CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike

Uzi mzito ,ushauri makini hakika kwa hili Paskali nakupongeza lakini pia naomba msifurahie kufa kwa upinzani hakika nawasii msifurahi kufa upinzani. Upinzani ukifa hata Ccm itagawanyika .
 
Uf
OK. Tuanzie hapo sasa.

Lowassa na kundi lake ni mafisadi ndio.

Lakini juzi mmezindua mahakama za mafisadi, kwanini msikamate na kuwapeleka huko ili wafungwe badala take mnakesha mitandaoni kuimba hili pambio?

Je, huko ccm akina ngeleja, Change, Kinana ni wasafi kiasi gani hadi mnamuona EL pekee?
Ufisadi wa Lowasa ulitajwa na CDM haikuwa CCM waliomtaja kama fisadi. Ndiyo anaweza kuwa ni fisadi ama la, lakini waliolianzisha ni CDM wenyewe.
 
Ilani au manifesto ni mwongozo wa wapi chama kinaelekea yaani kwa mfano dira ya maendeleo ya CCM ni ya 2010-2020 halafu kuna 2015-2025.

Hivyo CCM katika dira yake imekusudia kupambana na mambo manne:

1. Kuondoa Umaskini
2. Kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana.
3. Kuondoa tatizo la Rushwa na ubadhilifu wa mali ya umma.
4. Kudumisha Amani na ulinzi pamoja na usalama wa wananchi na mali zao.

Hivyo ni dira na inatekelezwa.

Kwa mfano Ilani kuu ya uchaguzi 2005 na 2010 ilikuwa ni Kasi mpya, Ari Mpya na Nguvu Mpya iliishia wapi? Maisha bora kwa kila mtanzania tunafahamu kilichototokea.

Sera ni mipango ya Serikali inayoundwa chini ya CCM kama dola ambapo ndiyo inaona sera ya viwanda, miundombinu kama barabara zinajengwa, Uchumi, sera za madini na nishati, sera ya elimu na sera ya kilimo na uzalishaji.

Itikadi yaweza kubadilika kulingana na mtazamo wa kiongozi aliepo madarakani maana hata huko Uchina raisi Xi anafanya mabadiliko kulingana na mahitaji yake na chama.

Hivyo kwa kuwa taifa letu bado linapiga hatua za maendeleo, basi itakadi yaweza kubakia kuwa ya ujamaa na kujitegemea kulingana na utelekezaji wa sera kama ya elimu bure ambapo serikali inalipia gharama za elimu ili kumkomboa mtoto asome na afahamu kusoma na kuandika.

China bado inacheza na itikadi hiyo huku ikikaribisha mabepari lakini ambao wapo tayari kufuata masharti ya China.
Utapeli huu
 
-Mwenyekiti Taifa-Freema Mbowe ni Mchaga na Mkristo
-Makamu Menyekiti ni Bara-Prof Safari Mwislam
-Makamu Mwenyekiti Zanzibar ni Mohammed, Mwislam na Mzanzibar
-Katibu Mkuu ni Vicent Mashinji-Msukuma, Mwanza na Mkristo
-Naibu wa Katibu Bara John Mnyika, Mkristo
-Naibu Katibu Visiwani ni Salum Mwalim, Mwislam na Mzanzibar
Kwa mifano hiyo michache pima mwenyewe huo udini na ukanda upo wapi. Mjomba hizo propaganda waliziweka CCM zimepitwa wakati.
Hao ndo wale wazee wa kukariri na kukurupuka! Tangu waaminishwe hivyo basi that shit got stuck in their dumb heads, wakilala wakiamka ni hilo tu! This ignorance sickens!
 
Tatizo kubwa ni kuwafunga mdomo CHADEMA kuzungumzia na kukemea ufisadi. Sasa CCM inajifanya ndiyo inayopambana na ufisadi kutokana na CHADEMA kuzibwa mdomo.
Kwa nini Chadema wamekubali kuzibwa midomo kizembe na kirahisi namna hii?
Hapo ndo shida ilipo.
Yaani kama chama kimeshindwa jambo rahisi hili, yaani hata hawajajaribu kupambana nalo na kuliondoa unategemeaje kichukue dola? Au kipambane na kitu dhalimu, au kuletea watu maendeleo?
 
Pascal Mayalla kaka yangu ushauri wako ni mzuri mno, mi naona wa kumshauri si mbowe maana anaona hana cha kupoteza amesha gain sana kupitia CHADEMA hasa malori chakavu na kukidai chama, hapa cha kufanya ni hawa vijana wapya wanaoibuka ndo wakuuzingatia ushauri huu,

nilichogundua ndani ya chadema ukiwa na maoni tofauti na mwenyekiti we ni msaliti, alafu ubovu wanachama wake amewafanya kama misukule wanafuata anachotaka yeye,

NAAMINI CHAMA CHA SIASA CHA UPINZANI MAKINI KINAKUJA MIAKA KAMA 30 IJAYO YAAN BAADA YA CCM KUONGOZA MIHONGO MINGINE MITATU NDO ITAPATAB MSHINDANI, SI KWAMBA ITATOKA MADARAKANI , HAPANA NAMAANISHA NDIPO ITAPATA MSHINDANI WA HOJA, SASA HIVI NI KUKURUPUKA NA WATU HAWAJUI WANASIMAMIA NINI
 
Wanabodi,

Declaration of Interest.
Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, hivyo ni kawaida, ukifanya ukosoaji wowote kuihusu Chadema humu jf, utanyooshewa vidole kuwa wewe ni CCM. Nafanya ukosoaji wangu constructively, truthfully with objectivity, impartiality and balancing, hivyo nawashauri Chadema, wawe tayari kupokea na kuuzingatia ushauri wowote, hata kama ushauri huo unatoka kwa kichaa au kwa shetani, ili kujitafakari na kujitathinini, kama inajidhania imesimama, na uiangalie isianguke. CHADEMA msipuuzie ushauri hata kama ni kutoka kwa shetani!, S ...

Utangulizi
Hili ni bandiko la ushauri wa bure kwa Chadema, na unatolewa na mtazamaji wa muda mrefu wa mchezo wa siasa nchini Tanzania, ambaye ameangalia tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Tanzania, uchaguzi wa jimbo la Kwahani, 1994, uchaguzi mkuu wa 1995, 2000, 2005, 2010, na 2015. Ushauri wenyewe ni kuhusu hii hama hama ya wanachama na viongozi wa Chadema kuhamia CCM. Naishauri Chadema Wajitafakari!, Wasiwabeze Wanaohama Kama Wafanyavyo CCM, Wanaohama Chadema, Wana Hoja za Msingi, Chadema Wanadhani Adui Yao Mkuu Anaowanya Kushindwa Kwenda Ikulu ni CCM, Kiukweli Adui Mkuu wa Chadema Sio CCM, Nitawatajia Adui Mkuu wa Chadema, na Mwisho Nitawapa Ushauri Chadema Wafanye Nini, Waweze Kuingia Ikulu 2025 Magufuli atakapomaliza and only if Magufuli atamaliza 2025!, kwa sababu haya ninayoshauri, kwa uchaguzi wa 2020, saa hizi tayari ni too little too late, na Magufuli ni just too powerful kiasi kwanza hakutakuwa na uchaguzi wa rais 2020, uchaguzi wa rais wa 2020 utakuwa ni igizo tuu la uchaguzi, lakini mshindi tayari ni Magufuli, hivyo wote watakaompinga Magufuli 2020, itakuwa ni kujifurahisha tuu, hivyo Chadema Watake Wasitake, Lazima Wabadilike, Vinginevyo...its the end of the road kwa Chadema, tunarudi kwenye nchi ya Chama Kimoja.

Why Chadema?
Tanzania japo tuna vyama vya siasa zaidi ya 22, lakini vyama vikubwa ni CCM, Chadema na CUF, by now CUF is already a gone case, hivyo tunapozungumzia upinzani Tanzania, tunazungumzia Chadema. Kifo cha CUF hichoo... chaja! Upinzani kubaki CHADEMA pekee ...

Justification ya Kuikosoa Chadema kwa Mtu Ambaye Sii Mwanachama.
Mashabiki na manazi wa Chadema humu jukwaani, ukifanya ukosoaji wa Chadema, au kutoa ushauri wowote kuhusu Chadema, watakubeza unashauri kama nani?. Kwa sababu Chadema ni public party paid by taxpayers money, then the taxpayers have the right to know the conduct of their tax, hivyo Watanzania wote wana right kujua mambo yote ya Chadema, public na private, ni haki yao kwa sababu kinaendeshwa kwa kodi zao!.

Kwanini Uishauri Chadema, Kwa Wao Wenyewe Hawajioni na Kujishauri?.
Ushauri huu nautoa kwa dhana kuwa Viongozi wa Chadema, wanachama wao, wafuasi wao, washabiki wao na manazi wa Chadema humu jf, wote ni pro Chadema, wako ndani ya box la Chadema, hivyo wanaweza wasiwe na uwezo wa kuona nje ya box, soso tulioko nje ya box ambao ni watazamaji, tunaweza kuwa tunaiona Chadema vizuri Zaidi kwa nje, kuliko waliomo ndani ya chama, lakini pia kuna walioko ndani, wanayaona madhaifu na mapungufu ya Chadema from within, lakini kwa vile wamo, wanakosa objectivity ya kujiambia, kujitathinini na kujikosoa, hata hivyo tathmini ya kweli, inapaswa ifanywe na watu wa nje na sio kujitathmini yenyewe.

Chadema Isiwabeze Wanaohama, Ni Haki Yao, Ila Pia Izingatie Hoja Zao, Wana Hoja za Msingi
Kati ya wanachama na viongozi wa Chadema wanaohamia CCM, kuna wengine wanahama kimya kimya bila kusema sababu, kuna wengine wananunuliwa, na kuna wengine na haswa baadhi ya viongozi, wanapohama, wanaandika barua Chadema na kuaga kwa kutoa sababu, ziwe ni sababu za kweli au ni visingizio tuu, lakini kuna kitu wanasema, na wengine hawasemi chochote kuhusu Chadema lakini siku wanapokelewa CCM, Chadema, japo ni kweli wengi kinachowahamisha Chadema ni njaa zao tuu, na wanakwenda CCM kufukuzia fursa, lakini kuna baadhi, wana hoja za msingi sana, hivyo Chadema inatakiwa kutozipuuza hoja zao, isisikilize na kujitathmini kuhusu ukweli wa hoja hizo.

A Way Forward, Chadema Ifanye Nini.

  1. Kwanza Chadema ijitathmini, is it on the right track?, itambue makosa yake, ikubali makosa, ijirekebishe, isonge mbele. CHADEMA ni sikio la kufa? Iambiwe vipi ili isikie? Masha ana hoja za msingi, zisikilizwe, zizingatiwe, zisipuuzwe!
  2. Ianzishe grassroots recruitment ya wanachama wake waaminifu, isije kujikuta imewakumbatia CCM ndani, Chadema nje hadi ndani ya CC yake, kama ilivyotokea kwa Mwenyekiti wa Bavicha.
  3. Ianzishe headhunting na spotting leadership talents na able people toka kwenye jamii kujiunga Chadema na kujenga kada ya viongozi wake wa kesho, born and breed in Chadema, kwa kuwafanyia grooming, ili kupata wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uongozi.
  4. Ipunguze kushobokea makapi kutoka CCM, wana CCM wanaojitoa CCM na kujinga Chadema, wawe wanachama wa kawaida tuu kama wanachadema wengine na sio kupapatikiwa na kupewa uongozi moja kwa moja.
  5. Chadema I invest on people na mass mobilization, na sio ku invest on vitu na mikutano tuu ya hadhara, kupitia social media na kumiliki media yake yenyewe, kutawafikia watu wengi Zaidi kuliko kutegemea mikutano na maandamano pekee.
  6. Chadema irudishe ukomo wa uongozi, hata kiongozi awe mzuri vipi, anafikia kiwango cha ukomo wake na kuwa kama saturated solution, he can do no more than what he can!, anakuwa hana jipya!, pia Chadema waandae succession plan, by now, wawe na a pool of able people from within kushika nafasi zote za uongozi, na kuendesha serikali, kungekuwa na ukomo, by now watu wangejua Mbowe amefikia ukomo wa uwezo wake, hivyo nani watampokea.
  7. CCM ni chama dola, hivyo Chadema isitumie model ya CCM kuitafuta ikulu, iandae model yake yenyewe ya kupata viongozi wake na wagombea wake, mtindo wa the democrats ya US ni mzuri kuanzia kwenye primaries.
  8. Kuondokana na viongozi ving'ang'anizi na miungu watu, maadamtarget ni kuingia ikulu, umeshindwa kuuingiza Chadema ikulu, unapisha wengine wanaendeleza, sio umeshindwa hala unang'ang'ania!.
  9. Kuwafanyia tathmini wabunge wake na kukubalika kwao, na kuwe hakuna haki miliki ya majimbo, mfano 2020, Mdee anatathminiwa amefanya nini Kawe for 10 years, na jee bado anakubalika?, Wanachadema wote wenye uwezo, wawe huru kumchallenge Mdee, akitokea mwanachama mwingine mwenye sifa Zaidi, uwezo Zaidi na kukubalika Zaidi, Mdee anawekwa pembeni, vinginevyo 2020, kuna majimbo kibao Chadema mtayarudisha CCM!.
  10. Chadema kionyeshe ukomavu na kuwa ni chama mbadala kwa kuachana na cheap politics ya siasa za matukio, na kujikita kwenye real politics ya kushindanisha sera, sio kwa kupinga kila kitu, CCM ikifanya mazuri, mfano elimu bure, Chadema ikubali hili ni zuri, lakini ionyeshe ingekuwa Chadema ingefanya bora zaidi kwa elimu bure hadi chuo kikuu, kwa kuonyesha how CCM inatapanya fedha kwa mambo yasiyo na maana, halafu inanyanyasa Watanzania masikini kwa kuwanyima mikopo. Chadema wajifunze kuibomoa CCM kwa hoja na sio siasa za matukio, mfano mwaka 2020, Magufuli anaingia ulingoni akiwa na elimu bure, ndege za ATCL zinapaa dunia nzima, flyovers, reli ya SGR, na Tanzania ya viwanda. Chadema lazima waje na sera mbadala kuonyesha jinsi ATCL, flyovers na SGR zilivyowatia umasikini Tanzania, kama fedha hizo zingewekezwa kwenye sekta ya kilimo nini kingepatikana, bila kuinua sekta ya kilimo, hiyo Tanzania ni Tanzania ya viwanda gani vinavyotumia malighafi gani?. Ijikite kwenye hoja kama hizi Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas ...
  11. Chadema ipiganie a level playing field kwenye the political ground, kupitia tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, haiwezekani watu wawili wanagombea urais, mgombea mmoja anakuja na vingora, na full government media team, paid by public money for the advantage ya CCM, halafu, mwingine with nothing, halafu utegemee kushinda!.
  12. Chadema ipiganie true free and fair elections with maximum transparency, kama hakuna manouvers zozote zinazofanywa na Tume ya Uchaguzi, kwa nini wazueie party tallying?, wanaogopa nini, kama matokeo yote hadi ya urais yanabandikwa vituoni mbele ya mawakala wa vyama, kuna kosa gabi kama mawakala wote watakuwa na smart phones, ku scan matokeo na kutuma makao makuu kwenye tallycenters za vyama, kama haki itatendeka, then tallying za vyama zitafana na tallying ya NEC, what is it there to hide kuzuia tallying?.
  13. Chadema kutimiza majukumu yake kikamilifu kama Chama cha upinzani kazi yake sio tuu kuikosoa serikali, bali ku I check serikali kuhakikisha inafuata katiba na kutekeleza sharia, taratibu na kanuni, mfano, katika kuzuia mikutano ya kisiasa, rais Magufuli amevunja katiba wazi wazi kabisa mchana kweupe!, chama chochote makini, by now, kingeifungua shauri mahakamani, ili mahakama itoe tafsiri rasmi, kama itathibitisha rais amevunja katiba, anashitakiwa na bunge, na kuondolewa madarakani!. Mfano hata suala dogo tuu kama Daudi Bashite, nilishauri Je, wajua suala vyeti vya Bashite, linaweza kabisa kumng'oa Rais ...
  14. Chadema waipinge CCM kwa kujikita kwenye hoja zenye maslahi kwa taifa, ujinga, umasikini, maradhi, rushwa na ufisadi, kwa kuonyeshea CCM katika kipindi chote cha miaka 50, CCM imeshindwa, na katika rushwa na ufisadi, Chadema iwaeleze wananchi, CCM ndio shina na mlezi wa rushwa zote na mafisadi karibu wote ni CCM!, ili wananchi waelewe kuwa CCM inapigana vita ilivyovilea na kuvijenga.
Ni hayo kwa uchache, nikikumbuka mengine nitayaongeza.

Paskali
Umetoa mapendekezo, lakini hujasema tatizo la Chadema ni nini? I wish ukaja ukaenda straight to the point nakusema matatizo ya Chadema ni 1,2,3....
Ubaya wa kutoa mapendekezo kabla ya kuainisha matatizo kinaga ubaga, ni kuwa haya mapendekezo yanaweza kuwa ni ya kufikirika ya tatizo ambalo halipo, haya mapendekezo yanaweza kuwa ni mwanzo na yanahitaji maboresho zaidi ili yaweze kutatua tatizo. mapendekezo yako yanaweza yakawa mazuri on paper, Lakini watu watajiuliza je anataka kutatua , ku improve au kubomoa.
Nimejaribu kusikiliza watu mbali Lakini hakuna anayekwenda straight to the point matatizo ni nini. They all sound like wasaka tonge, i.e. Chadema hawana nia ya kuchukua nchi, ninapendezwa na utendaji wa magufuli etc. Mwisho wa siku nakupongeza kwa andiko hopefully utaliboresha zaidi.
 
Umetoa mapendekezo, lakini hujasema tatizo la Chadema ni nini? I wish ukaja ukaenda straight to the point nakusema matatizo ya Chadema ni 1,2,3....
Nimejaribu kusikiliza watu mbali Lakini hakuna anayekwenda straight to the point matatizo ni nini. They all sound like wasaka tonge, i.e. Chadema hawana nia ya kuchukua nchi, ninapendezwa na utendaji wa magufuli etc. Mwisho wa siku nakupongeza kwa andiko hopefully utaliboresha zaidi.
Mkuu Semilong, kama umenote mabandiko yangu mengi, naandika kwa ajili ya watu wa aina tatu,
  1. Kufuatia Watanzania wengi kuwa ni wavivu wa kusoma hoja ndefu, mabandiko yangu huwa nayakata na kutoa a short version ili wavivu wa kusoma, wasome mwanzo tuu na mwisho.
  2. Kwa ajili ya wale wanaopenda kwenda deep, pale katikati kuna maneno haya
    Chadema Ina Matatizo From Top to Bottom, Left, Right and Center. Click to expand...
    ukiclick hapo ita expand, nimeyaweka matatizo lukuki ya Chadema.
  3. Pia huwa ninaandika kwa ajili ya Great Thinkers ambao ni wale tuu wenye uwezo wa to read in between the lines na kubaini the motive behind bandiko husika. Wewe ukiwa sio GT, pia utapata kitu, kama ni mpanda kusoma utasoma kitu na ma GT pia wanapata vitu kwa uelewa tofauti na watu wa kawaida.
Natumaini nimeeleweka.

Paskali
 
Sio siri tena; Kuna tatizo kubwa sana ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Hakuna haja ya kuendelea kulificha Bali kulikabili na kulitatua.

Haiwezekani wanachama kila uchwao wakawa wanaondoka tu bila kuwepo sababu za msingi??

Hata kama sababu zinaweza kuwa dhaifu kwa wengine lakini uwepo wa sababu zinazobebana unathibitisha kuwepo kwa tatizo.

Kuna tatizo kubwa sana CHADEMA..
 
Sababu ni njaa, wanaohama wana njaa ya pesa. Kuna wanaotishwa wakatishika kupoteza mali zao, wanahamia ccm kulinda maslahi.
 
Sio siri tena; Kuna tatizo kubwa sana ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Hakuna haja ya kuendelea kulificha Bali kulikabili na kulitatua.

Haiwezekani wanachama kila uchwao wakawa wanaondoka tu bila kuwepo sababu za msingi??

Hata kama sababu zinaweza kuwa dhaifu kwa wengine lakini uwepo wa sababu zinazobebana unathibitisha kuwepo kwa tatizo.

Kuna tatizo kubwa sana Chadema..
Mkuu unayeamini kuna tatizo CHADEMA fuatilia hao wanaohama wametoka wapi, ni watu wa CCM wamezoea mteremko ambao CHADEMA haupo. Hiki ni chama cha ukombozi kina hatari kibao ikiwemo kubambikiwa kesi, kukosa pesa, kutumia pesa binafsi kwa maslahi ya chama, kufungiwa biashara, kubomolewa nyumba, kufungwa kwa uchochezi, kuteswa na polisi, kukatwa mapanga na CCM, kupigwa risasi na usalama wa taifa nk! Wale wanaoona wamefuata mpunga CHADEMA wasepe watuachie chama chetu.
 
Back
Top Bottom