Meitinyiku L. Robinson
JF-Expert Member
- Aug 29, 2011
- 412
- 90
Kuna mambo ambayo inabidi ifikie mahali tuyajadili kwa kuamua kwa moyo wa dhati kabisa kuweka Itikadi zetu kando na kuamua kuzungumza na kutoa ushauri ili kuona ni kwa jinsi gani twaweze kutibu kosa kwa busara na si kwa kosa jingine. Lusinde Livingstone alipoteza utu, na heshima mbele ya jamii kwa kufikiri na kuamini kuwa kosa alilofanya flani yeye atalitibu kwa kufanya vivyo hivyo. Haiyumkini alikosa mshauri mzuri ama pale ndipo fikra zake zilipoishia.
Ntaomba nitazame mambo mawili ambayo CDM sijajua mpaka leo wamefikira nini juu ya hayo moja ni wimbo wa Taifa na la pili ni hili la kujitangazia Uhuru wa Jimbo.
Pamekuwa na mazungumzo na majadiliano mengi humu ndani juu ya Wimbo wetu wa Taifa kufanyiwa ama marekebishao au kuchakachuliwa Mkoani Arusha na kuingizwa maneno ambayo kwa hali ya kawaida hayaendi si tu na lengo ama maana ya wimbo bali yanapelekea kuvunja heshima ya Wimbo wenyewe.
Binafsi ni muumini mzuri ama najitahidi kuwa muunini mzuri wa dini yetu ya Uzalendo ambayo CDM imekuwa mstari wa mbele kuihubiri na kugusa jamii kubwa ya Watanzania manake katika hali ya kawaida bila Uzalendo wewe huwezi kuwa kitu katika Nchi ama Taifa lako zaidi utaendekeza unafiki. Na ndiyo maana tunaamini pasipo shaka kwamba hawa waibao mali za uma Uzalendo si tu kwamba ni walafi bali Uzalendo haumo na haujawahi kuwa ndani yao na wako tayari hata kuuza Nchi.
Taifa kama Taifa ukiacha mambo mengine mbali mbali kuna mambo makubwa ya msingi ambayo Nchi ama Taifa hujivunia, hueshimu, hutunza na kulinda kwa gharama yeyote na hufikia kutoa adhabu pale ambapo huona kuna ukiukwaji wa taratibu na hivi ni pamoja na WIMBO WA TAIFA na BENDERA YA TAIFA.
Unapozungumzia Wimbo wa Taifa unazungumzi nembo ya Nchi, unapoimba Wimbo wa Taifa unahisi kitu ndani yako na hicho unachokihisi ndio uzalendo wako kwa Taifa lako, unaposikia Redioni Wimbo wa Taifa unapigwa mtu unashtuka kwamba ni nini kimetokea n.k. Si wimbo kama Nyimbo za Chama flani ama Taasisi flani ama Nyimbo za Shule n.k. Ni Wimbo wa Taifa.
Kwa kweli binafsi nipata hofu sana kusikia Wimbo wa Taifa kubadilishwa na kuimbwa hivyo ulivyoimbwa na waliofanya hivyo ni wale tunaoamini kuwa wanafanya damu ya Watanzania ijawe na Uzalendo ili tuweze kutibu Nchi, hii ni hatari, Naamini kulikuwa na Viongozi waandamizi wa Chama waliokuwa na uwezo wa kusema hapana na kuwapa Wananchi wa Arusha sababu za kusema hapana na kwa vile naelewa kuwa wananchi wa Arusha ni waelewa wangilielewa hilo na kuacha mara moja lakini sijajua ni kwa nini walikaa kimya na kuacha yatokee hayo yaliyotokea.
Hoja ni kwamba Wimbo huo tayari maana yake imeshapotezwa na CCM lakini hii haiwezi kuwa hoja hata kidogo manake si vyema kuogelea katika makosa ambayo yamekwisha fanywa na CCM na badala yake ni kutafuta namna ya kuratibisha na kuyatibu tena kwa Chama kama CDM ambacho kina tazamia kuwa mbadala wa CCM walitakiwa watibu haya manake kama yakiachwa hivyo basi tutegemee NCCR ama vyama vingine vijavyo kuja kufanya haya siku za mbeleni lakini kama viongozi wangeamua kuwakataza na kutoa sababu juu ya kukataa ile maana halisi ya Uzalendo ingeendelea kumea vyema na hatimaye kuchipua vizuri. Kwa kweli hili si la kulifumbia macho na Viongozi waangalie namna yeyote ya kutoa kauli juu ya hili na kulisimamisha mara moja ili kujengea Wimbo wetu heshima. Isije kufikia mahali na Bendera ya Nchi nayo ikawekewa tafrani sasa.
Tuujengee Wimbo heshima; heshima ambayo tunadhani na tunaamini kuwa wengine wameshindwa kuujengea, heshima ambayo Mwalimu aliijengea lakini imeonekana kuwa haina mana tena, heshima ambayo itatupa kutambulika mbele ya Mataifa mengine, heshima ambayo tutajivunia kwayo, na heshima ambayo itatupa kuutambua Uzalendo wetu vyema kadiri siku zinavyozidi kwenda.
Jambo la pili nami nigusie kidogo ni hili la Mhe. Mbunge kujitangazia Uhuru wa Jimbo; binafsi hili kwanza lilinifurahisha pamoja na kuwa mtu anaweza kuongea tu kwa sababu anaongea ila naamini Viongozi ni sharti wawe na mipaka ama utashi wakati wazungumzapo. Na ni lazma ifikie mahali kiongozi kabla hujasema kwanza utambue faida na hasara ya hayo unayotaka kuyasema na italeta tafsiri ipi kwa jamii na wewe binafsi utapokelewaje na jamii na si jamii ile unayoiongoza tu bali hata ile usiyoiongoza. Vyovyote vile ambavyo Nassari alitaka kumaanisha ama kama alikuwa na maana yeyote nyingine iwayo ni lazma atambue kuwa kwa wakati huu jamii inamtazama kwa namna tofauti kabisa na wakati mwingine jamii inakuwa na imani chanya juu yake hivyo kila akisema jambo jamii huamini juu ya jambo lenyewe manake si wote wenye Elimu na Uwezo kama wa kwake.
Nakumbuka Mzee Kirilo Japhet (Marehemu) wakati Mwalimu anapigania Uhuru wa Tanganyika yeye alienda kuomba Uhuru wa Wameru sasa nashindwa kujua kama Nassari anafuata nyayo za mzee Kirilo ama! Ila kwa maneno haya unaweza ukaona ni kawaida sana lakini kwa tamko hilo la Mhe. Mbunge ni sawa na kusema kwamba Majimbo mengine hayako Huru hata yale yanayoongozwa na CDM nayo hayako Huru. Ni kauli ndogo isiyostahili hata kidogo kuachwa hivi hivi. Nassari apate karipio manake hapa hakuitukana CCM tu bali kakidhalilisha mpaka Chama chake anachokitumikia pamoja na Wabunge wa Chama Chake na wapiga kura wote na Taifa zima. Huu ni ubaguzi usiostahili na ni ukiukwaji na uvunjwaji wa Katiba hasa Ibara ya 1, 2, 28, na 26. Najua bado Mhe. Mbunge hajataja mipaka ya Nchi husika ambayo wengi wangependa kufahamu ili tujue kwa wale waendao Mikoani kupitia Meru je watahitajika kuwa na Pasi ya kusafikiria??
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki JF
MEITINYIKU L. Robinson