CHADEMA Mkituangusha hatutawasamehe

CHADEMA Mkituangusha hatutawasamehe

In theory ambayo wengi wanaiamini ni wapiga kura.
In reality inategemeana na hali ya nchi.

Wape taarifa tu kwamba watalegeza huu upuzi wa CCM na TISS kutupangia nani atawale mwisho ilikuwa 2010 vinginevyo tuingie kwenye umwagaji wa damu tu kwa sababu kuna ving,ang.anizi wanaodgarau maamuzi ya wananchi be careful
 
Chadema bana mara wanadai hawawezi kushinda urais bila katiba mpya,mara ushindi utategea tume hutu mara oooh mawakala! Mtaishia kuwa kama swahiba wenu Raila Odinga na mfahamu fika kuwa watanzania ni watu wa kukata tamaa. Walianza na Mrema wakaja kwa Lipumba sasa hivi wapo kwa Slaa na post 2015 wataboreka tena utasikia wapo chama cha Dovutwa!
 
:A S-heart-2:
Kumnyang'anya CCM TONGE mdomoni si kazi rahisi yuko tayari kupigana ili asipokonywe TONGE au ulaji. CHADEMA inahitaji maarifa zaidi ili iweze fanikiwa katika hili. Nahisi harufu ya damu 2015.

Uko sawa!Smtm ninaona Ma-people wengine wanadhani ni kazi rahisi kupambana na kuwang'oa magamba ya kugambana kunako sinia!!!La hasha, hawa jamaa ni makamanda pia wako na chapaa,dola na watu kiasi,tena haswaa ni mabingwa wa propaganda ambazo ndizo zimeua utendaji 'HAI' ktk mfumo mzima ndani ya serikali.,tumefika pabaya pa kubaguana,c kichama,kidini,kikanda na hata kikabila tulikosalimika."LEO HII KUSEMA KWELI KUNAGHARIMU MAISHA NA MATESO"NDANI YA TAIFA LILILOJAALIWA NA KUBARIKIWA",hivyo kama ni damu ishamwagika siku nyingi katika harakati hizi za mapambano ya mabadiliko ya mfumo ndani ya TAIFA hili,tangu enzi CUF imeshika usukani.Kilichobaki nadhani ni maamuzi ya ccm kwani ndicho kilichoshika ufunguo wa taifa hili kwa sasa pamoja na kuchanganyikiwa kwingi BUSARA NI IPI,KUACHIA UPEPO WA MABADILIKO UCHUKUE NAFASI KWA NAFASI AU KARAMU YA DAMU???Mh!kwa tunavyoenenda ninafikiri hawa jamaa washachagua damu.
 
Ikifika mwaka 2015 itakuwa ni miaka 20 kamili imepita tangu kufanyika kwa uchaguzi wa kwanza ulioshirikisha vyama vingi mwaka 1995 tangu kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi uliokuwa umepigwa marufuku miaka 30 kabla, yaani mwaka 1965. Kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 inaonekana mchuano utakuwa kati ya CHADEMA na CCM.

Kwenye mazoezi na mechi za utangulizi (Chaguzi ndogo) CCM inaonekana kuzidiwa kwa kupunguziwa viti ilivyokuwa inavishikilia kuanzia ngazi ya vitongoji hadi kwenye ubunge na CHADEMA ikiongeza idadi ya viti vyake sehemu mbalimbali za nchi.

Lakini kwenye uchaguzi wa mwakani ni uchaguzi ambao hautatoa nafasi kwa chama chochote kile kutumia viongozi wa kitaifa au maarufu kufanya kampeni nchi nzima. Uchaguzi wa serikali za mitaa kampeni zake hufanyika kwa siku saba tu. Na chaguzi hizo kwa uzowefu hukabiliwa na dosari nyingi (irregularities) sana na rafu (Rigging) za kutisha. Na ili kukabiliana na dosari na Rafu hizo CHADEMA inatakiwa kuwa na mtandao mpana wa chama ulio Imara.

Toka leo hadi uchaguzi wa mwakani inahitaji juhudi za ziada kujenga mtandao Imara wa chama. Na ujenzi wa mtandao huo huitaji sana fedha ambazo naamini CHADEMA hawanazo. Ule mpango wa kuichangia CHADEMA kwa njia ya simu sijui umeishia wapi? Ilitakiwa kila mwezi angalau wananchi wengejulishwa ni kiasi gani kimekusanywa ili kujenga hamasa na kufanya wanachama wenyewe wajitathimini ni kwa kiasi gani wanachangia chama chao. Bila fedha (Halali lakini) hakuna siasa endelevu kwa vyovyote vile.

CHADEMA inahitaji zaidi ya watu lakini moja kuwa wagombea kwa upande wake kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na maelfu mengine kwa ajili ya mawakala. Nguvu kazi hiyo na wagombea hao ni lazima wawe wametayarishwa tangu mwaka huu na wala si mwakani wakati wa uchaguzi.

Kuna kazi ya msingi ya kufanya kabla ya uchaguzi wa mwakani kama ndiyo msingi wa ushindi kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015. CHADEMA Msituangushe.
Mkuu Kigarama, nimekusoma na nimekuelewa.
Kuhusu uwezekano wa Chadema kuchukua nchi, 2015, mimi binafsi nimeisha zungumza sana, baadhi ya ma great thinkers wetu humu, kina Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Mchambuzi, Mag3 na wengine, pia wamesema sana!, I doubt kama Chadema wanamacho ya kuona, na masikio ya kusikia!.

Kwa vile wengi wetu humu ni watu wa "hopes" tuu (hope for the best) wana too great expectations kuwa Chadema "lazima" itachukua nchi 2015, hivyo ikitokea Chadema ikashindwa kuchukua nchi 2015, wataishia kwenye despair!, hivyo wengine wetu mimi nikiwemo sio watu wa just hopes bali ni ma "realist" kuhusu kuchukua nchi 2015!, Ikulu haitolewi kama "mana", it got to be earned!. Ili kuipata, lazima uonyeshe utayari wa kuingia ili wananchi wenye uamuzi wa mwisho, wakuaminie, wakukabidhi nchi yao!.

Sasa to be honest, hili la utayari kwa Chadema kuchukua nchi 2015, mimi bado sijaliana, ila naamini bado wanaendelea kujipanga!. Katika muda huu wanapojipanga, as a realist, nawaandaa watu wao kisaikolojia, "not only to hope for the best, but also to get prepared for the worst!, kuwa 2015, ni CCM Tena!. This is the very bitter pill they'll have to swallow kwa kutokujipanga kwao!.

Ukipata nafasi, unaweza kupitia nyuzi zangu hizi, kuona nilianza kulisemea hili lini, tulishauri Chadema ifanye nini, na kulinganisha ya kwa sasa Chadema inafanya nini, hivyo unaelewa 2015 kitatokea nini!.

Pasco.
Fanya Rejea on
  1. CCM Imechokwa; CHADEMA Haijajipanga!
  2. Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...
  3. Yametimia!, CCM Imechokwa!, Chadema Njia Nyeupe 2015!-Jipangeni
  4. Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio ...
  5. CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015
 
Kumnyang'anya CCM TONGE mdomoni si kazi rahisi yuko tayari kupigana ili asipokonywe TONGE au ulaji. CHADEMA inahitaji maarifa zaidi ili iweze fanikiwa katika hili. Nahisi harufu ya damu 2015.
ni kweli mkuu, hakuna mtawala yoyote duniani aliyewahi kuachia madaraka na kumkabidhi mpinzani kirahisi na kama huyu basi ni kwa shinikizo; CDM lazima watumie mbinu za kisasa kuidhibiti CCM.
CCM ina mkono mrefu sana tena wana support ya dola; Pamoja na katiba mpya, Tume huru ya uchaguzi lakini kumbukeni lazima CDM kiwe na mbinu kuwakabili hawa watu, na CDM lazima ije na plan B, endapo mambo haya yataenda kama ilivyokuwa 2015.

Pale segelea masanduku yalibebwa usiku wa manane, watu tuliona kabisa na police walishuhudia lakini kiko wapi? kesi ile imefia mahakamani, Pale ubungo na kawe bila kukomaa kwa wananchi ngoma ilikuwa isambe. sasa 2015 wizi huu utakuwa wa waziwazi kwa ulinzi wa vyombo vya dola.

Nachokiona mimi CCM watajaribu kwa namna yoyote ile, kufanya chochote kile ili wabakie madarakani, na kukuhakikishia hilo CCM haina dalili hata moja ya kuanza mchakato wa namna ya kukabidhiana dola endapo itashindwa 2015. we waambie kuhusu kuanzisha mchakato huo uone wakatavyong'aka. Na muda uliobakia hadi 2015 hawawezi kufanya lolote la kuwafanya wananchi wa Tanzania wawaamini tena.

CCM wapo radhi kutumia mbinu zozote zile zinazowezekana kuhakikisha CDM haitafika 2015, wanataka kutawala nchi hii milele; na nawaambieni kwa dalili nizionazo mimi ni vita ya ajabu sababu wananchi hawatakubali kuburuzwa tena, Baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 mtaanza kuona picha halisi ya nini nachokiongea.

nahisi Gharika kuu 2015, watakaopona wataandika historia.
 
Hapo umenena MKUBWA,

CDM TAIFA MIKAKATI IWE NI ELIMU KWA UMMA WA VIJIJINI.

YALE MAFUNZO YALIYOTANGAZWA ZIWE KWA UPANDE WA VIJIJINI ZAIDI.
 
Miye yangu macho tu; lakini nani atalaumiwa kama wote tumeweka mayai yetu kwenye kikapu kimoja ambacho hakiachi kutikiswa, kurushwa rushwa na kugongwa gongwa? Do we need another credible alternative opposition? Tunaweza kujifunza chochote toka kikapu cha Raila?
Mzee sauti yako inasikika kwamba mbali sana kama ya Pasco. Unaweza kuongeza sauti kidogo??
 
Last edited by a moderator:
Mwanamke anayependwa na anajua anapendwa na kila mtu huringa; anajua kuwa bado anapendwa. Mwanamke wa namna hiyo na mwenye uzuri wake wa asili haitaji mapambo mengi kuvutia suitors; ana uhakika watakuja tu. Kama siyo mwenye hekima basi anaweza kutegemea uzuri wake kama mtaji wake wa pekee. Lakini atakapoanza kukongoroka na uzee ukaanza kujionesha ataanza kuona kuwa wadau wanapungua kwa kasi. Wakati huo ataanza kujitahidi kuukumbushia uzuri wake kwa mapambo, manukato na hata kujiachilia kirahisi. Hata hivyo, wale wale waliokuwa wanampenda zamani wanaweza kujikuta wamepata kigori mwingine. Hili pia laweza kusemwa kwa wanaume kwa namna yake.

CDM ni kama mwanamke anayependwa na anajua kuwa anapendwa...
 
Mfano mjarabu kabisa kwa hali iliyopo!! Lakini wanaona?
 
Wajameni mie nasema kama kweli tunataka mabadiliko hapa Chadema ni wewe na mie tunaposema Chadema wasituangushe tuna maana kwamba ati viongozi wakitaifa watoke Dar-Es-Salaam kwende kila kijiji cha nchi hii no hapa cha msingi kama mpenda maendeleo atleast nasi tuwe mbele kama wenzetu ambao miaka ya zamani tulikuwa nao basi pale ulipo wewe/mie tuanze mkakati nafahamu Chadema hatuhitaji mipesa ya kutoa RUSHWA kama Maccm so we need to be serious kwenda nyumba hadi nyumba kijiji hadi kijiji ambacho kiko jirani na uishipo/niishipo tuwape waTanzania elimu ya Uraia wafahamu nini nchi yao inavyokwenda nini faida za kujiandikisha na kupiga kura so hapo 100%tutatoka na ifikapo 2015 kuanzia Januari mwendo ni ule ule kuwapa somo raia kila kona.Tusiwasubirie kina Mh Mbowe,Dr Wilbrod Slaa,Mh Mnyika, Mh Zitto,Mh Lema, na wengineo ati waje kila kona i mean tuishipo wewe/mimi ili wafanye kazi,ni jukumu letu sote kwa manufaa ya Taifa letu hakuna chama kingine ambacho kitatuletea maandeleo kama Chadema huu ni ukweli,nasema hivyo kwa kuwa sasa afadhali tunafahamu mambo mengi na sheria zetu kama raia tofauti na zamani vyama vipo lakini vinaficha kile ambacho kinaendelea ili tu kutufumba macho ili tusiwatilie vitumbua vyoa mchanga lakini leo hii aaah tunafahamu nini kinaendelea na hizi zote ni juhudi za Viongozi wa Chadema,Wanachama,Wapenzi wenye kufahamu nchi inavyotafunwa na wachache kwani siku hadi siku wanatumegea nini kinaenndelea hata kwa yale ambayo yalipita miaka ya nyuma.Huu ndio wakati wetu kujitoa ili hata familia zetu baadae waje kujinufaisha na rasilimali zao.Mwisho nawapenda sana watu wa mikoa ya kusini Lindi na Mtwara kwani sasa wanafahamu nini maana ya haki yao na hakuna wakuwadanganya hata kama kuna mwanasiasa njaa akapewa RUSHWA na MACCM kwani MACCM huwaga yanajali matumbo yao tu lakini hawatetereki na wakiwagundua wanasiasa njaa ambao wanawazunguka huwaga wanawapa live big up we shall take over YES WE CAN
 
Mkuu Kigarama, nimekusoma na nimekuelewa.
Kuhusu uwezekano wa Chadema kuchukua nchi, 2015, mimi binafsi nimeisha zungumza sana, baadhi ya ma great thinkers wetu humu, kina Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Mchambuzi, Mag3 na wengine, pia wamesema sana!, I doubt kama Chadema wanamacho ya kuona, na masikio ya kusikia!.

Kwa vile wengi wetu humu ni watu wa "hopes" tuu (hope for the best) wana too great expectations kuwa Chadema "lazima" itachukua nchi 2015, hivyo ikitokea Chadema ikashindwa kuchukua nchi 2015, wataishia kwenye despair!, hivyo wengine wetu mimi nikiwemo sio watu wa just hopes bali ni ma "realist" kuhusu kuchukua nchi 2015!, Ikulu haitolewi kama "mana", it got to be earned!. Ili kuipata, lazima uonyeshe utayari wa kuingia ili wananchi wenye uamuzi wa mwisho, wakuaminie, wakukabidhi nchi yao!.

Sasa to be honest, hili la utayari kwa Chadema kuchukua nchi 2015, mimi bado sijaliana, ila naamini bado wanaendelea kujipanga!. Katika muda huu wanapojipanga, as a realist, nawaandaa watu wao kisaikolojia, "not only to hope for the best, but also to get prepared for the worst!, kuwa 2015, ni CCM Tena!. This is the very bitter pill they'll have to swallow kwa kutokujipanga kwao!.

Ukipata nafasi, unaweza kupitia nyuzi zangu hizi, kuona nilianza kulisemea hili lini, tulishauri Chadema ifanye nini, na kulinganisha ya kwa sasa Chadema inafanya nini, hivyo unaelewa 2015 kitatokea nini!.

Pasco.
Fanya Rejea on
  1. CCM Imechokwa; CHADEMA Haijajipanga!
  2. Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...
  3. Yametimia!, CCM Imechokwa!, Chadema Njia Nyeupe 2015!-Jipangeni
  4. Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio ...
  5. CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015

Kama kweli tuna mapenzi na Nchi yetu ni kwa nini msitupe atleast,Chadema wajipange kivipi au wewe serious kivipi kama umeleta issue kama hii na umepoteza muda wako kuandika naona itakuwa vyema ukaweka nini Chadema wafanye na vipi wakabiliane na mapambano haya ya kuingia ikulu kama ulivyosema kwama ikulu haitolewi kama (Mana) tupe angalau hint na kumbuka kama ukitoa mchango wako wa ukweli tutakukumbuka maika ijayo kuwa oooh Pasco,Mzee mwanakijiji,Ritz walisema haya yatokeayo now kwa upande wangu mie namkubali Mchambuzi kwa jinsi anavyochambuua mambo yenye akili huyu jamaa hakunaga sio kama hao niliowataja maake wao hawaeleweki wako wa nchi gani!!Mchambuzi hayuko kichama japokuuwa ni mwanachama wa chama flani kama sikosei lakini yeye anasimamie ukweli na uwazi hakika ni Mpenda maendeleo anaweza kuwa kiongozi na sio mtawala.
 
Mkuu Mboko, kila kitu kimesemwa humu

Pasco.
 
Mboko kwanza ni makosa kumuingiza mtu kama Mzee Mwanakijiji kwenye kundi la kina Ritz kwani hawafanani hata kidogo. Ritz na wenzake wanafahamika kwamba ni "Watani" wa wana CHADEMA na wakati mwingine huwa nawashangaa wana CHADEMA wanapowachachamalia hawa jamaa. Unataka Sumu aisifie CHADEMA? Au unataka eti utaifakwanza aje na mikakati ya kuiondoa CCM madarakani, kweli!?

Pasco yeye tayari ameshatangaza maslahi yake kwamba anamuunga mkono Lowassa na ameshasema mara nyingi ni kwa nini. Kwa hiyo kuchukia chaguo la mtu huo nao si mfumo wa kufuatwa na wanademokrasia, tumuache ikifika mahala tukamshibisha kwa hoja zetu basi anaweza kubadili mawazo yake.

Sielewi ni kwa nini Mboko unataka watu wafanane kwenye kuchambua mambo. mwanakijiji aliandika mambo mengi sana mwaka 2010 na yote yakatokea, ushauri wake ulionekana unataka kuijenga CCJ chama alichokuwa anakishabikia sana na kwa taarifa yako mpaka leo Mwanakijiji anaamni kuwa kama nchi tunahitaji chama kingine imara cha upinzani zaidi ya CHADEMA au sivyo CHADEMA yenyewe ifanye juhudi ya kuwa imara. Hayo ni mawazo ya mwanakijiji na ni lazima yaheshimiwe kama tunavyotaka ya kwetu pia yaheshimiwe.
 
CHADEMA inahitaji zaidi ya watu lakini moja kuwa wagombea kwa upande wake kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na maelfu mengine kwa ajili ya mawakala. Nguvu kazi hiyo na wagombea hao ni lazima wawe wametayarishwa tangu mwaka huu na wala si mwakani wakati wa uchaguzi.

Kuna kazi ya msingi ya kufanya kabla ya uchaguzi wa mwakani kama ndiyo msingi wa ushindi kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015. CHADEMA Msituangushe.
Mkuu Kigarama, japo bandiko hili ni la zamani, lakini lina hoja za msingi sana kwa muktadha wa kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2020. Kama serikali za mitaa bila Chadema, what are the chances ya uchaguzi Mkuu wa 2020.

Mimi yangu ni haya
Huu ndio ukweli wenyewe. Hebu tuchangie bila povu wajameni.

Mkuu Magonjwa Mtambuka, asante sana kwa hii kitu. Huyu ni mmoja wa ma Prof wa ukweli ninao waaminia, hivyo naunga mkono hoja ya Prof. Safari.

Tulisema humu akina sisi,

Kuna kitu hapa kilisemwa na Masha

Kikapuuzwa, sasa leo kusema Prof. Safari, haya sasa manazi wa Chadema, njooni mumponde kama kawaida yenu.

Mkiambiwa
Mnakasirika

P.
 
Back
Top Bottom