEMI NINYI KUWA CHAMA CHENU NDICHO KILICHOONGOZA HARAKAKI ZA KISIASA ZA KUPATA UHURU? JE! HIYO MIKUTANO YENU SIO HARAKATI ZA KISIASA ZA KUBAKIA MADARAKANI? USIVIABISHE VYUO ULIVYOSOMEA MKUU KWA SABABU TU YA KUFIKIA MALENGO YAKO YA KISIASA.
 
Sasa ni karibu miezi mitano tangu atangaze na kuwasilisha ombi hili kwa wenzake lakini kwa masikitiko makubwa wenzake mmempuuza mwenyekiti wenu, badala ya kukibadilisha chama sasa mnakifanya cha harakati zaidi mpaka sasa mnapanga na kutekeleza kudhuru watu hasa wasiowaunga mkono.

Nilitarajia Kama Katibu wa Itikadi wa Chama ungenda mbali na kuthibitisha huo mpango unaozungumzia na Je unatofautiana na Ule wenu wa sinema ya Ugaidi?
Pia kwa sababu muda mrefu ulikuwa upo offline ungesaidia pia kutoa ufafanuzi wa mambo mbali mbali:

  1. Kinana na Meno ya Tembo
  2. Mpango wenu na China
  3. Je hili unalijua?
 
Nape na ccm wamechanganikiwa na speed ya CHAMEDA hivyo hayo ayasemayo Nape ni maneno ya mfa maji haachi kutapatapa, kumbukeni ccm wali wahi kusema vyama vya upinzani ni vya kwenye briefcase sasa leo wanaona speed ya ajabu ya CDM chini ya viongozi makini na sera makini wameanza kuita chama cha harakati, VIVA CDM
 
Hao jamaa kuacha harakati ni sawa na kusikia Wenger anataka kumnunua Christian Ronaldo.....

Labda kama watawafukuza kina (kama walivyowafukuza wale madiwani) Msigwa, Lisu, Lema, Sugu, Mdee, Wenje.....
 
nape akili zake zote na vijanao wao wote wa kulumba wanadhani adu mkubwa wa ccm ni chadema.....
umasikini ulio kidhiri unafanya ccm ionekane vituko....adui wa ccm ni umasikini.....
ccm ijaribu kuwa wajibisha mafisadi na kuleta maisha bora waone kama kuna mtu atajiangaisha na chadema...
chadema ni tumaini pekee kwa watanzania
 
Uzuri ninachompendea DJ Mbowe ni mkweli na muwazi kwani kwenye fact anaweka facta hasa kuwashauri viongozi wenzake na wafuasi wao.
Tena hayo aliyasema kwenye Ukumbi mdogo wa Mikutano wa Mkapa hapa Mbeya.
Lakini yule Babu Slaa amekosa matumaini ya kuishi basi anajifanya kujiwehusha tu na kuendeleza harakati wakati anajua fika harakati sio Siasa!
 

Hivi Ben umepona vizuri kweli wewe au ndo bado unaweweseka.
Hivi kwa akili yako unaona Mfumo wa Mjimbo ndio Kitanzi kwa Chama Dume CCM??
Nenda kajipange na wenzako na uwaambie CCM aitishwi na Majimbo na Chama kisicho na Sera zaidi ya Maneno machafu na Matusi pamoja na mbinu chafu.
 
Wewe Nauye nasikitika kama mpaka leo na wewe huwezi toka kwenye lindi hilo la mawazo finyu aka Ubongo wa mende kichwa cha tembo, kwa sasa njia pekee ya ninyi na wezi wenzio kuendelea kutawala ni kuachana na CHADEMA na kuweka mikakati yenu endelevu ya namna ya kurudisha imani ya wananchi ilopotea juu yenu ila mnabaki kila jukwaa mnalopanda mnaimba chadema tuuu sasa nini mawazo yenu mapya juu ya ukata huu wa maisha unaowasonga wananchi?

Hii inaonesha ni jinsi gani msivyo na maana sidhani kama manmtizamo sawa juu ya nini maana ya UPINZANI na hisi wewe na wenzio bado mnauchukulia upinzani kama ngumi mkononi no sivyo upinzani ni chanzo cha fikra mpya na ufanisi wa serikali katika kusimamia sera za chama chenu na pia kuongeza mpya mtazoona zafaa kutoka kwa wenzenu ili msimu ujao wanapokuja kwa wananchi wanakuta sera zao zote tayari wamesha zisikia kwenu .

Ila ninyi mnawaza ubaya tuu hadi mnafikia kupanga njama na kuwasingizia wapinzani ili wasiwepo je wakiondoka itakuwaje au mnataka kuturudisha enzi za kivuli shame on you tena jueni tumewachoka kabisa asee ata iweje 2015 lazima mng'oke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…