CHADEMA, mchungeni Mwenyekiti Mbowe

CHADEMA, mchungeni Mwenyekiti Mbowe

Benson Mramba

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2013
Posts
766
Reaction score
1,884
Wahenga walisema “Mtu Mzima akilia ujue kuna Jambo”

Katika siku za hivi karibuni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA akiwa jimboni kwake Hai amesikika akilalama au kujinasibu kuwa asingekuwa na roho ngumu angekuwa ameshaachana na upinzani. Nukuu iliyotolewa kwenye mitandao ya kijamii hususani kanda ya Kaskazini ilisomeka ifuatavyo “ Upinzani ni wito, wenye roho nyepesi hawawezi, kama ningekuwa napenda Fedha, nina roho nyepesi, ningeshachukua hizo pesa na ningeshakimbia kabisa upinzani” Habari hii pia iliandikwa kwenye gazeti la Mwananchi.

Habari hii haikuwa mpya kwangu kwani inaonekana Mh Mbowe amekuwa akiirudia sehemu mbalimbali anapokutana na viongozi wa Chama kwa malengo ya kuwajengea imani juu yake hususan kwenye swala zima la tamaa ya fedha. Maslani akiwa mkoani Tanga wakati wa Uchaguzi aliouvunja kwasababu zake binafsi wa Kanda ya Kaskazini Mh Mbowe inasemekana aliwaambia baadhi ya viongozi kuwa ameshawishiwa apewe Bilioni 70 ili aivuruge CHADEMA (Niliambiwa na kiongozi mmoja ambaye ni rafiki yangu mimi ninayemuamini) Baada ya kusikia habari hii ilinishtua sana na kuogopa kuwa huenda Fisi anajaribiwa kwa Mfupa.

Aidha Dr Mashinji Katibu Mkuu wa CHADEMA alitoa taarifa kwa Umma siku za karibuni pia kuwa kuna Wabunge wa CHADEMA wanataka kuhongwa ili wajiuzulu ubunge. Hakutuambia kama Mwenyekiti wake nae ni miongoni mwao au la.

Maoni yangu kwa mfululilizo huu ni kuwa Wanachama na viongozi wa CHADEMA wanapaswa kuwa macho sana na Mwenyekiti wao katika wakati huu kuliko wakati mwingine wowote kwasababu zifuatazo:-

1. Mbowe ametikiswa au kutikisika kiuchumi katika awamu hii kuliko ambavyo imewahi kumtokea wakati mwingine wowote. Billcanas imefungwa, gazeti halifanyi vizuri sana, Madeni ya malimbikizo ya kodi na shamba la mboga nalo limeharibiwa.

2. Awamu ya nne siasa ilikuwa ni mradi na fursa kwa viongozi wengi na makada wa vyama hususan vya upinzani. Lipo andiko la Mh Zito liliwahi kuonekana mtandaoni kuonyesha kuwa kuna wana CCM wa wakati huo waliokuwa wakiwapa fedha viongozi wakuu wa upinzani kwa maslahi yao. Mbowe amekuwa Mbunge katika awamu yote ya nne na biashara zake zikiendelea vizuri pia taasis kama TAKUKURU na TRA hazikuwa moto kama wakati huu. Ukaguzi kwenye vyama nao ulikuwa mdogo tofauti na ninavyotarajia kwa wakati huu.

3. Mbowe hajawahi kupata shida akiwa yoyote ya kiuchumi au msukosuko wa jela au mahabusu akiwa CHADEMA. Kuna wahenga wa Chama waliniambia miaka ya 2004 Mbowe alipata mtikisiko wa ndani ya Chama wakati huo akiwa amepoteza Ubunge wake huko Hai kwa hasira akatishia kuhamia CCM miaka hiyo. (Maneno ya Wahenga hayo sio yangu) Hii inamaanisha kuwa maslahi yake ndani ya upinzani yakidhibitiwa basi anaweza kufanya lolote kuyanusuru.

4. Ujio wa Mawaziri Wakuu wawili wastaafu nao ni Changamoto kwa Chama. Mawaziri hawa wanahesabika kama wasaliti ndani ya CCM na dola pia. Nakumbuka nguvu kubwa iliyotumiwa na CHADEMA kupambana na Zitto Kabwe kwa hoja au dhana kuwa Zitto ni Msaliti. Naamini kanuni ni hiyo hiyo hata CCM pia. So by Compromising or by Force Mbowe lazima atikiswe.

5. Dr Slaa wakati akijitoa kwenye Ukatibu Mkuu alidai kuwa alitaka kuhongwa Bilioni 5 ili ampokee Lowassa akakataa. Dr Slaa akadai anashangaa Mwenyekiti wake alivyokubali kumpokea Lowassa wakati alimjulisha juu ya swala la yeye kutaka kupewa fedha.

6. Dili ya Bilioni saba (7) ndani ya Chama nayo nimeitia mchanga naamini TAKUKURU watakuwa wanaifuatilia kwa karibu.

Kwa hoja hizo mimi binafsi simuamini Mbowe kabisa linapokuja swala la fedha. Na kwa yowe hili analolipiga sasa inaonyesha kabanwa mahali. Wito wangu wanachama na viongozi mchungeni Mwenyekiti wenu asije kutusaliti tena watanzania. Ukiona mtu mzima Analia ujue kuna jambo

.
 
Hebu tuondolee upuuzi wako. Shamba limeharibiwa ... umesikia maamuzi ya mahakama? Acha roho mbaya. Unafaidika nini mwenzio akiyumba kiuchumi kwa sababu ya chuki za kisiasa za watu kama wewe?

Umeachana na Chadema fanya yako acha kunusanusa kama simbilisi. Ok ya Mbowe hayakuhusu songa.......Next
 
Wewe usimuamini,wengine tuna imani naye!Tumevuka naye katika mengi na katuvusha salama,huu upupu wa leo hatuwezi kuutilia maanani!

Lipumba aliweza kununuliwa na kuiuza CUF, jambo hilo limeshindikana kwa CDM miaka nenda rudi!
Mbowe kaza buti, mpaka vibaraka wote waweweseke!
 
Mie ni Mwana CCM kindaki ndaki tangu ianzishwe 1977 na Kama kinavyonitaka kusema Ukweli Basi uhai wa Chadema kwa sasa unategemea uwepo binafsi wa Mh. Freeman Mbowe
Akiondoka Mbowe kwa sasa makambale ni wengi sana pale ukianzia kwa kina Lissu, Mnyika, Msigwa. N.k kila mmoja anajiona Much know na Dkt Mashinji wanamchukulia Kama Mgambo wa Jiji haheshimiwi kama Dkt Slaa
 
Hivi si ndio wewe siku chache zi'izopita ulileta uzi hapa kama umeamua kuwa mwanachama mfu?
Basi hayo mambo ya chadema waachie wanachama hai mkuu....
hutopungukiwa chochote!!
Kweli kabisa,ni huyu alisema ameamua kuwa mwanachama mfu! Sasa sijui anakereketwa na nini!
 
Kama Mbowe ana shida ya hela watu wanaoipenda chadema wako tayari kumchangia. Ccm kweli im3mbana.

Watu wengine ni wabaya Slaa yeye alihongwa ngapi hata akatoka?
Mbowe hapokei mshahara chadema.

Alihitaji fedha kwa ajili ya kampeni za election 2015. Au unafikiri chadema ni chama tawala inayoweza kubana wafanyi biashara ama serikali kuwalipia? Acha uwongo wako wewe msaliti Benson.

Ni ukeli mtupu kuwa kiongozi wa chadema inahitaji moyo siyo pesa.
Kwani unadhani vita yota hatuioni?
 
Mbowe haaminiki ni mhenga wa kupiga panga hata kumchunga huwezi ile ni Saccos yake.

Wote walipo ofisini kwake ni wajuba wake hakuna anayeweza kumuuliza lolote mbowe iwe katibu mkuu wakurugenzi, kamati kuu, hawana huo uwezo hawawezi kuthubutu. Sio fedha wala maamuzi, akishawapeleka hotelini kula kamaliza.

Sasa hivi wanamlipa kwa instalment bilion saba anadai alitumia kwa uchaguzi hata mkurugenzi wa fedha hajawahi kuziona lakini wanamlipa hakuna anayehoji.
 
Back
Top Bottom