CHADEMA mmeanza lini kuwaonea huruma CCM?

CHADEMA mmeanza lini kuwaonea huruma CCM?

Yes nakubaliana na baadhi ya mambo unayosema. Mimi ninaamini kwamba kura ya siri au ya wazi zote zinakidhi matakwa ya kidemokrasia ! Na kuna faida zipo kwa kupiga kura za wazi na baadhi umezitaja hapa. Hata hivyo ninaamini kura za wazi zitafanya baadhi ya wajumbe (especially wa CCM) wapige kinyume na vile ambavyo wangependa kupiga. Kwa sababu hiyo naona kura ya siri ndio muafaka kwani cha muhimu zaidi kwetu ni maamuzi sahihi zaidi ya kujua mtu gani alifanya maamuzi gani !

Kwa maneno mengine nikiambiwa nichague maamuzi sahihi au kujua nani amefanya maamuzi gani (in case siwezi kuvipata vyote kwa pamoja) nitachagua maamuzi sahihi !. Na ndio maana natetea kura ya siri !

Wananchi tutawajibu kwamba CCM wamewadharau kwa kubadilisha maamuzi yao kinyemela. Na hii tunaweza kuisema bila kumumunya maneno, kwani katika kubadilisha kutoka serikali 3 kwenda 2, hilo haliwezi kufanyika kwa kificho, litabadilishwa hadharani, na litatetewa hadharani, na watakaofanya hivyo...ofcourse watakuwa CCM !

uko sawa. niseme tu kwamba ccm znz wanataka serikali mbili zinafaida kubwa kwao na wanalielewa hilo, wananchi wao wengi hawataki.nielezee kidogo :nchi za afrika ni masikini kote afrika maji,umeme ,barabara,afya ni huduma za kusuasua sasa kwa znz viongozi wanautabia ya kusingizia kila jambo muungano,kiasi cha wananchi kujua tatizo lao ni moja tu muungano hiyo wanataka uondoe au zije serikali 3. sasa ukifanya kwa siri kwanza unakuwa umedumisha ulaji wa wana ccm znz , pili umekuwa umedumisha uwakilishi wao huko visiwani maana wataenda kuimba wimbo ule ule tulikuwa wachache wabara wengi wakapitisha.
waweke wazi kwani sababu si zipo zisemwe. sio uchawi kwamba unataka mbili bila sababu au tatu bila sababu.mambo yawe wazi.
 
CDM wanapinga kura ya wazi wanatoa hoja kuwa CCM wanataka kuwadhibiti watakaopinga serikali 3 na wanasema CCM wakiwajua hao watawafukuzwa uanachama.Swali langu linakuwa:CCM wakiwafukuza wanachama si itakuwa faida kwao?CDM wana huruma na CCM KWELI?
Come on Mburula!Issue sio faida gani CDM itapata mkiwafukuza wanachama wenu, issue ni uminyaji wa Demokrasia waziwazi, kwanini mtu asichague kwa siri akiwa huru? Matokeo yake tutapata matokeo ya katiba ambayo si matakwa ya wananchi bali ya Chama.Kweli we yaani unashindwa kufanya simple analysis ya kitu kiko wazi namna hiyo?
 
Kura ya siri ndyo itakayetoa demokrasia y kweli..wajumbe watapiga kura bila kuogopa ccm..

hao wajumbe hawana uwoga huo. wangekuwa na uwoga huo huko znz wasingekaa pamoja kuunda katiba ya znz ambayo imetikisa muungano, wasingekaa pamoja kwa sauti moja mafuta yasiwe ya muungano.hawaogopi lolote.hilo ni game limechezwa sendeka alikuwa akizingua tu ila serikali mbili zimepita.
 
Najiuliza hivi mnyika anaogopa kusema hadharani kuwa anataka serikali mbili au tatu? hivi mbowe anaogopa kusema hadharani anataka serikali mbili au tatu? sasa huo uwazi wanaogopa wa nini?

Nilitegemea Mbowe kuwaunga mkono wabunge wa ccm kura ya wazi ili wananchi tujue mbivu na mbichi.

Ccm mnafanya makusudi kujifanya mnajua zaidi kudanganya wale wenye uelewa mdogo juu ya mantic ya kura ya siri na wazi.

kiufupi kura ya SIRI ndiyo kura pekee ya kidemocrasia na kura ya wazi ni kumlazimisha mtumwa wako akutii unachotaka wewe kifanyike bila ridhaa yake.hivi viongozi wa kiroho wameshindwa kuishauri ccm mchakato uwe siri ili haki itendeke?
 
Come on Mburula!Issue sio faida gani CDM itapata mkiwafukuza wanachama wenu, issue ni uminyaji wa Demokrasia waziwazi, kwanini mtu asichague kwa siri akiwa huru? Matokeo yake tutapata matokeo ya katiba ambayo si matakwa ya wananchi bali ya Chama.Kweli we yaani unashindwa kufanya simple analysis ya kitu kiko wazi namna hiyo?

kama wanasimamia ya wananchi waliowachagua wanaogopa nini kufukuzwa? si wananchi waliowachagua watawachagua tena kwa chama kingine.
 
Ccm mnafanya makusudi kujifanya mnajua zaidi kudanganya wale wenye uelewa mdogo juu ya mantic ya kura ya siri na wazi.

kiufupi kura ya SIRI ndiyo kura pekee ya kidemocrasia na kura ya wazi ni kumlazimisha mtumwa wako akutii unachotaka wewe kifanyike bila ridhaa yake.hivi viongozi wa kiroho wameshindwa kuishauri ccm mchakato uwe siri ili haki itendeke?

mi naona kura ya siri ni mbaya sana maana ccm wanayo nguvu ya kuhonga sasa wakihongwa na kura kuwa hivyo wananchi watajua yupi msaliti, kwa nini isiwe wazi watanganyika kazaa kati ya kazaa wamesema serikali 3, wanz kazaa kati ya kazaa wamesema serikali tatu na majina yetu yawepo.

Ni kumbukumbu hata watoto wetu wakihoji wanakumbana na data, sasa baada ya miaka 20 wanaweza kuibuka waznz na kulalamika kura za serikali 2 zilipita kwa sababu wabara ndio walipitisha bila data hapo utakuwa na nguvu za kumpinga muhusika? tujenge mazingira ya wazi. kutaka serikali tatu sio dhambi bali hoja, serikali mbili nazo ni hoja tu.watu watoe hoja wazi zihifanywe huo ndio uwazi.

hatupitishi serikal 3 ili kuwanyonya tanganyika wala zanzibar, hatupitishi mbili ili kunyonya tanganyika wala zanzibar .mambo yawekwe wazi nachagua hizi mimi kama mnyka kwa sababu hii na hii ambazo katika mbili hakuna haki hii na hii. hapo ndio pazuri.
 
Mbona hao wabunge wa ccm zanzibar hutamka hadhari barazani kwao kuwa wanataka serikali tatu?mbona hata kificho kaandika barua kwa warioba iko wazi? Mbona kwenye kuandika katiba ya zanzibar hao wawakilishi wa zanzibar waliungana wakatunga moja? viongozi wa cdm wamekosea mi nilitaka kura ya wazi na bunge liwe live na kuwe na hansard za bunge kuwa kati ya wajumbe 600 ,kila mmjumbe kwa jina lake kujulikana alisema hivi.

Kura ni siri
 
uzi huu ni wakijinga ndio maana tpmazembe na deo ndio wanatiririka
 
mi naona kura ya siri ni mbaya sana maana ccm wanayo nguvu ya kuhonga sasa wakihongwa na kura kuwa hivyo wananchi watajua yupi msaliti, kwa nini isiwe wazi watanganyika kazaa kati ya kazaa wamesema serikali 3, wanz kazaa kati ya kazaa wamesema serikali tatu na majina yetu yawepo.

Ni kumbukumbu hata watoto wetu wakihoji wanakumbana na data, sasa baada ya miaka 20 wanaweza kuibuka waznz na kulalamika kura za serikali 2 zilipita kwa sababu wabara ndio walipitisha bila data hapo utakuwa na nguvu za kumpinga muhusika? tujenge mazingira ya wazi. kutaka serikali tatu sio dhambi bali hoja, serikali mbili nazo ni hoja tu.watu watoe hoja wazi zihifanywe huo ndio uwazi.

hatupitishi serikal 3 ili kuwanyonya tanganyika wala zanzibar, hatupitishi mbili ili kunyonya tanganyika wala zanzibar .mambo yawekwe wazi nachagua hizi mimi kama mnyka kwa sababu hii na hii ambazo katika mbili hakuna haki hii na hii. hapo ndio pazuri.

Mkuu acha kabisa kunaswa na huo mtego wa kura ya wazi ni hatari kwa katiba yetu.usikubali kabisa mkuu hapo kuna mtego utanikumbuka washauri na rafiki zako kura iwe siri tusifanye mchezo hii ni katiba ya watoto wetu na wajukuu sisi tutakufa soon huko mbinguni tutahukumiwa vibaya ndugu yangu.
 
Chadema ni chama cha upepo na matukio tusishangae kwa maamuzi ya ajabu ajabu.
 
CDM wanapinga kura ya wazi wanatoa hoja kuwa CCM wanataka kuwadhibiti watakaopinga serikali 3 na wanasema CCM wakiwajua hao watawafukuzwa uanachama. Swali langu linakuwa:CCM wakiwafukuza wanachama si itakuwa faida kwao?CDM wana huruma na CCM KWELI?
kuwapa tiba ya kichaa mbwa koko si lazima iwe huruma kwa mbwa,ila salama kwa viumbe wengine ambao watang`atwa na huyu mbw akichaa...........tafakari
 
Mkuu acha kabisa kunaswa na huo mtego wa kura ya wazi ni hatari kwa katiba yetu.usikubali kabisa mkuu hapo kuna mtego utanikumbuka washauri na rafiki zako kura iwe siri tusifanye mchezo hii ni katiba ya watoto wetu na wajukuu sisi tutakufa soon huko mbinguni tutahukumiwa vibaya ndugu yangu.

tatizo lako hutoi sababu ya kura ya siri na faida zake. mimi naongelea uwazi ambao watoto wetu wataukuta. niseme tu kwamba serikali mbili zinaifaidisha znz zaidi lakini tatizo ni viongozi wa znz kutowaambia wananchi wao faida za muungano na kutokuwa na uwazi katika muuungano wetu. uwazi katika muungano utasaidia wananchi wa pande zote kujua kweli waznz na watangy walikubaliana serikali hizi kwa data hizi. na muungano huu ni wa makubaliano pande zote mbili.
 
Sababu kuu ya kura ya siri ni kama ifuatavyo:
kura ya siri inatoa uwazi toka rohoni mwako ukiwa huru kabisa kufanya jambo ukiwa falagha bila kuingiliwa na mtu yeyote hata kama ni mke wako.
Huo ndo uwazi ulio sawia kabisa kwa kupiga kura ya siri.

Pili, kura ya siri mkimaliza mnabaki kuwa wamoja na kulijenga taifa

Tatu,kura ya siri imebeba rasmu ya wananchi ya muundo wa serikali 3.
Ukitaka uwazi ili watoto wetu wajuwe huyu ndiye aliyetupatia katiba mbovu hawatakaa waelewane hata siku moja na ugomvi utatawala daima.Lakini hata kama tutapiga ya siri katiba ikawa mbovu kama ya serikali 2 tutabaki wamoja ndugu yangu.
Nitashukuru sana kama utaunga mkono hoja chief asante.
 
CDM wanapinga kura ya wazi wanatoa hoja kuwa CCM wanataka kuwadhibiti watakaopinga serikali 3 na wanasema CCM wakiwajua hao watawafukuzwa uanachama.
Swali langu linakuwa:CCM wakiwafukuza wanachama si itakuwa faida kwao?CDM wana huruma na CCM KWELI?

Mbona umeandika pumba kiasi hiki? Tambua Wabunge wengi wa CCM ni wachumia Tumbo na hawana kazi nyingine zaidi ya Siasa hivyo iwapo kutakuwa na kura ya wazi hawawezi kuwa huru kwa kutoa maamuzi yao binafsi hivyo watatekeleza ya CCM na ndio maana viongozi wa CCM wanakazania hilo kwa kuwa wanajua udhaifu wa wabunge wao.
 
Huruma tunawaonea sana kuanzia kalenga na chalinze
 
CDM wanapinga kura ya wazi wanatoa hoja kuwa CCM wanataka kuwadhibiti watakaopinga serikali 3 na wanasema CCM wakiwajua hao watawafukuzwa uanachama.
Swali langu linakuwa:CCM wakiwafukuza wanachama si itakuwa faida kwao?CDM wana huruma na CCM KWELI?

Suala ni haki ya mtu kutetea akifikiriacho.Je,wadhani wabunge au wakilishi wote wa CUF na CDM wanataka serikali tatu?Hakuna kabisa ambaye yupo neutral au ambaye anapendelea serikali mbili?

Kura ya SIRI itamweka kila mtu kuwa huru kutumia nafasi na ubongo wake kuchagua akifikiriacho,hasa kwa wale waoga itawasaidia zaidi ambao wameshatishwa na wakatishika.Imagine Mbunge akose ubunge kisa ametetea jambo tofauti na chama chake yawezekana kweli?Atakula wapi?
 
CDM wanapinga kura ya wazi wanatoa hoja kuwa CCM wanataka kuwadhibiti watakaopinga serikali 3 na wanasema CCM wakiwajua hao watawafukuzwa uanachama.
Swali langu linakuwa:CCM wakiwafukuza wanachama si itakuwa faida kwao?CDM wana huruma na CCM KWELI?
Chadema wanachofanya sasa hivi ni kurusha ngumi hewani.
 
CHADEMA wanapinga kura ya wazi wanatoa hoja kuwa CCM wanataka kuwadhibiti watakaopinga serikali 3 na wanasema CCM wakiwajua hao watawafukuzwa uanachama.

Swali langu linakuwa: CCM wakiwafukuza wanachama si itakuwa faida kwao?CHADEMA wana huruma na CCM KWELI?
tatizo hapa sio kufukuzwa au huruma, tatizo ni kutuaribia katiba kabla ya kuwafukuza
 
Back
Top Bottom