CHADEMA laleni tu mtayaona ya CCM, wao hawalali ng'ooo....

Ndg zangu (Hossam,Sangarara), mimi naona badala ya kuzidi kulumbana ni bora sasa tusaidiane kuunda hoja ili tufikie malengo.
Nikweli kabisa ndg Hossam kwamba nguvu ya kisiasa inaitajika vijijini(japo hukufafanua ndo maana ukapewa majibu mepesi) na mnavojua vijiji vingi hapo kwetu viko nyuma ki-elimu ndo maana ni wepesi kukubali kutoa haki yao kwa 1kg tu ya nyama! Hivo basi inahitajika mikutano mingi ya hadhara kwa kila kijiji kuelimishwa juu ya ulaia, ikiwezekana nyumba hadi nyumba!

Pili,akina Mama wengi vijijini ni "ccm imenilea!!" Cdm iunde mkakati hasa kwa kutumia wanawake wenzao kuwaelimisha juu ya dhana hiyo potovu walionayo kuwaondolea uoga! e.g kijiji kwetu 2010 wanawake waliambiwa maana ya neno Slaa ni mapanga na bunduki, hivo mkimpa kura Slaa atawamaliza! Wengi waliogopa na hawakupiga kura!!

Kwa kushirikiana na wazawa wekeni makazi ya kudumu(ofisi) japo moja tu hii itatusaidia sana mbeleni.
Cdm kuna wasomi, wabunifu na sera zao ni kali tukishirikiana vyema na wewe unaesoma jf nina uhakika nchi itakombolewa.
Cdm msikate tamaa sasa tuko 50/50 inahitajika nguvu kidogo tu tufikie malengo!

GOD BE WITH CDM!!
 
Wote hossam na sangara mna mawazo mazuri tunaomba yafanyiwe kazi. Labda nichangie kwamba kuna haja ya kukagua kadi za kupigia kura kwa wote wanaokuja kwenye mikutano kabla ya mkutano ili kujiridhisha kwamba ni wapiga kura halali na hawatafanya makosa bila hivyo tutakuwa tunajaza watu lakini wachache ndo wanatuchagua lakini margin na ccm inakuwa ndogo wanachakachua wanashinda sasa inatakiwa gap liwe kubwa ili uchakachuaji ushindikane pia watawi kila kijiji Tanzania naamini utakuwa mkakati wa ushindi.
 
" Cdm iunde mkakati hasa kwa kutumia wanawake wenzao.......

.....Kwa kushirikiana na wazawa!!....

GOD BE WITH CDM!!
Haya mambo mawili ni makubwa na ya msingi sana. Kule Igunga CDM ilkosa mawakala wazawa. swali la kujiuliza ni kwa nini? pia CDM haijawekeza katika kuwatoa na kuwaonyesha upendo wanawake kwani mikutano mingi ya CDM inajaza watu lakini 99% ya watu hao ni wanaume na moja asilimia ni wanawake.

wanawake wana tabia ya kuwasiliana wenyewe kwa wenyewe hivyo ni vizuri ukawepo mkakati wa kuongeza idadi ya wanawake kwenye watu wanaoiunga mkono CDM!
 
Asante Mkuu kwa kufikia tamati, jasho limenitoka lakini Mungu atatusaidia tu. CDM inaaminiwa, sasa ni jukumu lao kujua nguvu kuu iliyo nyuma yao, na kamwe wasiichezee. Asalam Aleykum!
naomba nimalize mjadala kwa kusema yafuatayo:
CCM imefanya hayo waliyofanya, kama mabaya tutawahukumu na kama ni mazuri tutawapongeza. CDM tunahitaji kutafuta mtaji wa wanachama wa dhati kila mahala wanapopatikana. Ufaransa 2010 walifanikiwa kucheza WOZA 2010 kwa goli la THIERY HENRY la mkono. CDM ikiwezekana kucheza reafu tucheze rafu. Faireness itafuata tukishachukua dola.
Vijana tulionao bado hawana ushawishi wa kutosha kuteka hisia za wazee hasa akina mama ambao bila ubishi ni mtaji kwa CCM. TUSIGOMBANE KWA KUWA TU TUNATOFAUTIANA KATIKA HOJA. UKOMAVU WA DEMOKRASIA NI PAMOJA KUVUMILIANA KTK HOJA NA HATIMAYE TUFIKIE MUAFAKA.
NAUNGA MKONO HOJA.
 
Back
Top Bottom