CHADEMA lazima watambue kuwa huwezi tibu kosa la Kwanza kwa kosa la Pili.

  • Thread starter Meitinyiku L. Robinson
  • Start date

Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2011
Messages
412
Likes
1
Points
0
Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2011
412 1 0
Kuna mambo ambayo inabidi ifikie mahali tuyajadili kwa kuamua kwa moyo wa dhati kabisa kuweka Itikadi zetu kando na kuamua kuzungumza na kutoa ushauri ili kuona ni kwa jinsi gani twaweze kutibu kosa kwa busara na si kwa kosa jingine. Lusinde Livingstone alipoteza utu, na heshima mbele ya jamii kwa kufikiri na kuamini kuwa kosa alilofanya flani yeye atalitibu kwa kufanya vivyo hivyo. Haiyumkini alikosa mshauri mzuri ama pale ndipo fikra zake zilipoishia.

Ntaomba nitazame mambo mawili ambayo CDM sijajua mpaka leo wamefikira nini juu ya hayo moja ni wimbo wa Taifa na la pili ni hili la kujitangazia Uhuru wa Jimbo.

Pamekuwa na mazungumzo na majadiliano mengi humu ndani juu ya Wimbo wetu wa Taifa kufanyiwa ama marekebishao au kuchakachuliwa Mkoani Arusha na kuingizwa maneno ambayo kwa hali ya kawaida hayaendi si tu na lengo ama maana ya wimbo bali yanapelekea kuvunja heshima ya Wimbo wenyewe.

Binafsi ni muumini mzuri ama najitahidi kuwa muunini mzuri wa dini yetu ya Uzalendo ambayo CDM imekuwa mstari wa mbele kuihubiri na kugusa jamii kubwa ya Watanzania manake katika hali ya kawaida bila Uzalendo wewe huwezi kuwa kitu katika Nchi ama Taifa lako zaidi utaendekeza unafiki. Na ndiyo maana tunaamini pasipo shaka kwamba hawa waibao mali za uma Uzalendo si tu kwamba ni walafi bali Uzalendo haumo na haujawahi kuwa ndani yao na wako tayari hata kuuza Nchi.

Taifa kama Taifa ukiacha mambo mengine mbali mbali kuna mambo makubwa ya msingi ambayo Nchi ama Taifa hujivunia, hueshimu, hutunza na kulinda kwa gharama yeyote na hufikia kutoa adhabu pale ambapo huona kuna ukiukwaji wa taratibu na hivi ni pamoja na WIMBO WA TAIFA na BENDERA YA TAIFA.

Unapozungumzia Wimbo wa Taifa unazungumzi nembo ya Nchi, unapoimba Wimbo wa Taifa unahisi kitu ndani yako na hicho unachokihisi ndio uzalendo wako kwa Taifa lako, unaposikia Redioni Wimbo wa Taifa unapigwa mtu unashtuka kwamba ni nini kimetokea n.k. Si wimbo kama Nyimbo za Chama flani ama Taasisi flani ama Nyimbo za Shule n.k. Ni Wimbo wa Taifa.

Kwa kweli binafsi nipata hofu sana kusikia Wimbo wa Taifa kubadilishwa na kuimbwa hivyo ulivyoimbwa na waliofanya hivyo ni wale tunaoamini kuwa wanafanya damu ya Watanzania ijawe na Uzalendo ili tuweze kutibu Nchi, hii ni hatari, Naamini kulikuwa na Viongozi waandamizi wa Chama waliokuwa na uwezo wa kusema hapana na kuwapa Wananchi wa Arusha sababu za kusema hapana na kwa vile naelewa kuwa wananchi wa Arusha ni waelewa wangilielewa hilo na kuacha mara moja lakini sijajua ni kwa nini walikaa kimya na kuacha yatokee hayo yaliyotokea.

Hoja ni kwamba Wimbo huo tayari maana yake imeshapotezwa na CCM lakini hii haiwezi kuwa hoja hata kidogo manake si vyema kuogelea katika makosa ambayo yamekwisha fanywa na CCM na badala yake ni kutafuta namna ya kuratibisha na kuyatibu tena kwa Chama kama CDM ambacho kina tazamia kuwa mbadala wa CCM walitakiwa watibu haya manake kama yakiachwa hivyo basi tutegemee NCCR ama vyama vingine vijavyo kuja kufanya haya siku za mbeleni lakini kama viongozi wangeamua kuwakataza na kutoa sababu juu ya kukataa ile maana halisi ya Uzalendo ingeendelea kumea vyema na hatimaye kuchipua vizuri. Kwa kweli hili si la kulifumbia macho na Viongozi waangalie namna yeyote ya kutoa kauli juu ya hili na kulisimamisha mara moja ili kujengea Wimbo wetu heshima. Isije kufikia mahali na Bendera ya Nchi nayo ikawekewa tafrani sasa.

Tuujengee Wimbo heshima; heshima ambayo tunadhani na tunaamini kuwa wengine wameshindwa kuujengea, heshima ambayo Mwalimu aliijengea lakini imeonekana kuwa haina mana tena, heshima ambayo itatupa kutambulika mbele ya Mataifa mengine, heshima ambayo tutajivunia kwayo, na heshima ambayo itatupa kuutambua Uzalendo wetu vyema kadiri siku zinavyozidi kwenda.

Jambo la pili nami nigusie kidogo ni hili la Mhe. Mbunge kujitangazia Uhuru wa Jimbo; binafsi hili kwanza lilinifurahisha pamoja na kuwa mtu anaweza kuongea tu kwa sababu anaongea ila naamini Viongozi ni sharti wawe na mipaka ama utashi wakati wazungumzapo. Na ni lazma ifikie mahali kiongozi kabla hujasema kwanza utambue faida na hasara ya hayo unayotaka kuyasema na italeta tafsiri ipi kwa jamii na wewe binafsi utapokelewaje na jamii na si jamii ile unayoiongoza tu bali hata ile usiyoiongoza. Vyovyote vile ambavyo Nassari alitaka kumaanisha ama kama alikuwa na maana yeyote nyingine iwayo ni lazma atambue kuwa kwa wakati huu jamii inamtazama kwa namna tofauti kabisa na wakati mwingine jamii inakuwa na imani chanya juu yake hivyo kila akisema jambo jamii huamini juu ya jambo lenyewe manake si wote wenye Elimu na Uwezo kama wa kwake.

Nakumbuka Mzee Kirilo Japhet (Marehemu) wakati Mwalimu anapigania Uhuru wa Tanganyika yeye alienda kuomba Uhuru wa Wameru sasa nashindwa kujua kama Nassari anafuata nyayo za mzee Kirilo ama! Ila kwa maneno haya unaweza ukaona ni kawaida sana lakini kwa tamko hilo la Mhe. Mbunge ni sawa na kusema kwamba Majimbo mengine hayako Huru hata yale yanayoongozwa na CDM nayo hayako Huru. Ni kauli ndogo isiyostahili hata kidogo kuachwa hivi hivi. Nassari apate karipio manake hapa hakuitukana CCM tu bali kakidhalilisha mpaka Chama chake anachokitumikia pamoja na Wabunge wa Chama Chake na wapiga kura wote na Taifa zima. Huu ni ubaguzi usiostahili na ni ukiukwaji na uvunjwaji wa Katiba hasa Ibara ya 1, 2, 28, na 26. Najua bado Mhe. Mbunge hajataja mipaka ya Nchi husika ambayo wengi wangependa kufahamu ili tujue kwa wale waendao Mikoani kupitia Meru je watahitajika kuwa na Pasi ya kusafikiria??

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki JF

MEITINYIKU L. Robinson
 
KOMBESANA

KOMBESANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2009
Messages
905
Likes
33
Points
45
KOMBESANA

KOMBESANA

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2009
905 33 45
Mchg Mtikila anapeperusha bendera ya Tanganyika hapa Ilala maeneo ya TBL na hajafanywa kitu na yeyote.Sasa wewe huoni kuwa hata Uhuru alioenda kudai Nyerere baadaye Tanganyika ilimezwa?Je ardhi ya Wameru aliyoenda kudai imeshapatikana?Tafuta kitabu ya ISMAELI MBISE-BLOOD ON OUR LAND,hujui kabisa historia ama kama unajua maslahi ya rejareja yamekufanya uzibe fahamu zako na utake kuleta mjadala tata
Nina hakika wewe siyo mzalendo ni mwana CCM ambaye umeogopa mno kuona watu wakivua magamba na kuvaa magwanda na unaweza kujifia kwa shiunikizo la damu Arusha yote na Kilimanjaro au Tanzania ikiwa chini ya CDM.
Kwa sasa mkuu wangu kata shauri maana neema ya kujivua gamba itakapokwisha watakuvua gamba na kukupeleka kwa hakimu na pengine Kisongo utapaishikama mfungwa.
 
Ronal Reagan

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
4,837
Likes
1,558
Points
280
Ronal Reagan

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
4,837 1,558 280
Hilo la pili lilijibiwa muda ule ule na kufutwa kwenye hansard na Mh. Mbowe.

Hilo la wimbo lina mambo kadhaa ambayo lazima uyafikirie. Utashi, umilki, maudhui nk. Kwa mfano wimbo wowote lazima ujenge hisia kwa yule mwenye kuusikia/kuimba. Wimbo bila hisia ni kama wingu bila mvua, hutapata kilichokusudiwa.

Sasa huu wimbo tulio nao una mapengo kidgo. Of coz ulikopwa kwa jirani zetu wa nchi za kusini, na ukawekewa maneno ya kiswahili tu basi. Unahitaji kuangaliwa upya.

Pamoja na hayo, sio busara wala sheria ku-puuza wimbo uliopo pamoja na madhaifu yake.

Ila ningependa Tanganyika irudi, iwe na wimbo, bendera, serikali yake nk. Z'bar inavyo tayari. Kisha baada ya hapo tukae chini pamoja na kuangalia maswala haya ya "Muungano", sio kabla.
 
M

MAKAWANI

Senior Member
Joined
May 3, 2012
Messages
101
Likes
1
Points
35
M

MAKAWANI

Senior Member
Joined May 3, 2012
101 1 35
Nadhani hukumwelewa Nassari na Zitto aliyezungumzia jambo hilo vizuri. Uhuru aliouzungumzia Nassari na Zitto ni huu wa wawekezaji kupewa mashamba yote ya arumeru huku wana arumeru wakiambulia kuwa Manamba. Ukweli wa hili jambo haukupingwa na Mzindua Kampeni wa ccm bwana Mkapa ambaye alijifanya eti atayapeleka matatizo hayo kwa rais ilihali akijua ni yeye chanzo na haitowezekana. Kinachoendelea sasa kati ya wawekezaji na waarumeru ni uthibitisho tosha wa hili. Wapiganaji wanaojua ukweli wamechinjwa na hakuna hatua za kuridhisha zaidi ya washiriki wa watuhumiwa kujichunguza wenyewe. Swala la wimbo wa Taifa limechangiwa na watawala wenyewe na sio CDM maana uzalendo wa nchi hii umetaifishwa na watu flan flan wanaotafuna nchi mchana kweupe. Hilo ni ashiria la Taifa kupoteza uelekeo na suluhisho pekee ni MABADILIKO YA KWELI.

Mungu ibariki Tanzania, wabariki na watu wake!
 
Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2011
Messages
412
Likes
1
Points
0
Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2011
412 1 0
Mchg Mtikila anapeperusha bendera ya Tanganyika hapa Ilala maeneo ya TBL na hajafanywa kitu na yeyote.Sasa wewe huoni kuwa hata Uhuru alioenda kudai Nyerere baadaye Tanganyika ilimezwa?Je ardhi ya Wameru aliyoenda kudai imeshapatikana?Tafuta kitabu ya ISMAELI MBISE-BLOOD ON OUR LAND,hujui kabisa historia ama kama unajua maslahi ya rejareja yamekufanya uzibe fahamu zako na utake kuleta mjadala tata
Nina hakika wewe siyo mzalendo ni mwana CCM ambaye umeogopa mno kuona watu wakivua magamba na kuvaa magwanda na unaweza kujifia kwa shiunikizo la damu Arusha yote na Kilimanjaro au Tanzania ikiwa chini ya CDM.
Kwa sasa mkuu wangu kata shauri maana neema ya kujivua gamba itakapokwisha watakuvua gamba na kukupeleka kwa hakimu na pengine Kisongo utapaishikama mfungwa.
Ni kwa vile hukujua ila ni bora ungekuwa wa mwisho kuchangia badala ya ulivyokuwa wa kwanza manake ungejifunza toka kwa wapili na watatu....... Hilo ni moja lakini la pili usidikiri tena na wala usithubutu kukifananisha ama CDM na Mchungaji Mtikila ama CDM na Chama anachokiongoza Mtikila na hayo usiyafanye ama kwa akili zako au za kukopeshwa...... Sorry to say so!!
 
Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2011
Messages
412
Likes
1
Points
0
Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2011
412 1 0
Nadhani hukumwelewa Nassari na Zitto aliyezungumzia jambo hilo vizuri. Uhuru aliouzungumzia Nassari na Zitto ni huu wa wawekezaji kupewa mashamba yote ya arumeru huku wana arumeru wakiambulia kuwa Manamba. Ukweli wa hili jambo haukupingwa na Mzindua Kampeni wa ccm bwana Mkapa ambaye alijifanya eti atayapeleka matatizo hayo kwa rais ilihali akijua ni yeye chanzo na haitowezekana. Kinachoendelea sasa kati ya wawekezaji na waarumeru ni uthibitisho tosha wa hili. Wapiganaji wanaojua ukweli wamechinjwa na hakuna hatua za kuridhisha zaidi ya washiriki wa watuhumiwa kujichunguza wenyewe. Swala la wimbo wa Taifa limechangiwa na watawala wenyewe na sio CDM maana uzalendo wa nchi hii umetaifishwa na watu flan flan wanaotafuna nchi mchana kweupe. Hilo ni ashiria la Taifa kupoteza uelekeo na suluhisho pekee ni MABADILIKO YA KWELI.

Mungu ibariki Tanzania, wabariki na watu wake!
Mkuu sina mashaka na maneno yako ila kwa masahihisho aliyafanya Mhe Mbowe baada ya kauli ya Nassari ambayo nayakiri kuyapokea na kuelezwa baada ya kupost thread hii ni dhahiri kwamba kauli ya Nassari haikuwa kama ambavyo umefafanua humu ilikiuka taratibu.

Na hili la Wimbo wa Taifa ndiyo maana nimesema kosa la kwanza halitibiwi na la pili kama watawala wameshauharibu bado ni Wimbo wetu wa Taifa hatuna namna zaidi ya kuuheshimu na kuuenzi mpaka pale utakapopatikana mbadala. Lakini si kurudia kosa walilolifanya hao watawala manake sasa mwishowe wataonekana wote sawa.
 
Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2011
Messages
412
Likes
1
Points
0
Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2011
412 1 0
Hilo la pili lilijibiwa muda ule ule na kufutwa kwenye hansard na Mh. Mbowe.

Hilo la wimbo lina mambo kadhaa ambayo lazima uyafikirie. Utashi, umilki, maudhui nk. Kwa mfano wimbo wowote lazima ujenge hisia kwa yule mwenye kuusikia/kuimba. Wimbo bila hisia ni kama wingu bila mvua, hutapata kilichokusudiwa.

Sasa huu wimbo tulio nao una mapengo kidgo. Of coz ulikopwa kwa jirani zetu wa nchi za kusini, na ukawekewa maneno ya kiswahili tu basi. Unahitaji kuangaliwa upya.

Pamoja na hayo, sio busara wala sheria ku-puuza wimbo uliopo pamoja na madhaifu yake.

Ila ningependa Tanganyika irudi, iwe na wimbo, bendera, serikali yake nk. Z'bar inavyo tayari. Kisha baada ya hapo tukae chini pamoja na kuangalia maswala haya ya "Muungano", sio kabla.
Reagan Mkuu;
Kwanza nikushukuru kwa ufafanuzi na kuweka mambo sawa na nikiri nami nimepokea taarifa muda huu juu ya kufutwa kwa kauli ya Nassari na Mhe Mbowe nikiri pia kuwa ni busara ya hali ya juu aliyoitumia Mhe Mbowe katika kuweka mambo sawa na kuonesha kuwa CDM kipo kwa ajili ya Taifa na Watanzania kwa ujumla very impressing.

Lakini vile vile nikushuru kwa kutambua na kuona umuhimu wa kutokupuuza kwa namna yoyote ile Wimbo wetu wa Taifa haijalishi una kasoro gani ama umetokea wapi uheshimiwe kama ulivyo sasa hivi muda ukifika na pakionekana kuwa unahitaji kufanyiwa marekebisho basi ufanyiwe hivyo na si kudhihakiwa.
 
masopakyindi

masopakyindi

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2011
Messages
14,506
Likes
3,193
Points
280
masopakyindi

masopakyindi

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2011
14,506 3,193 280
Mtu yeyote(I mean yeyote yule iwe wa CCM,CUF au CHADEMA) kuchezea alama za Utaifa ni lazima achukuliwe hata kali ili liwe fundisho.
Kosa hili sasa hivi linaota mizizi, lilianzia kule visiwani.CUF na tamko la Zanzibar Ni Nchi hatujalisahau.
Kama hilo halikukemewa kwa nguvu zote nitashangaa kwa sasa kulikemea hili la Nassari na "Nchi yake ya Arumeru).
Miaka ya Nyerere watu hawa waliwekwa katika chumba kidogo na funguo kutupwa kwa miaka kadhaa ili watambue umuhimu wa Taifa kwanza.
 
M

MAKAWANI

Senior Member
Joined
May 3, 2012
Messages
101
Likes
1
Points
35
M

MAKAWANI

Senior Member
Joined May 3, 2012
101 1 35
Nchi ikiendeshwa kienyeji na mambo yake huwa ya kienyeji! Uzalendo unapaswa kuanzia kwa viongozi wa nchi wenyewe! Kama mtu anaiba bilioni tisa then kiongozi anasema hiyo ni changamoto badala ya kumchukulia hatua unategemea nini kwa walipa kodi wanaonyanyaswa na chao. Lisilokwepo machoni na moyoni halipo.
 
L

LOVI MEMBE

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2012
Messages
1,120
Likes
10
Points
135
L

LOVI MEMBE

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2012
1,120 10 135
Nadhani hukumwelewa Nassari na Zitto aliyezungumzia jambo hilo vizuri. Uhuru aliouzungumzia Nassari na Zitto ni huu wa wawekezaji kupewa mashamba yote ya arumeru huku wana arumeru wakiambulia kuwa Manamba. Ukweli wa hili jambo haukupingwa na Mzindua Kampeni wa ccm bwana Mkapa ambaye alijifanya eti atayapeleka matatizo hayo kwa rais ilihali akijua ni yeye chanzo na haitowezekana. Kinachoendelea sasa kati ya wawekezaji na waarumeru ni uthibitisho tosha wa hili. Wapiganaji wanaojua ukweli wamechinjwa na hakuna hatua za kuridhisha zaidi ya washiriki wa watuhumiwa kujichunguza wenyewe. Swala la wimbo wa Taifa limechangiwa na watawala wenyewe na sio CDM maana uzalendo wa nchi hii umetaifishwa na watu flan flan wanaotafuna nchi mchana kweupe. Hilo ni ashiria la Taifa kupoteza uelekeo na suluhisho pekee ni MABADILIKO YA KWELI.

Mungu ibariki Tanzania, wabariki na watu wake!
Swala la wimbo wa Taifa limechangiwa na watawala wenyewe na sio CDM maana uzalendo wa nchi hii umetaifishwa na watu fulani fulani wanaotafuna nchi bila huruma kwa nchi yenyewe na wananchi wake bila chembe ya huruma mchana kweupe.mmojawao ni rais jakaya kikikwete na mwanaye wa kuzaa ridhiwani jakaya mrisho halfani kikwete
 
mnyongeni

mnyongeni

Senior Member
Joined
Dec 6, 2011
Messages
137
Likes
0
Points
33
mnyongeni

mnyongeni

Senior Member
Joined Dec 6, 2011
137 0 33
uzalendo wa kwenye wimbo huku watu wanaumia, wanateseka, hawana chakula, wamekata tamaa, wanaibiwa kila siku, watoto wanafeli kila kukicha, mahospitali hayana vifaa,..........
uzalendo huu hauna maana ndo maana zamani watu wimbo ulikuwa ukiimbwa tunasimama, mi siku hizi hata sisimami. kwasababu vyote hivyo vimeshachakachuliwa na ZZM cdm wanafanya kuedit tu..
 
Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2011
Messages
412
Likes
1
Points
0
Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2011
412 1 0
uzalendo wa kwenye wimbo huku watu wanaumia, wanaseteka, hawana chakula, wamekata tamaa, wanaibiwa kila siku, watoto wanafeli kila kukicha, mahospitali hayana vifaa,..........
uzalendo huu hauna maana ndo maana zamani atu wimbo ulikuwa ukiimbwa tunasimama, mia siku hizi hata sisimami. kwasababu vyote hivyo vimeshachakachuliwa na ZZM.
"................................akawauliza mwanao akinyea kiganja chake utausafisha ama utaukata......??" Mi nadhani ndugu yangu mnyongeni wewe jibu lako litakuwa "utaukata"
 
Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2011
Messages
412
Likes
1
Points
0
Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2011
412 1 0
Swala la wimbo wa Taifa limechangiwa na watawala wenyewe na sio CDM maana uzalendo wa nchi hii umetaifishwa na watu fulani fulani wanaotafuna nchi bila huruma kwa nchi yenyewe na wananchi wake bila chembe ya huruma mchana kweupe.mmojawao ni rais jakaya kikikwete na mwanaye wa kuzaa ridhiwani jakaya mrisho halfani kikwete
Mkuu;

It should be noted clearly that I aint disputing the fact that the so called watawala wamechangia katika kuharibu ama kudhalilisha nembo zetu za Taifa....... I have tried to put myself cristal clear that TWO WRONGS WILL NEVER MAKE IT RIGHT...... Hatupaswi kufuata ya hao waitwao watawala bali kimsingi tunapaswa kuwafahamisha kuwa wanaharibu Nchi kwa neno na kwa tendo........... Period
 
democratic

democratic

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2011
Messages
1,644
Likes
2
Points
0
democratic

democratic

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2011
1,644 2 0
Reagan Mkuu;
Kwanza nikushukuru kwa ufafanuzi na kuweka mambo sawa na nikiri nami nimepokea taarifa muda huu juu ya kufutwa kwa kauli ya Nassari na Mhe Mbowe nikiri pia kuwa ni busara ya hali ya juu aliyoitumia Mhe Mbowe katika kuweka mambo sawa na kuonesha kuwa CDM kipo kwa ajili ya Taifa na Watanzania kwa ujumla very impressing.

Lakini vile vile nikushuru kwa kutambua na kuona umuhimu wa kutokupuuza kwa namna yoyote ile Wimbo wetu wa Taifa haijalishi una kasoro gani ama umetokea wapi uheshimiwe kama ulivyo sasa hivi muda ukifika na pakionekana kuwa unahitaji kufanyiwa marekebisho basi ufanyiwe hivyo na si kudhihakiwa.
kaka kwanza nikushukuru kwamba ni mtu unaetambua kuwa kuna umuhimu wa kuheshimu nembo zetu kama taifa.Jambo la pili hiki kitu kama hujui kin achochewa sana na uzalendo,na uzalendo huu ni lazima wananchi wauige kutoka kwa viongozi wao na mbowe hawezi simama mbele ya mkutano mkubwa kiasi kile na kuwafundisha watu namna ya kuimba wimbo wa taifa
so katika hili ndugu yangu utawaonea tu cdm kwani uzalendo umevurugwa na viongozi kwanza,hivyo huwezi ukakuta viongozi ambao hawana uzalendo,mafisadi,watu wanaiba hawapelekwi mahakamani halafu wananchi wawe ni wazalendo na waimbe wimbo wa taifa inavyopaswa.
 
Fredrick Sanga

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2011
Messages
3,149
Likes
22
Points
135
Fredrick Sanga

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2011
3,149 22 135
Jamani huu wimbo umefanyiwa nini? Hebu nielimisheni, sijaelewa.
 
M

MAKAWANI

Senior Member
Joined
May 3, 2012
Messages
101
Likes
1
Points
35
M

MAKAWANI

Senior Member
Joined May 3, 2012
101 1 35
Punda utampeleka mtoni but huwezi kumlazimisha anywe maji. Na wahenga walisema sikuzote nyuki hakumbatiwi wala hapigwibusu! TAFAKARI.... CHUKUA HATUA. LETA MABADILIKO.
 
Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2011
Messages
412
Likes
1
Points
0
Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2011
412 1 0
kaka kwanza nikushukuru kwamba ni mtu unaetambua kuwa kuna umuhimu wa kuheshimu nembo zetu kama taifa.Jambo la pili hiki kitu kama hujui kin achochewa sana na uzalendo,na uzalendo huu ni lazima wananchi wauige kutoka kwa viongozi wao na mbowe hawezi simama mbele ya mkutano mkubwa kiasi kile na kuwafundisha watu namna ya kuimba wimbo wa taifa
so katika hili ndugu yangu utawaonea tu cdm kwani uzalendo umevurugwa na viongozi kwanza,hivyo huwezi ukakuta viongozi ambao hawana uzalendo,mafisadi,watu wanaiba hawapelekwi mahakamani halafu wananchi wawe ni wazalendo na waimbe wimbo wa taifa inavyopaswa.
Ndugu yangu Mwanademokrasia shukrani hizi zikuridie pia Mkuu;

Lengo langu kuu ndugu ni wajibu walio nao CDM juu ya Taifa hili naamini mafunzo na changamoto wanazozitoa CDM ndani ya Taifa hili ndiyo yaliyoikisha hapo ilipo mpaka Wananchi kuamini kwamba sasa tumepata mbadala. Hivyo basi kuwaasa ama kuwajuza wananchi juu ya umuhimu wa nembo za Taifa haigharimu kitu na kingefanyika pale pale kwa kuwaelewesha Wananchi juu ya hilo manake kama wasipoambiwa wao wataona wako sawa na ni haki wao kufanya hivyo sasa wahenga walisema Samaki Mkunje angali Mbichi binafsi napata taabu kama tusipowaambia leo kesho watakuwa wameshaota mizizi na mifupa hivyo kuwarudisha kule tunakotaka itakuwa kazi. It can be done.......
 
Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2011
Messages
412
Likes
1
Points
0
Meitinyiku L. Robinson

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2011
412 1 0
Punda utampeleka mtoni but huwezi kumlazimisha anywe maji. Na wahenga walisema sikuzote nyuki hakumbatiwi wala hapigwibusu! TAFAKARI.... CHUKUA HATUA. LETA MABADILIKO.
Kuna vitu vingine vinahitaji uweke rohoni pembeni ili uchangie mathalan hili la Nyuki katika hali ya kawaida wewe umetoka wapi mpaka ukakumbatie ama kubusu nyuki. Na kuna aina nyingi za Nyuki sasa ni yupi asiyekumbatiwa ama kupigwa busu.
 
Forum statistics

Threads 1,272,642
Members 490,095
Posts 30,455,814