CHADEMA mna jipya gani kwa hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA mna jipya gani kwa hili?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zema21, Aug 24, 2012.

 1. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Kwa sasa hivi nchi inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana wetu wanaohitimu mafunzo yao mbalimbali, hakuna juhudi za dhati zinazochukuliwa kukabiliana na tatizo hilo; kama kawaida yetu ya kulalamika kila mmoja analalamika; lakini hakuna hatua za dhata kunusuru tatizo hilo!!

  Ufisadi unaongezeka kila kukicha ukiacha matukio yaliyoripotiwa miaka iliyopita hv sasa kuna utoroshaji wa fedha kwenda nchi za nje!
  Kama kawaida yetu linafanyiwa kazi na vyombo husika, watanzania tumebaki kulalamika huku tukiwa na hali ngumu za maisha, kiasi cha baadhi kukosa hata mlo mmoja wa siku!

  Vijana na hawajui future yao, wengi wao ukiwauliza mipango yao katika miaka miwili ijayo hawajui wakujibu nini!
  Wanaambiwa wakajiajiri huku wakiwa hawana mitaji, vifaa, wala hata elimu ya ujasiria mali bila kusahau ukosefu wa masoko! Watajiajiri vp! Jaribu kufuatilia watoto wa hao wanaowambia vijana wetu wakajiajiri uone kama wamejiajiri wao! Rasilimali za wananchi zinaliwa na wachache!

  Ebu nyie mnaojiita nguvu ya umma tuambieni mtatatua vp haya mattizo yetu?
  Manake siasa zimetuchosha! Hamna lolote tunalosaidika badala ya kuwa walalamishi tuuu! Pia tuzingatie kuwa na nyie mna matumbo kama hawa wengine waliopo sasa pia mna njaa kama wao! Nini kitawafanya msile kama hawa jamaa ile hali mna sifa zinazofanana za njaa na matumbo pia?

  Naomba kuwasilisha
   
 2. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Acha uvivu soma ilani ya cdm ya uchaguzi 2010/2015 ina majibu ya maswali yako, pia bajeti mbadala na taarifa ya mwelekeo wa uchumi kuna uainishaji wa jinsi ya kupunguza uhaba wa ajira, kuziba mianya ya ufisadi na kukuza uchumi ili kutoa matumaini mapya kwa vijana na wananchi kwa jumla.
   
 3. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,832
  Trophy Points: 280
  hivi huoni jansi walivyo saidia vijana katika kupata ajira? nenda hata kwa wale wanaokaa vijiwen kazi hawana lakini kutwa kucha kuipigia debe chadema mbona tayari hii ni ajira?
   
 4. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  hata katiba ya hawa jamaa wengine(ccm) ni nzuri mno lakini hakuna lolote lililofanyika kutokana na ubora wa katiba yao
   
 5. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  kuwa serious kidogo mkuu
   
 6. Root

  Root JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,241
  Likes Received: 12,954
  Trophy Points: 280
  kufufua viwanda vilivyo kufa,migodi ndo njia ya kuongeza ajira so si chadema tu ndo itoe ajira hata wewe pia waweza anzisha ili uisaidie nchi yako na vijana wenzako kupata ajira
   
 7. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Mkuu
  Serikali/dola wao ndo watunga sera pamoja na sheria, kuzisimamia na kuhakikisha zinatekelezwa!
  Ni kweli mtu mmoja mmoja anahusika lakini serikali ndo inatakiwa iwe inatoa miongozo na kuwachukulia hatua wale wote wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao kisheria!
  isingekuwa ni hivyo tusingekuwa na serikali!
  kila mtu angefanya atakavyo
   
 8. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Binafsi nadhani msukumo unatakiwa utoke ndani ya mtu mwenyewe kama mtu hana nia hata ufanye vipi hawezi kuwa na nia na cjui kwann hili serikali halitaki kuliweka wazi kuwa sekta binafsi ndio injini ya gurudumu la maendeleo ya taifa letu kama ndio hivyo fursa zinapaswa kuwa wazi ili vijana hasa wanaomaliza vyuoni waweze kupata moyo wa kujiajiri kuliko kukaa kusubiri ajira za kuajiriwa.Fursa kwakweli kwa mtu anayeumiza kichwa kuzitafuta ziko nyingi sana sema kulalamika ndio imekuwa njia yetu ya kupoza machungu kwa wengi wetu,nilishawahi kuandika humu jamvini kuwa moyo wa kujituma na kujitolea unahitijika kwa mtu kama anataka kujiajiri maana sio lelemama yahitaji kujitoa kwa dhati na wakati mwingine bila kukata tamaa maana sio kila ufanyacho unaweza kufanikiwa kama mtu mmoja maarufu duniani Edson huyu alikuwa ni mvumbuzi wa 'bulb' tunazozitumia hii leo lakini katika tafiti zake za kutengeneza bulb alifail majaribio 1000 (1000 times) katika hali ya kawaida mtu unaweza kukata tamaa na msaidizi wake alishakata tamaa akamwambia kuwa anachokifanya hakiwezekani alichomjibu ni kuwa hajafail mara 1000 bali amejua njia 1000 ambazo haziwezekani.Hivyo kwa vijana wenzangu tuko na changamoto nyingi cha msingi ni kutokata tamaa
   
 9. w

  winner forever JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 1,097
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama CDM wana njaa na ulafi wa kukwapua rasilimali za nchi hadi kufikia wanafunzi kukaa chini,mahospitali kukosa dawa etc kama wanavyofanya hao wengine,
   
 10. M

  Mujwahuzia Senior Member

  #10
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nia yako si kujua CHADEMA itawasaidiaje vijana wasiokuwa na ajira tu hata kuwasaidia wenye akili mbovu kama yako kwani kwani kama ungetaka kujua chadema itawasaidiaje usingemaliza kwa kashifa uko mwishoni mwa maelezo yako. Hivyo jibu la kwanza chadema itaanzia kwako kukuomba uachane na mawazo potovu ya wanachadema ambao wanapambana na udhalimu wa nchi hii uliowafanya Wtz wawe masikini kila uchao.
   
 11. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  suala la kujiajiri si dogo mkuu!
  kumbuka vijana wengi wanatoka katika familia za kimaskini!
  wazazi wake wanamtegemea kuwa ndo mkombozi mara atakapohitimu masomo yake!
  uje umwambie ajiajiri atahitaji fedha za kupanga ofisi si chini ya milion moja kwa mwaka!
  atahitaji vitendea kazi zikiwamo furniture za office!
  atahitaji fedha za kuendesha ofisi huku biashara yake ikikuwa!
  atahitaji marketing ya bidhaa!
  tukumbuke hapo tu ndo ametoka masomoni!
  naomba tusijifananishe na hawa wenzetu wa huko ng'ambo embu tuambiane ni mtanzania yupi na amefanya kipi cha kuigwa na cha kutoa funzo kwa vijana wengine?
   
 12. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  wao wanautofauti gani wakati ni watu wale wale tena watanzania wale wale makabila yale yale, mazingira tunayoishi ni yale yale
   
 13. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Katiba kijana inahitaji usimamizi katika utekelezaji, kwanza katiba hiyo unayosema sio nzuri ndio maana kuna mchakato wa katiba mpya. Kwanza hawa wezi wanaofilisi nchi inahitajika waondolewe kwenye madaraka ili mambo mengine yapate kutekelezwa!! Kuna mambo mengi tuu yamekaa tenge, kama wewe sio mnafiki basi unajua nazungumzia nini, kama fedha zetu zilizofichwa nje ya nchi zinahitaji kurudishwa zisaidie maendeleo!!!

   
 14. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Tena kusimamia katiba na sheria, wezi woote na wala rushwa kuwekwa lupango (jela) ndiyo sehemu yao, sio wezi wawe kwenye majukwaaa ya siasa na wenyeviti wa tume za bunge linalotunga sheria!!!

   
 15. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  mkuu punguza jazba jaribu kuwa rational lengo hapa sio kashfa wala lengo si kujisingizia utakatifu ili mtakapoingia madarakani muwageuke watanzania hawa maskini!
  hebu tuangalie yaliyoipata kenya majirani zetu hapo walipowaweka akina kibaki! lakini uchaguzi uliofuatia ulishuhudia wimbi la mauaji!
  hebu tafuta hotuba za rais wa uganda alivyokuwa akiahidi kabla hajapata urais na leo hii alivyong'ang'ania madaraka na anavyomtesa kiza
  tunatakiwa tujue ukweli are you really committed or mnatuhadaa? kwanza mi nilidhani ungenijibu kwa hoja ili nikukubali lakini umeishia kunitusi! kumbuka wengi wanasoma hapa so unaposhindwa kujibu kwa hoja ila kwa matusi ni dharihi utatutia mashaka na cdm yenu buree
   
 16. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  nimekusoma
   
 17. Root

  Root JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,241
  Likes Received: 12,954
  Trophy Points: 280
  system of education inabidi ibadilishwe uwe ni ule unaomfungua mtu akili na sio ule wa kusoma ili ufaulu mtihani baada ya hapo unasahau kila kitu. Pia sisi kama wananchi tunatakiwa tuwe na ile hali ya kufikiria kujiajiri na sio kila mtu akimaliza chuo anaanza zunguka na bahasha kwenye.ofisi kufanya interview. Serikali pia ijenge jinsi ya kusaidia watu wanao onesha nia ya kujiajiri mfano kutoa motivation na awards mbali mbali kwa wavumbuzi wa ndani hii itacreate creativity ambayo at the end huu msemo wa ajira utapungua hapa kwetu. Ni maoni yangu nirekebishe nilipokosea
   
 18. data

  data JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,747
  Likes Received: 6,524
  Trophy Points: 280

  em mweleze huyo! Hajui kama CHADEMA ndo manabii tulokua tukiwasubiri,wenye uwezo wa kufanya wa TZ kujikuta tumelala maskini afu twaamka mamilione.. Mwambie bana
   
 19. w

  winner forever JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 1,097
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  CDM ina dhamira safi,kumbuka hawa wengine wameingia madarakani kwa rushwa na fedha chafu (baadhi yao),hivyo uongozi kwao ni biashara na kusafisha fedha chafu. Ndani ya CDM mchakato wa kupata viongozi ni wa kuzingatia uadilifu,uwezo,uwajibikaji etc na si vinginevyo. CDM inahitaji miaka mitano tu kuonyesha uwezo wako wa kutumikia wananchi,amka kabla hujaachwa nyuma,
   
 20. MADAXWEYNE

  MADAXWEYNE JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 718
  Likes Received: 1,826
  Trophy Points: 180
  Majibu kama haya hua yanapendeza,pia yanajenga CDM. Naomba na wengine wajaribu kuiga haya majibu na waache kubomoa CDM kwa majibu ya kashfa,kejeli na matusi.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
Loading...