CHADEMA: Mchakato wa kuwania Ubunge Arumeru Mashariki umeanza rasmi

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,071

TAARIFA KWA UMMA

RATIBA YA CHADEMA YA UCHUKUAJI FOMU NA UTEUZI WA MGOMBEA WA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI

Baada ya kupokea taarifa za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), juu ya kuwepo kwa uchaguzi katika Jimbo la Arumeru Mashariki, Sekretarieti ya CHADEMA tayari imekaa na kuandaa utaratibu mzima wa uchukuaji na urudishaji wa fomu, ambao utafuatiwa na vikao vya chama, kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa, kwa maana ya Kamati Kuu, katika kufanya uteuzi wa mwisho wa kumpata mgombea.

Ili kutoa muda wa kutosha kwa shughuli ya utoaji na urejeshaji fomu, Sekretarieti ya CHADEMA imeamua kuwa wanachama wa CHADEMA wenye nia ya kuwania uteuzi wa kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, kwa ajili ya kuwatumikia watu wa Arumeru Mashariki, wataanza kuchukua na kurudisha fomu kuanzia leo tarehe 14 Februari 2012 hadi tarehe 25 Februari 2012 saa 10 Jioni.

Fomu zinatolewa kupitia ofisi ya CHADEMA ya Wilaya ya Meru zilizopo eneo la Maji ya Chai-USA River, na pia katika ofisi za CHADEMA za Mkoa wa Arusha zilizopo Ngarenaro katika Mtaa wa NHC.

Baada ya hapo, vikao vya chama vinavyohusika na uteuzi wanachama watakaokuwa wamechukua fomu na kutimiza masharti kadri inavyoelekezwa, vitakaa kufanya uteuzi na hatimaye kumpata mgombea mmoja, ambaye chama kitamsimamisha na kumsimamia kuwania jimbo hilo, ili ashinde na kuongeza nguvu ya wapambanaji ndani ya wabunge, kuwawakilisha Watanzania.

Mchakato wa uteuzi ngazi ya jimbo na wilaya utafanyika kati ya tarehe 26 Februari 2012 mpaka tarehe 29 Februari 2012 wakati uteuzi ngazi ya taifa utafanyika tarehe 3 Machi mpaka 4 Machi 2012.

Kupitia kwa Kurugenzi ya Habari na Uenezi, CHADEMA ikiwa ni chama mbadala katika kuunda serikali na chama kikuu cha upinzani nchini, kinawahakikishia wanachama, wapenzi wake na Watanzania wote kwa ujumla, kuwa kama ilivyo kawaida yake, kitashiriki katika uchaguzi huo mdogo wa Arumeru Mashariki, kwa lengo la kushinda.

Kwa umakini na uimara ambao kimeendelea kuudhihirisha katika kuwatumikia na kuwawakilisha Watanzania kupitia majukwaa mbalimbali, tangu Watanzania walipoonesha dalili zote za kukiunga mkono na kukiamini kuwa kinaweza kupewa dhamana ya uongozi wa nchi hii, ari ya chama hiki imezidi kuongezeka siku hadi siku, kikijiandaa kupokea dhamana kubwa zaidi kadri siku zinavyokwenda.

Hivyo katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki Wanachama na wananchi kwa ujumla wazingatie kwamba CHADEMA itaendelea kutimiza dhima yake ya kuhakikisha uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni dhabiti kwa maendeleo endelevu ya Tanzania.

Imetolewa leo tarehe 14 Februari 2012, Dar es Salaam na;

John Mnyika

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
 
Noted Mkuu. All the best.

Sawa sawa kamanda. Sasa tunaelekea Arumeru Mashariki. Utartibu ndiyo huo, wenye sifa zinazofaa kutumika kwa maendeleo ya watu, kupitia chama mbadala, chama makini, CHADEMA, wajipime kisha waingine ulingoni.
 
Kila la kheri mkuu.Ushindi ni lazima.Kumbuka Arusha ni ngome kuu ya CDM
 
Noted Mkuu. All the best.

Sawa sawa kamanda. Sasa tunaelekea Arumeru Mashariki. Utartibu ndiyo huo, wenye sifa zinazofaa kutumika kwa maendeleo ya watu, kupitia chama mbadala, chama makini, CHADEMA, wajipime kisha waingine ulingoni.
 
Tupo pamoja makamanda katika ukombozi wa mtanzania,katika kudai haki na utu wa mtanzania unaogandamizwa na serikali legelege na dhaifu ya CCM.
 
Kuna thread moja nimechangia asubuhi nikasema CDM isijiamini sana kwasababu wapiga kura wengi vijana toka ktk shule za sekondari,vyuo na wafanyabiashara sidhani kama wamejiandikisha kama wapiga kura ktk jimbo la Arumeru mashariki. Licha ya NEC kupata mwenyekiti na mkurugenzi mpya,mpaka sasa imekaa kimya kuhusu uboreshaji wa daftari la wapiga kura!
 
TAARIFA KWA UMMA

RATIBA YA CHADEMA YA UCHUKUAJI FOMU NA UTEUZI WA MGOMBEA WA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI

Baada ya kupokea taarifa za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), juu ya kuwepo kwa uchaguzi katika Jimbo la Arumeru Mashariki, Sekretarieti ya CHADEMA tayari imekaa na kuandaa utaratibu mzima wa uchukuaji na urudishaji wa fomu, ambao utafuatiwa na vikao vya chama, kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa, kwa maana ya Kamati Kuu, katika kufanya uteuzi wa mwisho wa kumpata mgombea.

Ili kutoa muda wa kutosha kwa shughuli ya utoaji na urejeshaji fomu, Sekretarieti ya CHADEMA imeamua kuwa wanachama wa CHADEMA wenye nia ya kuwania uteuzi wa kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, kwa ajili ya kuwatumikia watu wa Arumeru Mashariki, wataanza kuchukua na kurudisha fomu kuanzia leo tarehe 14 Februari 2012 hadi tarehe 25 Februari 2012 saa 10 Jioni.

Fomu zinatolewa kupitia ofisi ya CHADEMA ya Wilaya ya Meru zilizopo eneo la Maji ya Chai-USA River, na pia katika ofisi za CHADEMA za Mkoa wa Arusha zilizopo Ngarenaro katika Mtaa wa NHC.

Baada ya hapo, vikao vya chama vinavyohusika na uteuzi wanachama watakaokuwa wamechukua fomu na kutimiza masharti kadri inavyoelekezwa, vitakaa kufanya uteuzi na hatimaye kumpata mgombea mmoja, ambaye chama kitamsimamisha na kumsimamia kuwania jimbo hilo, ili ashinde na kuongeza nguvu ya wapambanaji ndani ya wabunge, kuwawakilisha Watanzania.

Mchakato wa uteuzi ngazi ya jimbo na wilaya utafanyika kati ya tarehe 26 Februari 2012 mpaka tarehe 29 Februari 2012 wakati uteuzi ngazi ya taifa utafanyika tarehe 3 Machi mpaka 4 Machi 2012.

Kupitia kwa Kurugenzi ya Habari na Uenezi, CHADEMA ikiwa ni chama mbadala katika kuunda serikali na chama kikuu cha upinzani nchini, kinawahakikishia wanachama, wapenzi wake na Watanzania wote kwa ujumla, kuwa kama ilivyo kawaida yake, kitashiriki katika uchaguzi huo mdogo wa Arumeru Mashariki, kwa lengo la kushinda.

Kwa umakini na uimara ambao kimeendelea kuudhihirisha katika kuwatumikia na kuwawakilisha Watanzania kupitia majukwaa mbalimbali, tangu Watanzania walipoonesha dalili zote za kukiunga mkono na kukiamini kuwa kinaweza kupewa dhamana ya uongozi wa nchi hii, ari ya chama hiki imezidi kuongezeka siku hadi siku, kikijiandaa kupokea dhamana kubwa zaidi kadri siku zinavyokwenda.

Hivyo katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki Wanachama na wananchi kwa ujumla wazingatie kwamba CHADEMA itaendelea kutimiza dhima yake ya kuhakikisha uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni dhabiti kwa maendeleo endelevu ya Tanzania.

Imetolewa leo tarehe 14 Februari 2012, Dar es Salaam na;

John Mnyika

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

ningependa kuchukua fursa hii kumuomba joshua nasari kuchukua fomu na kugombea ili kupata nafasi ya kuiwakilisha chadema ktk kinyanganyiro hiki.
 
Aisee hawa watu wanafikra zinazofanana kiasi hiki, neno kwa neno!!:lol::poa
Sawa sawa kamanda. Sasa tunaelekea Arumeru Mashariki. Utartibu ndiyo huo, wenye sifa zinazofaa kutumika kwa maendeleo ya watu, kupitia chama mbadala, chama makini, CHADEMA, wajipime kisha waingine ulingoni.

Sawa sawa kamanda. Sasa tunaelekea Arumeru Mashariki. Utartibu ndiyo huo, wenye sifa zinazofaa kutumika kwa maendeleo ya watu, kupitia chama mbadala, chama makini, CHADEMA, wajipime kisha waingine ulingoni.
 
Tujipange vizuri, jimbo tutalichukua. Wenye sifa wajitikeze.

Kama Chadema watajipanga vizuri zaidi kuanzia uongozi wa jimbo, mkoa hadi taifa, basi hakuna wasiwasi wa kulinyakua jimbo hilo.

This time around around, sidhani kama kutakuwa na excuses!!
 
Mussa Juma, Arumeru.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza ratiba yake ya kushiriki uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Arusha huku wanachama wake wanne wakiwa tayari wamejitokeza kuomba kuteuliwa.

"Chama cha Chadema kinawahakikishia … kitashiriki katika uchaguzi huo mdogo wa Arumeru Mashariki, kwa lengo la kushinda,” alisema Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika katika taarifa yake jana.

Alisema fomu zilianza kutolewa tangu jana na kwamba mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Februari 25.
Mnyika alisema fomu zinatolewa katika Ofisi ya Chadema ya Wilaya ya Arumeru, Maji ya Chai-USA River na pia katika Ofisi za Chadema za Mkoa wa Arusha.

“Baada ya hapo vikao vya chama vinavyohusika na uteuzi vitafanyika ili kumpata mgombea mmoja,” alisema.
Uchaguzi huo unafanyika baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo hilo, Jeremia Sumari.
Mnyika alisema anaamini umakini na uimara ambao kimeendelea kuudhihirisha katika kuwatumikia na kuwawakilisha Watanzania, kitashinda.

Mchakato wa uteuzi ngazi ya jimbo na wilaya utafanyika kati ya Februari 26 na 29, mwaka huu wakati uteuzi ngazi ya taifa utafanyika Machi 3 Machi mpaka 4.

Waliochukua fomu
Wanachama wa Chadema waliojitokeza kutaka kupeperusha bendera ya chama hicho ni Joshua Nasari, Samweli Shami, Francis Tembo na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Wilaya ya Arumeru (Bawacha), Anna Mwagirwa.

Kujitokeza kwa wanachama hao wanne wa Chadema, kunafanya idadi ya waliojitokeza kuwania kiti hicho kufikia sita. Juzi, wanachama wawili wa CCM walichukua fomu kupitia chama hicho.

Waliojitokeza ni pamoja na mtoto wa Sumari, , Sioi na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, William Ndeoya Sarakikya.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema Mkoa wa Arusha, Ephata Nanyaro alisema wanachama hao wanatarajiwa kuanza kupewa fomu za kugombea leo.

Alisema utaratibu wa kura kumpata mgombea wa chama hicho, unatarajiwa kutangazwa mara baada ya kukamilisha kikao cha sekretarieti ya Chadema, Dar es Salaam.

Sarakikya akana

Katika hatua nyingine, William Sarakikya aliyechukua fomu juzi kugombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, amesema kwamba si mtoto wa Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali, Mirisho Sarakikya.

Akizungumza jana mjini Arusha, Sarakikya alisema kwamba wote ni wa ukoo mmoja lakini hajazaliwa na Mkuu huyo wa majeshi wa zamani.

Wakati William akikanusha, Jenerali Sarakikya naye alisema jana kwamba mgombea huyo anatokea katika ukoo wake, lakini siyo mtoto wake wa kumzaa.

“Kimsingi ukoo wote wa Sarakikya ni ndugu lakini William siyo mtoto wangu wa kumzaa, ni mtoto wa jamaa yangu. Mimi nina watoto wanne ambao hawako kabisa kwenye siasa,” alisema Mstaafu huyo wa jeshi na kutaja kazi za wanaye hao kuwa ni udaktari, uhandisi ualimu na taaluma ya benki.
 
HAPA NI NYUMBANI NJOONI TU. NYUMBA ILIKUWA IMEVAMIWA NA SIAFU TU(ccm) WAMESHATOKA. NAOMBA NIWE MTU WA KWANZA KUTANGAZA HALI YA HATARI KAMA YALE TULIFANYIWA IGUNGA YATAJIRUDIA HAKIKA TUTACHAPANA SANA. UKOMBOZI WETU UNAANZA RASMI ARUSHA TUMECHOKA NA MAKUCHA DHALIMU YA CCM
 
Back
Top Bottom