CHADEMA mmeanza lini kuwaonea huruma CCM?

CHADEMA mmeanza lini kuwaonea huruma CCM?

Tutaikataa hiyo katiba kwenye kura ya maoni !

Na nina uhakika wabunge wengi especially wale wanaotetea maslahi ya wananchi kwa uwazi ambao ni CDM, nao wataungana na wananchi kuipiga chini hiyo katiba ! Tofauti ni kwamba kama kura itakuwa ya siri, ninaamini mchakato wa bunge maalumu utakamilika ila katiba itakwama kwenye kura ya maoni ! Ila kama CCM watalazimisha kura ya wazi ili wapitishe serikali mbili ninaamini hata mchakato katika bunge la katiba hautakamilika. Utasambaratika kabla ya kufika kwenye kura ya maoni !

vipi kama itapita kura ya siri na cdm watashindwa na serikali zao 3 wanazopigania?
 
Nani kasema tunawaonea huruma CCM ?

1. Tunawaonea huruma wananchi wanaotaka serikali tatu lakini CCM wanataka kulazimisha serikali mbili kwa kutumia wingi wa wabunge wao !

2. Tunajua kuna wabunge wa CCM ambao kama sisi wanataka kusimamia maslahi ya wananchi ila wanaogopa uongozi wa CCM

3. Sisi na hao CCM (wanaotetea maslahi ya wananchi) tunashare interest moja i.e. tuna lengo moja, ambalo ni serikali tatu kama wananchi wanavyotaka. Hivyo ni interest yetu kuwatetea hawa ili wawe huru kutetea maslahi ya wananchi kwani wakifanikiwa kutetea maslahi ya wananchi na sisi tutakuwa tumefanikiwa !

sasa ccm ikihonga,ikapigwa ya siri serikali mbili zikipita,mtawajibu nini wananchi? watamjuaje msaliti? kwani kama wanafanya maamuzi ya wananchi kwa nini waogope kufukuzwa na chama? maana kama wako na wananchi chama chochote wakigombea watapita tu. sasa uwoga unatoka wapi?

wananchi tunataka data,tunataka waznz wakilia muungano tuwaambie kwa data kuwa wawakilishi wenu 60 ,fulani na fulani walisema hivi na kuchagua hivi usimpige padri au mzungu asiye na kosa na muungano huu. maana wawakilishi hao wakija znz husema tatizo muungano wananchi wanajaa chuki wakija kwenye maamuzi wako kimya huu ni unafiki
 
CDM wanapinga kura ya wazi wanatoa hoja kuwa CCM wanataka kuwadhibiti watakaopinga serikali 3 na wanasema CCM wakiwajua hao watawafukuzwa uanachama.
Swali langu linakuwa:CCM wakiwafukuza wanachama si itakuwa faida kwao?CDM wana huruma na CCM KWELI?

Wakifukuzwa itakuwa hasara kubwa kwa CHADEMA.Kwani itakosa chama cha upinzani imara mwaka 2015.
 
Tutaikataa hiyo katiba kwenye kura ya maoni !

Na nina uhakika wabunge wengi especially wale wanaotetea maslahi ya wananchi kwa uwazi ambao ni CDM, nao wataungana na wananchi kuipiga chini hiyo katiba ! Tofauti ni kwamba kama kura itakuwa ya siri, ninaamini mchakato wa bunge maalumu utakamilika ila katiba itakwama kwenye kura ya maoni ! Ila kama CCM watalazimisha kura ya wazi ili wapitishe serikali mbili ninaamini hata mchakato katika bunge la katiba hautakamilika. Utasambaratika kabla ya kufika kwenye kura ya maoni !

utaikataa vipi angali bado ccm ni chama tawala, maana yake hata kura za wananchi wanaweza shinda kwa shwange na rushwa. wananchi wanategemea makubwa bungeni,wananchi wengi vijijini ambako ndio kuna watu wengi hawajui chochote kuhusu katiba, katiba ni tume na bunge ndio kazi kwa wananchi ni kupitisha tu.
 
Binafs sioni kosa la viongozi wa chadema,hii ni nchi yetu sote katiba ni ya watz,hata ccm wanakosea sana wanapo ingiza uccm kwenye bunge hili maalum la katiba,wabunge wote wa bunge hili wanapaswa kuweka pembeni itikadi za vyama vyao, nakufanya mijadala ya pamoja juu yanini kiwepo nini kisiwepo kwa maslahi yetu sote,wakimaliza majukwaa ya siasa mbona yapo tu,
 
Chadema ina uhakika gani kuwa kuna baadhi ya wajumbe wa ccm wanataka serikali 3? Leo cdm wanaamini kuwa hawa ccm tunaowalaumu daily ndo watabadilika na kututetea watanzania?
Kweli tunapoteza time huko bungeni kubishania hayo?
 
alama za mnafiki ni
1.........................?
2.........................!
3.........................!
4..........................!
5.........,...,............!

Kwa hiyo umeamua tu kumsema tpmazembe japo hujakusudia.
 
Last edited by a moderator:
Wakifukuzwa itakuwa hasara kubwa kwa CHADEMA.Kwani itakosa chama cha upinzani imara mwaka 2015.

Haaahaaa eti nasikia Itapigwa kura za siri kuamua kura gani itumike kwenye maamuzi! Ikipita ya wazi CDM mtafanyaje?
 
alama za mnafiki ni
1.........................?
2.........................!
3.........................!
4..........................!
5.........,...,............!

Zoote anazo mwenyekiti wako!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Yes nakubaliana na baadhi ya mambo unayosema. Mimi ninaamini kwamba kura ya siri au ya wazi zote zinakidhi matakwa ya kidemokrasia ! Na kuna faida zipo kwa kupiga kura za wazi na baadhi umezitaja hapa. Hata hivyo ninaamini kura za wazi zitafanya baadhi ya wajumbe (especially wa CCM) wapige kinyume na vile ambavyo wangependa kupiga. Kwa sababu hiyo naona kura ya siri ndio muafaka kwani cha muhimu zaidi kwetu ni maamuzi sahihi zaidi ya kujua mtu gani alifanya maamuzi gani !

Kwa maneno mengine nikiambiwa nichague maamuzi sahihi au kujua nani amefanya maamuzi gani (in case siwezi kuvipata vyote kwa pamoja) nitachagua maamuzi sahihi !. Na ndio maana natetea kura ya siri !

Wananchi tutawajibu kwamba CCM wamewadharau kwa kubadilisha maamuzi yao kinyemela. Na hii tunaweza kuisema bila kumumunya maneno, kwani katika kubadilisha kutoka serikali 3 kwenda 2, hilo haliwezi kufanyika kwa kificho, litabadilishwa hadharani, na litatetewa hadharani, na watakaofanya hivyo...ofcourse watakuwa CCM !

sasa ccm ikihonga,ikapigwa ya siri serikali mbili zikipita,mtawajibu nini wananchi? watamjuaje msaliti? kwani kama wanafanya maamuzi ya wananchi kwa nini waogope kufukuzwa na chama? maana kama wako na wananchi chama chochote wakigombea watapita tu. sasa uwoga unatoka wapi?

wananchi tunataka data,tunataka waznz wakilia muungano tuwaambie kwa data kuwa wawakilishi wenu 60 ,fulani na fulani walisema hivi na kuchagua hivi usimpige padri au mzungu asiye na kosa na muungano huu. maana wawakilishi hao wakija znz husema tatizo muungano wananchi wanajaa chuki wakija kwenye maamuzi wako kimya huu ni unafiki
 
Ni aibu kubwa ambayo inanipa shaka na uongozi wetu cdm

kweli wewe ni mwana CHADEMA Kweli? Kama ni kweli basi wewe uwezo wako ni mdogo sana ushauri jitahidi kufanya research kidogo tu utajua umuhim wa kura ya siri
 
Mkuu 2010 wananchi walikuwa tofauti kabisa na 2005 katika kufanya maamuzi. Na 2014 pamoja na 2015 ni tofauti zaidi !. Subiri tu ndugu yangu, si mbali ni mwaka huu huu....Kama bado unafikiri wabongo ni wale wale utashangaa sana !

Na hii ya kubadilisha maamuzi ya wananchi kinyemela ndio itakayowapa wananchi hasira zaidi !

utaikataa vipi angali bado ccm ni chama tawala, maana yake hata kura za wananchi wanaweza shinda kwa shwange na rushwa. wananchi wanategemea makubwa bungeni,wananchi wengi vijijini ambako ndio kuna watu wengi hawajui chochote kuhusu katiba, katiba ni tume na bunge ndio kazi kwa wananchi ni kupitisha tu.
 
Mkuu 2010 wananchi walikuwa tofauti kabisa na 2005 katika kufanya maamuzi. Na 2014 pamoja na 2015 ni tofauti zaidi !. Subiri tu ndugu yangu, si mbali ni mwaka huu huu....Kama bado unafikiri wabongo ni wale wale utashangaa sana !

Na hii ya kubadilisha maamuzi ya wananchi kinyemela ndio itakayowapa wananchi hasira zaidi !

hujanielewa nasema wanaachi hawaelewi maana ya katiba walio wengi hasa vijijinii hilo halihitaji elimu liko wazi. mchunga mifugo umwambie serikali mbili au tatu yeye ataona umuhiga gani nazo?au mkulima wa pamba au mahindi maana hazimuhusu. ila watu wanaumia wachache wanaoelewa ndio maan hata matokeo ya udiwani mabadiliko yanatokea mijini zaidi kwenye uelewa.
 
Chadema wanasumbuliwa na unafiki tuu, maana kushadadia ya ccm sijuwi maana yake nn, siku zote wanalilia uwazi leo wanataka usiri wa nn?
 
Mbona hao wabunge wa ccm zanzibar wanaoogopa kufukuzwa mbona waliungana pamoja na wacuf kusema mafuta isiwe ya muungano, kwa nini hawakuogopa kufukuzwa? angali Tanzania ilikuwa ikusua sua swala hilo. mbowe hapo anapotezwa na watu hao

Hiyo ya kura ya wazi ina nia ovu! Ukishasema kura tu, basi ni SIRI. Kura kama zile za ndiyooo ni unafiki mkubwa. Sawa na mtihani, kuna closed paper exams na open, ila njia inayokubalika sana ni CLOSED, sawa na Open ballot na closed(SIRI) ndiyo inayokubalika. Tafiti nyingi zote zinakubaliana modelities hizo za kufanya mitihani na kupiga kura,na CLOSED approach ndiyo Fair kwa nyanja zote!
 
kweli wewe ni mwana CHADEMA Kweli? Kama ni kweli basi wewe uwezo wako ni mdogo sana ushauri jitahidi kufanya research kidogo tu utajua umuhim wa kura ya siri

Kiukweli mi naelewa hayo yote, kura ya siri haina mashiko kwa wananchi, kwanza ccm ina nguvu za kuhonga, pili mwanaccm znz ni kama watakuwa wamebebwa na cdm kuitisha serikali mbili bila wananchi wao kujua. ndio maana hata ndani ya ccm Shamsi Vuai Nahodha alikubali kura ya siri. maana ccm zanzibar wanatafuna ruzuku yote inayotoka bara na kuwaeleza wananachi kuwa muungano ni tatizo hapo wananchi wao wataamini zimepita mbili wabara ndio wamepitisha, watu watazidi kuumizwa viongozi wa dini kuteseka pamoja na watalii kana kwamba ni watu wabaya. ipigwe ya wazi bunge liwe live wazanzibar na watanganyika waone wawakilishi wao wasiporizika nao wawawajibishe wawakilishi
 
Hiyo ya kura ya wazi ina nia ovu! Ukishasema kura tu, basi ni SIRI. Kura kama zile za ndiyooo ni unafiki mkubwa. Sawa na mtihani, kuna closed paper exams na open, ila njia inayokubalika sana ni CLOSED, sawa na Open ballot na closed(SIRI) ndiyo inayokubalika. Tafiti nyingi zote zinakubaliana modelities hizo za kufanya mitihani na kupiga kura,na CLOSED approach ndiyo Fair kwa nyanja zote!

Ndugu yangu nikuambia kabisa wabunge wa ccm znz wanaipenda sana kura ya siri na ndio walikuwa nyuma kuwapressure cdm waitete, watu wale ndio wanaitafuna znz na ndio wanaolalamika kwa wananchi kuwa tatizo ni muungano, wanapokea bil 4 kila mwezi, maji hakuna husema muungano,umeme shida muungano matatizo makubwa ni wao kutowaeleza waznz faida za muungano, nakuhakikishia pale bungeni kura ya siri zinapita mbili alafu watanganyika waliko znz wataendelea kuuwawa kwa chuki na kuteswa bila sababu. wapige kura ya wazi wananchi wabara wakipiga kelele tunawaeleza fulani na fulani wa bara walisema hivi na kumb zipo bungeni, waznz wakilalamika tunawaambia wajumbe wenu 60 kati ya 87 walisema hivi na majina yao yako bungeni na kumb.

nacho maanisha kama wawakilishi/wajumbe watakuwa wawazi kwa wananchi na kusimamia ya wananchi hata wakitoka chama fulani kwenda kingine watashinda tu maana wananchi ndio wanapiga kura.
 
CDM wanapinga kura ya wazi wanatoa hoja kuwa CCM wanataka kuwadhibiti watakaopinga serikali 3 na wanasema CCM wakiwajua hao watawafukuzwa uanachama.
Swali langu linakuwa:CCM wakiwafukuza wanachama si itakuwa faida kwao?CDM wana huruma na CCM KWELI?
Ndugu yangu issue ya kura za wazi au siri si ya vyama pekee. Inaenda beyond vyama. Uwazi huu unaotetewa utazaa mgawanyiko utakao kwenda hata nje ya bunge na hata ndani ya jamii na Imani zao. Subira tutaona kwa sababu mnairahisisha kwa kuifanya ni ya siasa za CHADEMA na CCM.
 
Kura ya siri ndyo itakayetoa demokrasia y kweli..wajumbe watapiga kura bila kuogopa ccm..
 
Back
Top Bottom