Bedullah
JF-Expert Member
- Dec 9, 2012
- 206
- 79
Hata CCM hawana demokrasia ndani ya chama chao! Wanabadili Mwenyekiti pale tu urais unapobadilishwa kwa mwingine, ndiyo baada ya miaka kumi. Katiba ingebadilika na urais kuwa wa vipindi viwili vya miaka saba saba uenyekiti ungedumu miaka hiyohiyo!Naweza kukubaliana kabisa na wewe. Ila kwa upande fulani jaribu kuangalia hao wachache wanaobadilishana madaraka kuliko yule mmoja tu aliyekuwa pale miaka nenda miaka rudi. Hii ni aibu kubwa kwa chama ambacho kinajinasibu kwa kupigania democracy nchini. CCM kama chama wako na madudu yao mengi ambayo almost kila siku tunayaimba hapa, lakini je hawa wapinzani ambao wao huwa wako msitari wa mbele kabisa kukosoa serikali ya ccm wao wenyewe wanaipractice democracy? Issue ndio iko hapo.
Tumeshuhudia wanachama wakipigwa mkwara walipojitokeza kugombea katikati ya mhula wa urais! Mbaya zaidi demokrasia ndani ya CCM imeyeyuka kabisa sasa zaidi ya kipindi chochote! Mwenyekiti wa sasa aliweka hadharani nia ya " kuwapoteza" waasi ndani ya chama!
Halafu kuna mtu anabana pua na kuushutumu upinzani kwa kukosa demokrasia ndani ya vyama!