Elections 2015 Kutoka Iringa: Kampeni CCM uwanja wa Samora

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,575
2,000
CCM wao wenyewe walishakaaga chini na kusema kumshambulia Lowassa ni sawa na kumpandisha chart!
 

jipange

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
208
170
Hawa jamaa sjui wanatumia kilevi gani kabla ya kupanda jukwaani

http://m.youtube.com/watch?v=VZdbqAJGf20

Vyombo husika tunataraji hatua kali kwa huu udhalilishaji
Mkuu mbona link haifunguki.pls iweke tena
 

Perus

Member
Aug 17, 2015
34
0
Habari wakuu,

Leo ni muendelezo wa kampeni, mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi ndugu Magufuli leo yupo uwanja wa Samora mjini Iringa. Tuwe pamoja kujuzana yanayojiri kutoka Iringa.
======
View attachment 292579
Anaeongea kwa sasa ni aliyekuwa waziri wa ardhi, ndugu William Lukuvi na anampigia chapuo mgombea anaewania ubunge jimbo la Iringa mjini ndugu Mwakalebela, pia anampigia chapuo mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi ndugu Magufuli.

Nape: Siku moja UKAWA walikuwa wanazindua mkutano wao Dar, nikiwa pale wakaanza kubishana Magufuli ametumia muda mrefu sana kuongea, nikawaambia mgombea wa UKAWA akifikisha dakika kumi na tano natoa milioni tano na nikazitanguliza, nikaulizwa ulijuaje, nikawaambia tatizo Lowassa anadhani Ikulu ni wodi ya wagonjwa.

Watanzania hatutaki Rais wa majaribio, ambae tukimwambia akakague majeshi yetu hawezi, tumchague tingatinga. Watanzania wameshaamua, hawawezi kupeleka fisadi Ikulu. Nakumbuka nilikuwa nahangaika na magamba, gamba namba moja Lowassa kashaondoka na chama kiko safi.

Kuna watu walikuwa wanakifanya chama chaka la kujifichia, wanaharibu katika serikali na kukimbilia katika chama wakiongozwa na Lowassa, tunaamini mabadiliko tunayoyataka ndani ya serikali na CCM tutayapata kwa ndugu Magufuli, katika orodha hakuna mtu alienistua kama Edward Lowassa. Nikasema na huyu fisadi anataka kwenda ikulu? Akasema hamuwezi kuzuia mafuriko, nikamwambia mafuriko yanazuiwa hata kwa kidole.

Mimi ni msemaji wa chama, kwanini hatukumpa nafasi mwizi? Hiyo habari ya ugonjwa anaijua yeye mwenyewe na tumuombee mungu tarehe 25 ashuhudie tunavyorudi Ikulu kwa kishindo!

Tunataka watuambie hata kazi moja tu ambayo Lowassa amefanya hakuiba, tulimpa uwaziri mkuu na miaka miwili tu Richmond, kazi gani ambayo tumempa Lowassa hakutumia madaraka yake vibaya na hakuiba? Mtu mwenye historia ya namna hii hatuwezi kumpeleka Ikulu, weka mbali na Ikulu.

Upande wa pili tunae Magufuli, nitajieni doa moja la Magufuli! Mbowe siku moja anasema vibaka wanachomwa moto, kibaka mkubwa Edward Lowassa yuko mtaani, leo amefika bei ya CHADEMA, wote kawatia mfukoni. Mzee Mtei kapigwa bilioni mbili, Mtei bilioni tatu na Msigwa ambae alisema atakaemuunga mkono Lowassa akapimwe akili. Sasa Msigwa tangulia mwenyewe ukapime akili yako mwenyewe.

Wakati wanajadili bei ya kuuzwa chama chao, Slaa alikuwemo ndani, nayajua mengi lakini leo nasema yanayomuhusu Msigwa, akaambie aende kufuta kauli akasema hawezi, akaambiwa basi nyamaza, akasema nipeni uji nishindwe kuinua mdopo, milioni 340 zikawekwa mezani ndio maana akipita anashindwa kumsema Lowassa na Magufuli, anabaki kusema nipeni kura. Uchungaji amesahau mtumishi huyu, tapeli mkubwa. Msigwa alisema watu wa Iringa msitumie bidhaa za ASAS, anaajiri vijana zaidi 400 Iringa na ndiye mlipa kodi mkubwa hapa Iringa. Anataka wale vijana 400 waje mtaani kuja kuwaandamanisha.

Tarehe 25 lazima tumwadhibu kwa kuhahakisha kura zote zinaenda kwa Mwakalebelela, wakati wa ujenzi wa barabara Iringa kwenda Dodoma, kambi ya Ujenzi ilitaka kuwekwa Iringa lakini ikabidi ikawekwe Dodoma akitaka eneo , kwanini! Msingwa. Sina mashaka Iringa tumemaliza, mwambieni pesa ziko wapi, pesa kidogo zilizobaki akale na mkewe, ya ubunge imeshaharibika.

Watanzania muombeeni mzee afya aone tunavyochukua nchi kwa kishindo, wanasema Nape alituambia bao la mkono, kelele watapiga sana lakini Ikulu inaenda kwa rangi za kijani, wenzetu wanahubiri mabadiliko, madadiliko ya kumuacha muadilifu tumpeleke mwizi, mabadiliko ya kumuacha mzima na kumpeleka marehemu. Kwa leo inatosha.

Magufuli
Anaeongea kwa sasa ni Magufuli na anawakosoa wale wanaosema serikali haijafanya kitu akiwemo mchungaji wa Iringa ambae aliamini anafata amri kumi. Anasema hata amani hamna chochote kilichofanyika! Anasema ni serikali hii hii ilileta vyama vingi 1992.

Sasa anaelezea kwanini ameomba urais ikiwemo kudumisha amani iliyopo na la pili ni kuafanya kazi na hatakuwa na blabla, analinganisha lami iliyoacha na mkoloni kwa miaka 76 na lami aliyojenga Kikwete kwa miaka 10. Pia anaelezea mipango yake ujenzi wa barabara njini Iringa ili magari makubwa yasikatishe Iringa mjini.

Anasema anafahamu hela ziko wapi na mapato hayo yatashuka chini kwa wananchi na anaeleza vipi atagharamia elimu bure mpaka kidato cha nne.


Hivi CCM imeshindwa kabisa kuilazimisha Serikali yao ipeleke mafao ya wastaafu pspf? Kazi ya chama ni nini?

Hao pspf sashivi wameshindwa kabisa, Ukiwapigia simu wanaweza wasipokee siku nzima, siku wakipokea unapewa majibu ya mkatao tu.
Na ukifanikiwa kuunganishwa na watu wa uhasibu, angalau wao ndio wanakupa majibu ya hali ilivyo kwenye file la mtu wenu. Kwamba hazina haijapeleka makato, ila unaweza kuwasiliana na CUSTOMER CARE MANAGER, yeye atajua namna ya kushughulikia madai yenu kwa haraka.

Tatizo sasa, ni namna ya kumpata huyo Customer Care Manager, mara uambiwe hayupo ofisini, mara uambiwe simu yake inaita tu bila majibu. Jamani tufanyeje sasa sisi watu wa huku mbali, na ndugu yetu ni mahututi? BACK TANZANIA
 
Last edited by a moderator:

aminah9

Member
Oct 8, 2014
83
125
Taarifa ya 4u movement kuhusu waliozimia tanga


Waliozimia ni watu waliotoka Kilimanjaro, Arusha na Manyara, walikuwa wana UCHOVU wa safari. Maana waliondoka kwao Asubuhi kwa kusombwa na mabasi na wakaingia Tanga mchana bila kupumzika, kula wala kunywa maji wala juice wakapitilizia uwanjaNi. Kwann wasizimie❓❗

Ninawapa pole maana ni watanzaNia wenzangu.

Ila huu mchezo wa kusomba watu kwenye mabasi mikoa mpaka mikoa uishe, watanzaNia wanateseka saNa.

Watu walisombwa kama watumwa toka mikoani kuja Tanga tena bila kula lazimwazimie, mungu awaponye haraka majerui tare 25 wachague hapa kazi tu
Pole we mleta umbea maana picha nliyoiona ni ya mwanafunzi wa mkwakwani, moshi hakuna uvaaji wa hao watu waliodondoka. Naandika kwa confidence kwa kuwa naishi moshi ila kikazi naishi tanga so kote kote nakufaham vizuri
 

danimutta

Senior Member
Nov 4, 2011
169
250
Mimi huwa ninashangaa na kusikitika sana kuona CHADEMA, Lowasa na Mbowe ambao ni viongozi wenye heshima na wafuasi wengi sana hapa nchini hawamchukulii hatua za kisheria Nape kwa kuwakashifu juu ya kuuziana Chama cha siasa kwa mabilioni ya fedha. Ninajiuliza pia ni kwanini Nape hajatakiwa kuwasaidia Polisi au TAKUKURU kufanya uchunguzi juu ya madai haya ya rushwa kwenye majukwaa ya kisiasa mbele ya maelfu ya watanzania. Hapa juzi karudia tena Iringa kwa kumuingiza Mchungaji Msigwa katika rushwa/mauziano haya eti kachota million 340! Jamani mkewe, ndugu zake na wafuasi watamuelewaje kama hawapati mgao? Huku si ni kuhatarisha maisha yake?

Huyu Nape, hajawahi kutoa ushahidi wowote mahali popote kuhusu madai haya ambayo ni very serious ambayo kama ni kweli ni hatari kwa mustakabali wa kisiasa wa nchi yetu. Hivi ni kweli na haki watu wazima naheshima zenu mkubali kuitwa wezi kwa majina mbele ya halaiki ya watanzania na mkae kimya as if nothing has been said? Wako wapi wanasheiria Kibatala, Lisu, Prof. Safari na Marando? Je? mnataka tuamini kwamba madai haya ni kweli? Kumbuka "Uongo ukirudiwa mara nyingi, watu wengi huamini kuwa ni ukweli" – joseph Goebbels ( mpiga propanda wa hitler)
 

Akilinzangu

Senior Member
Aug 15, 2015
133
170
Nape kaka yangu hii Dunia niya Mungu,kumwita mtu aliye hai maiti nimatusi makubwa sana,nakuhakikishia Nape tutakuzika wewe Lowasa akiwa hai hii dunia sio ya ccm maisha na kuishi ni Mungu anatupea sasa wewe unamkosoa Mungu kwa kumpa Lowasa maisha unamwita maiti akiwa hai sasa wewe ndiye utatanguli mbele za haki Lowasa utamuacha hapa Tz akiwa Raisi au akiwa Raia wakawaida.tuheshimu uhai wa watu wengine.
 

Akilinzangu

Senior Member
Aug 15, 2015
133
170
hivi kweli tumefikia kiwango hiki wtz?mtu anatoshana na baba yako unamtusi kiwango hicho?mimi siamini kama ni ccm hii inayo fanya kampeni za matusi kama haya
 

twahil

JF-Expert Member
May 31, 2011
4,059
2,000
Acheni propaganda zenu nyie ufipa...Nape anawapelekesha puta mnakimbilia hapa kutoa povu...
 

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
12,747
2,000
Kwani anajua nini huyo Nape???! Amekuwa akibebwa sana na JK. hajawahi kjitafutia amebebwa shauri wazazi wake ndio anakufuri
 

kamagetac

JF-Expert Member
Jul 25, 2014
2,478
2,000
Katika biblia kuna sehemu wameandika kuwa aombae hupewa na abishae mlango atafunguliwa na Mungu

Ninaomba kwa Mungu Nape asione siku Lowasa akiapishwa kuwa rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania

Awe ameshatangulia mbele kaburini,ndio ombi langu
 

KISHINDO

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
1,747
2,000
Nape kaka yangu hii Dunia niya Mungu,kumwita mtu aliye hai maiti nimatusi makubwa sana,nakuhakikishia Nape tutakuzika wewe Lowasa akiwa hai hii dunia sio ya ccm maisha na kuishi ni Mungu anatupea sasa wewe unamkosoa Mungu kwa kumpa Lowasa maisha unamwita maiti akiwa hai sasa wewe ndiye utatanguli mbele za haki Lowasa utamuacha hapa Tz akiwa Raisi au akiwa Raia wakawaida.tuheshimu uhai wa watu wengine.


Nadhani nape apewe nafasi akamwulize komba alichokisema kwa mzee warioba then arudi atwambie.

Nahisi nape ana elements za ukichaa so wakati mwingine tumhurumie tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom