CHADEMA mlishakose kwenye hili...

nisile23

JF-Expert Member
Apr 11, 2013
440
176
Chadema hii nguvu mnayoitumia sasa baada ya Lissu kutangaza nia,mngeitumia katika kuhamasisha wafuasi wenu kipindi kile daftari la wapiga kura linaboreshwa na uandikishaji wa wapiga kura sahizi mngekuwa mnaongea mengine.

CCM ilihakikisha wanachama wake wanahakiki taarifa zao na wapya wanajiandikisha, lakini Chadema mlifanya nini?

Mlisahau watu wapo bize kutafuta vitambilisho vya Taifa, hawakuona umuhimu wa vitambilisho vya kura na mitaani hakuna aliyechukua jukumu la kuelimisha mliwaza nini?

CCM inawanachama wake ambao viongozi wa vijiji walipita nyumba kwa nyumba kuhakikisha wamefanya zoezi hilo ninyi mlifanya nini?
Mnajua kabisa uchaguzi wa serikali za mitaa uliwavunja wanachama wenu moyo nini mlifanya kukabili hali hiyo?

Maandalizi ya mashindano yanaanza mapema sio kipyenga kinapotaka kulia ndio unaingiza wachezaji kwenye zoezi.
Kwa hilo Magufuli keshawazidi point.

Mtajibu kwa mihemko ya mitandaoni Ila hii ndio hali halisi HAMKUJIPANGA MAPEMA..
 
Hivi wewe upo nchi gani? Huo uhamasizhaji wangeufanyia wapi? Hujui Kama haikuwa inaruhusiwa kwa miaka yote mitano kufanya siasa? kwenye kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura hakuna chama chochote Cha siasa au taasisi yeyoyete iliyo ruhusiwa kuhamasisha watu waende kujiandikisha, tume yenyewe ndiyo ilikuwa inafanya kazi hiyo ikisaidiana na ofisi za wakurugenzi, CCM haeakupita popote kuhamasisha watu wakajiandishe acha kupotosha

Uandikishaji wa awamu hii ni tofauti na uandishi wa mwa mwaka 2014-2015 wahamasishaji walikuwa wengi,,hata sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu hakuna taasisi binafsi ambazo zimeruhusiwa kutoa elimu kwa mpiga kura Kama ilivyo zoeleka

Nimehusika kwenye kuboresha daftari la uchaguzi sikuona ccm wakileta watu wao.ndani walikwepo mawakala wa kila chama.
 
Hao wanachama wa ccm ndio wataipigia kura chadema, nao wanaisoma namba vilevile. Watanzania wanahitaji mabadiliko ya maisha, hasa mifukoni. Huko kwingine (ndege, umeme, SGR, mifugale etc) kulikuwepo na kutaendelea kuwekezwa hata aje nani.

Si kweli wapinzani watauza screpa, ni mawazo mfu
 
Upo sahihi.

Maandalizi ya vita hufanyika wakati wa Amani na Kanzu ya Ijumaa Huandaliwa Alhamis
 
Back
Top Bottom