Chadema: Mazungumzo na jk bado hayajaisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema: Mazungumzo na jk bado hayajaisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Jan 25, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kitaendelea kuwasiliana na Rais Jakaya Kikwete na serikali kufanya mashauriano ili kuhakikisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 inafanyiwa marekebisho ya msingi kabla ya mchakato wa kukusanya maoni kwa mujibu wa sheria hiyo haujaanza.
  Uamuzi huo ni kati ya maamuzi yaliyofikiwa na Kamati Kuu (CC) ya Chadema, katika mkutano wake, uliofanyika kwa siku mbili, kuanzia Januari 20, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

  Mkutano huo wa CC ulikuwa na ajenda mbalimbali, ikiwamo uteuzi wa mgombea wa uwakilishi wa Jimbo la Uzini, kisiwani Unguja.

  Ajenda nyingine, kupitisha mkakati na bajeti ya uchaguzi husika; taarifa ya kamati maalum ya CC kuhusu sheria hiyo na taarifa ya fedha (mapato na matumizi ya chama) kwa mwaka 2011.

  Mawasiliano mashauariano hayo na Rais Kikwete na serikali, yamekuwa yakifanywa na kamati maalum iliyoundwa na CC Novemba 20, mwaka jana.

  Kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

  “Kamati Kuu imeamua kwamba Kamati Maalum iendelee kufanya mawasiliano na mashauriano na Rais Kikwete na serikali kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 inafanyiwa marekebisho ya msingi kabla ya mchakato wa kukusanya maoni kwa mujibu wa sheria husika haujaanza,” ilieleza sehemu ya taarifa ya Chadema jana.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, katika mkutano huo, CC ilipokea na kujadili taarifa ya kamati maalum kuhusu sheria hiyo.

  Pia ilieleza kuwa CC ilijulishwa hatua, ambazo serikali imefikia katika maandalizi ya kuifanyia marekebisho sheria hiyo katika Mkutano wa Sita wa Bunge unaotarajia kuanza Januari 31, mwaka huu.

  Ilieleza kuwa CC imeendelea kusisitiza azimio lake la kikao cha Novemba 20, mwaka jana linalotamka kuhusu ushiriki wa Chadema katika mchakato wote wa kupata Katiba Mpya uliowekwa na sheria hiyo.

  Kwamba, utategemea utayari wa serikali ya Rais Kikwete kufanya mabadiliko ya kimsingi katika sheria hiyo kwa lengo la kujenga muafaka wa kitaifa juu ya mchakato huo.

  Kadhalika CC imepokea taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa na chama katika kufanya mikutano ya ndani katika maeneo mbalimbali kulenga kuelimisha viongozi, wanachama na wananchi kuhusu upungufu wa sheria hiyo pamoja na kupokea maoni kwa ajili ya kuboresha sheria husika.

  Vilevile, CC imeamua kwamba, Chadema iendelee kutekeleza azimio la kikao cha CC cha Novemba 20, mwaka jana la kutoa elimu kwa wananchi na wadau wote juu ya ubovu wa sheria hiyo na juu ya haja ya kuwa na sheria itakayoweka utaratibu bora zaidi wa kuunda Tume Shirikishi ya Katiba kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi.

  Pia kuandaa ripoti na Rasimu ya Katiba Mpya, Bunge Maalum la Katiba na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki.

  CC iliendelea kuwaagiza viongozi wote wa chama kama ilivyoelekezwa na waraka namba 3 wa Katibu Mkuu wa mwaka 2011, katika ngazi zote kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara.

  Kuhusu uchaguzi wa Uzini, alisema CC imeridhika na maandalizi ya awali, ambayo chama kimeyafanya katika jimbo hilo na kuagiza sekretariati ya chama kufanya maandalizi zaidi kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi husika.

  Mbali na hayo, taarifa hiyo ilieleza kuwa CC pia ilifanya mapitio ya bajeti na kuweka kikomo cha matumizi ya fedha katika uchaguzi huo.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,999
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  CCM wavue tu hicho kiatu, kimewabana mno, bora wavae sandles.
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kiatu kinapwaya mkuu hakiwabani. ni kubwa mno siyo size yake!
   
 4. k

  kipinduka Senior Member

  #4
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa lip! 2namsubir tundu lissu uzin atuambie yale aliosema bungen
   
 5. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nadhani kiatu kimetobaka kwa chini huku wakitembea kwenye miiba
   
 6. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli usiopingika kwamba Chadema wamefanya kila linawezekana ili kufikia mwafaka mwema kwa amani. CCM wasipokubali wakabadili sheria ya mabadiliko ya katiba watanzania na dunia nzima watajua nani ni chanzo cha kuvunjika kwa amani yetu.
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  si kwamba wameona maandamano hayalipi? Au unaongelea amani ipi?
   
 8. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ukweli utasimama kua ukweli!
   
 9. d

  dotto JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kamuulize WAsira alichovuna pale jimboni kwake Bunda,Makutano na Serengeti.
   
 10. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Achana nae huyo mkuu hajui analolisema
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mazungumzo ni mchakato! Sasa sijui CDM itabidi wapewe draft ya mabadiliko kabla haijapelekwa Bungeni ili waridhie? Manake inaweza kwenda draft ambayo itakuwa haina vionjo vyao na ikapitishwa. Kama ikipitishwa bila vionjo vyao itabidi tena waanze mchakato wa mazungumzo!
   
 12. O

  Omr JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwaka huu mtapata kisukari na hizo juice za ikulu.
   
 13. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hawa JK akiwaendekeza sidhani kama tutafika mahali...Naina wanafurahia sana kwenda Ikulu kupiga picha.
   
 14. m

  mwikumwiku Senior Member

  #14
  Jan 25, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera mbowe na timu yako! Mwaka huu utajaza albamu
  mbili za picha na Mhe. Rais! Kwahiyo mnarudi tena lini vile!? Ha ha ha ha kahawa ya ikulu tam! Mtuleteage japo taarifa za utamu Wa juisi na kahawa ya ikulu.
   
 15. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Human being is humble if u treat him by persuasion viva chadema
   
 16. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nyie magamba mnasisitiza mazungumzo kuwa ndio njia pekee ya kutatua matatizo, CDM wameamua kutumia njia hiyo mnawabeza, wakiandamana mnakasirika. sasa mwambieni jk asipotekeleza maoni ya CDM maandamano yatafuata.
   
 17. d

  dada jane JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kweli we ngwendu. Akili yako haishtuki tu.
   
 18. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Lakini si zinatokana na kodi zao? Au mkuu alitengenezea machungwa ya tanga kwa ka bi kadogo kake????
   
 19. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Napendekeza kikao kijacho kifanyikie makao makuu ya chadema,kwanini ikulu kila siku?kuna biashara ikulu ccm wanaiendesha kwa ubi na chadema ambayo sisi hatuijui?ikulu ni mahali patakatifu,sio kijiwe cha kukutania wanasiasa pale!waende wakakutanie kwenye vyama vyao huko au mahotelini,maana naona sasa umekua mchezo watu wanapisha tu kwenye mageti ya ikulu,wakitoka hawa wanaingia wale wengine wanaofukuza wabunge ili tulipie gharama za uchaguzi mdogo kwa hela zetu za kodi..
   
 20. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #20
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,999
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mkuu kiliwapwaya baada ya nyerere kung'atuka na kuwaachia, loh! wakajaza matambala mabovu na soksi zinazotoa uvundo (mafisadi) ili angalau kiwabane bane kumbe ndo wameharibu kabisa, asaivi wamenenepeana mavitambi hayo, miili km mapipa, viatu vinawabana hadi vinawachubua ngozi na kutoa vidonda, heri wavue waachie mwingine avae.
   
Loading...