CHADEMA mkiishindwa na CCM safari hii mjiue! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA mkiishindwa na CCM safari hii mjiue!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, Feb 24, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  HALI ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Arumeru Mashariki, bado si swari baada ya mchakato wa kura za maoni kumpata mgombea wa chama hicho katika kinyang’anyiro cha ubunge kukamilika, Raia Mwema.
  Ingawa mshindi katika kinyang’anyiro hicho amepatikana ambaye ni mtoto wa Mbunge aliyetangulia, marehemu Jeremiah Sumari, Sioi Sumari, wenzake wamelalamikia ushindi wake wakidai umetokana na matumizi ya fedha na si kukubalika kwake kisiasa wakionya kwamba, ameshinda ndani ya chama kwa nguvu ya fedha, lakini nje ya chama hicho, hali itakuwa ngumu kwake kushinda.

  Katika hatua nyingine baadhi ya washindani wake wamedai kuwa hata kanuni za CCM hazijazingatiwa ambazo zinataka mshindi wa kura za maoni apate zaidi ya asilimia 50 ya kura zote lakini kwa upande wa Arumeru Mashariki, ameshinda kwa asilimia Kama mgombea huyo atapitishwa katika vikao vingine vya juu vya CCM ambavyo ni Kamati Kuu na Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho 34.91, ambayo ni sawa na kura 361 (34.91).


  Kijana huyo wa marehemu Sumari ambaye pia kwa sasa ni Mkwe wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, alifuatiwa kwa idadi ya kura na William Sarakikya aliyepata kura 259 ambazo ni sawa na asilimia 25.


  Wengine waliofuatia katika kinyang’anyiro hicho ndani ya CCM ni pamoja na Elirehema Kaaya aliyepata kura 205 sawa na asilimia 19.82; Elishilia Kaaya kura 176 sawa na asilimia 17.02, Antony Musani kura 22 sawa na asilimia 2.12 na Rashiankira Urio aliyeambulia kura 11 ambazo ni sawa na asilimia 1.06.


  Kwa upande mwingine, wepesi wa kampeni za mgombea huyo wa CCM kama atapitishwa na vikao vya juu vya chama hicho utategemea zaidi na ushirikiano kutoka kwa washindani wake hao kwenye kinyang’anyiro hicho ambao baadhi wamesikika wakisema mwenzao huyo alitumia fedha kupata ushindi huo.


  Uchaguzi wa Arumeru Mashariki utarajiwa kufanyika mapema Aprili, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Jeremiah Sumari, ambaye alifariki dunia kutokana na maradhi ya saratani yaliyokuwa yakimsumbua.


  Wakati wa awamu ya kwanza ya ubunge wake, Sumari alipata kushika wadhifa wa Naibu Waziri hadi Serikali ya awali chini ya Waziri Mkuu, Lowassa, ilipovunjwa mwaka 2008 na kuundwa nyingine chini ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Wajiue kwa lipi? Kwani kuvunjika kwa koleo ndio mwisho wa ujenzi
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kichwa cha habari hakijakaa sawa.Kwanini wajiue?? Demokrasia maana yake nini? Think twice men!!
   
 4. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Mbona Chama Cha Mafisadi-CCM hakijajiua baada ya kugaragazwa kwenye majimbo mengi mwaka 2010?
  Tunajua CCM ni waizi wa kura. Hakuna ushindi wowote ambao CCM wanaweza kushinda kihalali. Huo ndiyo ukweli.
  Take from me: Kama CCM watafuata sheria na kanuni za Uchaguzi kiukweli hawawezi kushinda jimbo lolote nchi hii labda iwe kwa miujiza!
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Believe me or not, EL will be a stumbling block for CDM's trophy
   
 6. Chali wa Moshi

  Chali wa Moshi JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hii hoja haina mashiko. kwani asiyekubali kushidwa si mshindani.
   
 7. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  majimbo mengi kuliko chama gani labda???

  pili kama mnajua mnaenda kushindwa kutokana na hicho mnachotakiaminike kwamba mnaibiwaga kura kwa nini mnapoteza muda kushiriki chaguzi mbalimbali kila siku na kutangaza mnaenda kushinda?huwa mnakua na mning'inio mnapotamka hayo au?acheni siasa za maji taka,tumewashauri kwa muda mrefu bila mafanikio mumsimamishe heavy weight politician mr.wilbroad slaa pale mmeleta ukaidi na kusema yule dogo anaweza,tunataka tuone sasa tena habri njema ni kwamba mnayo advantage ya mtafaruku ccm uliotokana na kura za maoni,sasa itakua si ajabu kushindwa kwenue na ccm bali ya mwaka kushindwa na ccm dhaifu yenye madonda na majeraha ya kura za maoni kumpata mgombea wao,ama hakika hiki ni kipimo cha kama kweli chadema ni maarufu kama watu humu wanavyotaka tuamini au umaarufu unaishia arusha mjini na kibororonyi kidogo na pale Hai kwa mzee..
   
 8. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mnaanza kuweka akiba ya maneno ya kuhalalishia kipigo kabla sio?
   
 9. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Na wewe mleta mada utajiua CCM ikishindwa na CDM?
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Hata kama hali ingelikuwa shwari isingekuwa tatizo kwa CDM.
  CDM wamejiandaa vya kutosha kulichukua jimbo lao!
   
 11. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  hapana kwa kuwa chadema inaingia kupambana na mwigulu peke yake yenyewe ikiwa imekamilika idara zote,ccm iko nyang'anyang'a na vipande vipande kutokana na mchakato wa kura za maoni..siwezi ku risk roho yangu kwa ccm dhaifu hiyo huko arumeru
   
 12. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono hoja ili kuonyesha niko fair,chadema inaingia pale ikiwa moja,ccm vipande vipande...
   
 13. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  naona wanamtumia wakala wa vifo john tendwa.

  naomba kukuuliza kim balozi wetu huko katika serikali ya washiri hawezi kumtetea lema?kwa sababu naona sheria zao ni kama za kichina wanahukumu vifo kupitia msajili wa vyama.
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Unaleta habari za makanjanja.

  Hivi magwanda saa hizi mavi debe. Mkwewe akishindwa huko atakuwa hana maana kweli kweli.

  Hainiingii akilini hata kidogo kuwa Arumeru magwanda wanaweza kupata hata robo ya kura. Laibon? majonzi makubwa sana yanawangoja huko.

  Bora wajitoe tu, maana hilo pigo la huko litawamaliza kisaikolojia. Kama wana uongozi unafikiri haswa, basi watajitoa huko, tena wana sababu nzuri sana ya kujitoa. Wanaweza kusema tu, kwa heshima ya marehemu na mambo aliyotarajia kuyafanya na imebaki miaka mitatu tu, tumeona bora tujitoe na tumpe fursa mwanae ya kumalizia kazi za marehem baba yake. Hapo watatoka kiume na bila maumivu ya baadae.
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Uzini ilikuwa 5% magwanda 95% CCM, Arumeru na Lowassa ni kama Uzini na Razza.

  Hayo mapande ya CCM unayoyafikiria yatakupigia wewe kura, ujuwe unajipa moyo tu lakini matokeo umesha yajuwa. Huna chako.
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Angalau sasa, kuliko wakati mwingine wowote, kujiamini kwa CCM kwenye chaguzi hizi ndogo kumepungua sana au hakupo kabisa kwa sababu ya ushindani mzuri inaotoa CHADEMA pamoja rafu nyingi za CCM zinazochagizwa pia na wateule wa JMK akina Tendwa na vyombo vya DOLA. Safari bado ni ndefu lakini matumaini yapo na kila penye nia, njia ipo kwani NCHI hii ni yetu sote na UONGOZI wa nchi unapaswa kuwa wetu pia.
   
 17. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #17
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Bila shaka Mwigulu ana ukaribu na mkeo
   
 18. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Yani sasa mnamlaumu kila mtu kwa mafanikio hafifu kwenye chaguzi?Tendwa kwa mfano umemtaja unaweza kumhusisha vipi na uchache wa kura zenu kwenye chaguzi mbalimbali ukiwamo ule wa igunga ambao mlijitapa sana kwamba mtashinda?Tendwa alisababisha dipi kushindwa kwenu pale?na halafu mtaishi kwa hizi "angalau" mpaka lini hasa?
   
 19. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #19
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mzee angle hiyo usiende kabisa maana inawagusa zaidi watu wakubwa sana huko chadema kuhusu wake za watu(wakiwemo wanachama wao),wakubwa hao siku marafiki zangu sasa nawastahi sipendi kuwaumbua kwa u.j.i.n.g.a wa mashabiki tu wachache wa chadema wa aina yako,ngoja nikuache ili kulinda urafiki wetu.

  Kitu kingine mpaka sasa hujui jinsia yangu naweza nisiwe na mke bali mume,who knows zaidi yangu mwenyewe.
   
 20. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #20
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Hoja za ajabu sana hizi. Hoja za wanafunzi wa kidato cha pili wa zile shule zetu za seminari za kiarabu. Lowassa alishindwaje kumpigania hawara yake A-town ambako alikuwa anajisifu kuwa ana nguvu mithili ya Yesu?
  Arusha sio Lindi we dada
   
Loading...