Kijakazi
Platinum Member
- Jun 26, 2007
- 9,237
- 14,875
Ingawa ni ukweli ulio wazi kwamba Chama cha CHADEMA hakiwezi kushinda Uchaguzi wa Uraisi na Ubunge 2015, lakini ni jambo lililo wazi pia CHADEMA wamefungua njia ya mabadilko nchini mwetu!
Serikali ijayo ya CCM, haiwezi kuwa ya kisanii ukiilinganisha na ya sasa hivi, na nathubutu kusema pia Serikali zilizopita, na sio kwa sababu haiwezekani, bali ni kwa sababu CCM hawana jinsi bali kubadilika kwani kila siku zinavyozidi kwenda ndivyo watu wanvyozidi kuhoji Uhalali wao wa kuongoza, hivyo basi naweza kusema 2015 ndiyo karata ya mwisho kwa CCM, na kama wasipobadilika basi 2020 au 2025 CHADEMA kama wataendelea na kasi hii hii walionayo sasa hivi ni lazima watashinda Uchaguzi wa Uraisi na Ubunge!