Mimi huwa ninashangaa na kusikitika sana kuona CHADEMA, Lowasa na Mbowe ambao ni viongozi wenye heshima na wafuasi wengi sana hapa nchini hawamchukulii hatua za kisheria Nape kwa kuwakashifu juu ya kuuziana Chama cha siasa kwa mabilioni ya fedha. Ninajiuliza pia ni kwanini Nape hajatakiwa kuwasaidia Polisi au TAKUKURU kufanya uchunguzi juu ya madai haya ya rushwa kwenye majukwaa ya kisiasa mbele ya maelfu ya watanzania. Hapa juzi karudia tena Iringa kwa kumuingiza Mchungaji Msigwa katika rushwa/mauziano haya eti kachota million 340! Jamani mkewe, ndugu zake na wafuasi watamuelewaje kama hawapati mgao? Huku si ni kuhatarisha maisha yake?
Huyu Nape, hajawahi kutoa ushahidi wowote mahali popote kuhusu madai haya ambayo ni very serious ambayo kama ni kweli ni hatari kwa mustakabali wa kisiasa wa nchi yetu. Hivi ni kweli na haki watu wazima naheshima zenu mkubali kuitwa wezi kwa majina mbele ya halaiki ya watanzania na mkae kimya as if nothing has been said? Wako wapi wanasheiria Kibatala, Lisu, Prof. Safari na Marando? Je? mnataka tuamini kwamba madai haya ni kweli? Kumbuka "Uongo ukirudiwa mara nyingi, watu wengi huamini kuwa ni ukweli" joseph Goebbels ( mpiga propanda wa hitler)