Uchaguzi 2020 CHADEMA, mlituahidi kampeni nyumba kwa nyumba lakini mnaruka Wilaya na Vijiji kwenye misafara yenu

puza46b

Member
Nov 3, 2010
91
261
Huu ni ushauri wa bure: Ni makala yangu ya pili leo maana mmenitibua CHADEMA. Mkitaka kujua hasira zangu zimeanzia wapi kasome hii Anayesimamia Idara ya Habari CHADEMA anakihujumu chama

Nimeona mmetoka Dar - mkaenda Arusha, kisha Mwanza halafu Shinyanga, sijui nia ni kujaza watu kwenye kampeni au kufikisha ujumbe wenu kwa wananchi

Sababu kubwa ya kampeni ni kuwaelimisha wananchi kuwa mfalme wanayemuamini ni kichaa na afai kuongoza nchi.

Sasa basi:

· Kuna uwezekano kuwa nia ya kwenda kwenye makao makuu ya mikoa ni kuonyesha kuwa chama kinakubalika. Nadhani hilo lishaonekana na ujumbe umefika.

· Kushinda uchaguzi ni kupata wapiga kura wengi. Asilimia 80 ya watanzania ni wakulima na wanaishi vijijini. Wengi hawazipati tena taarifa zenu kwasababu radio na magazeti yametishwa na sababu zake nilizifafanua hapa Kwenye Vita ya Uchaguzi CCM wameshachagua nini wanatoa kafara

· Hivi mtafikishaje ujumbe vijijini kama hamsimami na kuongea nao.

Ushauri:
· Angalieni kampeni za Marekani, kuna kitu wanaita town halls meeting. Wanaenda mji kwa mji kufikisha ujumbe. Hawajali kama wako watu watatu au watu laki moja. Wanachojali ni ujumbe umefika.

· Pangeni safari zenu mmfanye mikutano mingi kwa siku. Kwa mfano mikutano ya wikiendi mnaweza kufanya mitatu kwa siku. Kila wilaya mnasimama kwenye safari yenu. Mlifanya vizuri sana mlipokuwa mnatoka Iringa kwenda Mbeya naombeni mrudie hili.

· Pangeni safari zenu ili mpite kila mahali na pia iwapunguzie gharama. Kwa mfano, mlipokuwa Dar. Mgeendesha gari kuelekea Arusha. Mgesimama, Kibaha, Chalinze, Segera, Korogwe, Mombo mpaka mfike Arusha. hata kama safari itachukua siku tatu, muhimu ni mnaacha mbegu ya mabadiliko. Wale waliowaona wataenda kuongea na watu wengine, watawafanyia kampeni.

· Tumieni wabunge na madiwani wenu kuwafanyia kampeni za Urais.

Nakumbuka 2015 kuna mgombea alikuwa ananitafuta aniombe nimtumie hela kwa sababu ameishiwa na hakuweza kulipia posters za kampeni. Nikamuuliza kwanini hamna poster moja yenye tangazo la Rais, mbunge na diwani? Akaniambia hao viongozi wametusahau sisi wabunge. Hili ni kosa kubwa, wabunge na madiwani ni foot soldiers. Mtaua ndege watatu kwa jiwe moja mkiunganisha hizi kampeni.

· Nendeni hata kule ambako hamkubaliki. Narudia tena, muhimu ni kufikisha ujumbe siyo kujaza watu kwenye viwanja.

Msikubali CCM wawape changa la macho mkangangania kushindana nao kujaza watu uwanjani. CCM wana wajumbe nchi nzima ambao wanawafanyia kampeni.

Mwisho ningependa kuongelea niliyoyasikia jana kutoka kwa mwanakijiji aliyekuwa na chachu ya mageuzi 2015. Akaniambia watu wengi wanaomba huu uchaguzi upite tuu. Huyu jamaa alikuwa amekunywa bendera ya CHADEMA 2015 hasikii wala haelewi. Leo anaonyesha kuwa wengi wamekata tamaa, wengi wamesahau nini maana ya kuwa huru na maendeleo, wengi wanahitaji elimu. Hiyo elimu wataipata kama kampeni za CHADEMA zitawafikia wote.
 
CCM waliahidi kitanda kwa kitanda, mtu kwa mtu. Nimelala kitandani kwangu hapa nasubiri mrembo wa CCM aje kunishawishi hajafika hadi sasa. Hebu njooni kabla sijakasirika niwapigie wapinzani.
 
Waache kutoa ahadi za uongo hao,Et nyumba kwa nyumba wakati hata wilaya kwa wilaya yenyewe hawapiti
 
Wabunge Walichangishwa hela kwa madai ni za uchaguzi. Leo mnachangisha wananchi mnaodai maisha yao yakoo Duni mntaka kuwakomboa kama kweli maisha yao yakoo Duni kwa nini Mnaamini Kuwa wanahela, je wanazitoa Wapi Kama Sio Kwenye Maendeleo Waliyoletewa na MAGUFURI mhujumu Wa CHADEMA NI MBOWE.MSIWAZE MTAMWONA MAGU AKIWA ANAAPISHWA TENAA
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom