CHADEMA laleni tu mtayaona ya CCM, wao hawalali ng'ooo....

Hossam

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
3,399
1,857
Kumtambua adui yako ni 50% ya kumshinda, kutambua mbinu ya adui yako ni 75% ya kushinda na ilobaki ni juhudi ili ufanikishe ushindi wako. CDM isikae ikajidanganya na Peoples Power bila kuwa na mbinu za kuitunza na kuiongoza nguvu hiyo. Imani yangu ni kwamba CDM ishaeleweka sana mijini ila vijijini hawajui huyo ndio mnyama gani mkubali msikubali, ipo haja ya kusoma alama za nyakati. CCM kila siku tunasema hawajui kusoma alama za nyakati, ukweli ni kwamba wanajua tena sana kabisa.

Hawa wanazisoma. Sisi CDM tunatakiwa tu kuimarisha chama vijijini. Haya tunayasema. CCM nao wako macho wanajua CDM inataka kuwanyang'anya tonge, hawawezi kukubali kirahisi hivi. Miaka ilobaki ni miatu tu. Je tuko tayari kuingiza wabunge wengi bungeni huku nafasi ya raisi ikibaki na Magamba?

Mzaha mzaha utatumbua usaha soon! Vijana wengi wanajua Peoples Power maana yake maandamano na matumizi ya marungu, fimbo nk bila akili. Kumbe maana yake ni kwamba kwa mujibu wa Katika chokambaya ya Tanzania ibara ya 8, mamlaka ya nchi yako kwa wananchi wenyewe na serikali ipo kama msimamizi tu. Hapa haimanishi mimi Hossan naweza kumwambia ****** 'haloo unajua mimi ndio bosi wako, hifai bwana umekuwa mkwaree sana aisee' ujue utafungwa hadi segerea ibomoke. Dola imeshikwa na CCM na ndio maana hayo mamlaka ya wananchi hakuna, kama yapo iweje sasa kila siku ni kulalama tu vijiweni, upuuzi.
 
Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,636
Wewe utakuwa na tatizo.
Our reference point kwa sasa ni IGUNGA, Igunga ni Mjini? pale watu hawajui kusoma wala kuandika, hakuna umeme,
wanalala kwenye nyumba za manyata, wanapikia na kunywa maji wanayokunywa ng'ombe. CHADEMA wamepata asilimia
zaidi ya arobaini ya kura zilizopigwa, na hapo kadi za kupigia kura za wataka mageuzi nyingi tu zimenunuliwa. unataka
hawa watu wafanye nini cha kukulidhisha we mwana wa adamu. nyie ndio Magufuri anasema hamna shukurani.

CCM inakataliwa kila sehemu sasa, wewe unasema wako macho, wako macho wanafanya nini, wanakimbia people's power au?
sawa, wanambinu na wanakesha wakipanga mbinu zaidi, kwa ajili ya kuiba kura, kufanya kampeni hatarishi kwa amani ya nchi
yetu, kufisha muamuko wa mabadiriko ya kidemocrasia, kutoa rushwa, kutumia nguvu za dora nk.

Mbinu hizi haziwezi kudumu milele
 
Sawa mzee wa Sangara, miaka ile sisi tulikuwa tunasema 'Someni kwa Maarifa' sio kusoma tu ilimradi umalize aya. Busara ya mtu wakati mwingine ni kunyamaza tu na hasa kama jibu lako litakuwa linahisia. Kufanya reference point Igunga eti CDM ndio ijidai na ushindi huo mimi binafsi sikubali, labda nikuelimishe kidogo; huko Igunga CDM 'ilishindana na serikali' sio CCM ingawa na CDM ilipeleka karibu 'serikali yote' huko.

Tusiwe washabiki kwa kuegemea upande mmoja tu, CDM. Huo sio uzalendo mzee ni ulaghai tu, hata wewe unalijua hilo sema destiny ndio issue hapa. Kufanya mengi mniridhishe mie hakusaidii CDM iwe chama - dola 2015, tunachosema ni kwamba tunahitaji kuona na kusimia mabadiliko ya siasa vijijini kaka. We baki ukisema Igunga ni kijijini na wanakunywa maji mamoja na ng'ombe wako halafu subiri wenzio wawape chumvi mabalozi wa nyumba kumi uone mweleka wa 2015, unadhani CCM ni wapumbavu kiasi hicho. Lazima CDM iwe macho na ifanye vitu ambavyo hata 'hata kipofu' aone. Acha jazba na majibu mepesi kwa hoja nzito kaka.

Tanzania ina 80% ya wakulima ambao wanakunywa maji wanayokunywa ng'ombe wao, hawa wengi wao hawajui hata kusoma wala kuandika, sasa ni juu ya CDM kuwa na mbinu za kuwadaka na hawa, sio kuwa na jazba bila kutumia akili kaka. Sisi wote ni wanamapinduzi na tunajitahidi kuandika haya ili kwa bahati mbaya viongozi wa CDM wakiyaona yanajirudiarudia basi washtuke na hili ndilo lengo la kuamsha topiki za ushindi wa CDM 2015 ujue hilo.

Wewe kutetea CDM hata natural justice inakupinga mzee. Ujue mwalimu mzuri ni yule asiyemwambia mwanafunzi wake 'umefanya vizuri nenda kacheze chandimu - mpira' utamsikia mwalimu makini anasema 'vizuri Hossam, ongeza bidii'. Kwa CDM kufanya operation Sangara tunasema bravo kwa sababu sasa mageuzi yanakaribia, ila kivipi 80% CDM isifanye bravo? Unadhani ni rahisi kuwafikia watu zaidi ya 40million kwa miaka 3 halafu uwape elimu wakuelewe? CCM wengi wa vijijini wanasema 'Hiki chama kimetulea' hii ni kwa sababu wana mtandao hadi mitaani huko bush na sio sisi ofisi tu ya CDM huko Kawe kwa Halima Mdee inakuwa tabu, sembuse kibondo vijijini?

Acha hasira na kukurupuka ndugu yangu, hadi tunaandika haya ni kwamba tunayaona na yanatuuma mzee! Kama CDM hatuko tayari basi ni heri tuwaachie nchi magamba! Sasa leo hebu niambie kuna program gani vijijini ya CD?
 
STIDE

JF-Expert Member
Sep 1, 2011
997
349
Wewe utakuwa na tatizo. Our reference point kwa sasa ni IGUNGA, Igunga ni Mjini? pale watu hawajui kusoma wala kuandika, hakuna umeme, wanalala kwenye nyumba za manyata, wanapikia na kunywa maji wanayokunywa ng'ombe. CHADEMA wamepata asilimia zaidi ya arobaini ya kura zilizopigwa, na hapo kadi za kupigia kura za wataka mageuzi nyingi tu zimenunuliwa. unataka hawa watu wafanye nini cha kukulidhisha we mwana wa adamu. nyie ndio Magufuri anasema hamna shukurani. CCM inakataliwa kila sehemu sasa, wewe unasema wako macho, wako macho wanafanya nini, wanakimbia people's power au? sawa, wanambinu na wanakesha wakipanga mbinu zaidi, kwa ajili ya kuiba kura, kufanya kampeni hatarishi kwa amani ya nchi yetu, kufisha muamuko wa mabadiriko ya kidemocrasia, kutoa rushwa, kutumia nguvu za dora nk. Mbinu hizi haziwezi kudumu milele
Mkuu mimi niko tofauti kidogo na wewe, unajua ktk mapinduzi ambayo mimi na wewe tunayahitaji yanatakiwa yasiwe na shaka, yaani hata wakiiba zisitoshe! Na pia ndugu nakuomba ukubaliane na Hossam kuwa nguvu nyingi, thabiti na ya uhakika bado inahitajika vijijini, watu bado wamelala! Ni dhahiri kabisa kwamba mtaji mkubwa wa ccm uko vijijini, tunatakiwa kuhakikisha mtaji huo tunaufilisi kwa kasi kabla ya 2015!! "Go on CDM".
 
Mrx

Member
Feb 6, 2011
22
7
nakupongeza Hossam mtoa hoja. Ila hapa naomba niseme haya. Sisi watanzani ni vigeugeu . Isitoshe upeo wetu wa kufikiria ni mdogo sana. Mtu anatoa mawazo mazuri ya kuasaidia anatokea mwengine anaponda mawazo yale kwa ubabe. Badala kupinga kwa hoja inayoeleweka. Daima 2 tabaki kuwa watumwa kwa kuwa tumeweka mbele maslahi binafsi. Badala ya maslahi ya taifa kwa ujumla. "Tafakari"
 
Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,636
Hossam.
naona tunatofautiana approach 100%. style yangu ni kufocus kwenye kile nachoweza kukifanya
kwa ufanisi, basi, weaknesses zangu naweka pembeni.

CHADEMA wamefanya namna hiyo pia, wametarget vijana (kwa kutumia lugha na maelezo wanayoyaelewa)
sababu kwa swala la matatizo yanayotukabili hayachagui vijana pekee, ni jamii nzima.

Kuna mtu anaitwa FUSO, (Namchukulia ni kichwa zaidi yako wewe Hossam) kaeleza vyema, kwamba mtaji wa
ccm umebaki kuwa wanawake, labda hapa tunaweza kuongea kwamba CHADEMA watumie mbinu gani kuwafumbua
macho wanawake wa kitanzania na sio kulalamika tu, ccm wana mbinu ccm wana mbinu, mbinu zipi, hauelezi, badala
yake una andika andika tu, na kukimbilia kusontea wenzako kidole kwamba wana jazba na majibu mapesi.

Mwisho wake unabaki kujicontradict na hoja zako mwenye, unadai unanielimisha kidogo kwa kusema "HUKO IGUNGA
CHADEMA ILISHINDANA NA SERIKALI SIO CCM INGAWA CHADEMA ILIPELEKA SERIKALI YOTE HUKO" so what?
Unataka CHADEMA wakabiliane vipi na mkakati wa CCM kutumia serikali kwenye kampeni? kuwa wazi kaka, waombe
msaada NATO? au?

Haya, unaendelea oooh! tusiwe mashabiki kuegemea upande mmoja, Huo sio uzalendo. what a point? kuna pande
ngapi katika hili tunalolizungumzia. ONLY TWO. how can you be on both sides, unataka niwe sitaki nataka. unataka
niwe vuguvugu?.

unacomplicate mada kwa kutoa maelezo yasiyoeleweka kabisa, kwamba, "tunachotaka ni kuona na kusikia mabadiliko
ya kisiasa vijijini" hapo ni baada ya kusema "Kufanya mengi mniridhishe mie hakusaidii CDM iwe chama - dola 2015"
anyway, labda mi ni shallow kweli kweli, lakini hapa haueleweki unasimamia nini, Hakuna Mabadiliko ya kisiasa tunayoyataka,
zaidi ya yale yanayowawezesha wananchi kuchagua na kuwa na viongozi wa kisiasa wanaowataka wao, kwa manufaa
yao. Tanzania kuna utitiri wa vyama vya siasa, katika vyama vya upinzani vyoote kimebaki kimoja tu cha kuaminika,
CHADEMA, labda kama unataka kunirudisha nyuma kuangalia kama CUF, SAU, UDP, NSSF nao wamo.

Zaidi ya hapo mabadiliko halisi ya kisiasa ni kuwa na mfumo huru wa uchaguzi na usimamizi wa rasilimali zetu, haya mambo
mjini hayapo, hivyo sitegemei uwe unamaanisha kwamba ndio unataka yapatikane vijijini.

Unaandika in a very vague way, alafu unategemea watu tukusome na tukuache tu, Kwamba "Tanzania ina 80% ya
wakulima ambao wanakunywa maji wanayokunywa ng'ombe wao, hawa wengi wao hawajui hata kusoma wala kuandika,
sasa ni juu ya CDM kuwa na mbinu za kuwadaka na hawa, sio kuwa na jazba bila kutumia akili kaka" unaona,
mbinu zipi, toa mbinu ambazo unataka wazitumie zaidi ya ambazo wamezitumia, zipi? unasema CHADEMA
wamepeleka serikali yao yote Igunga, kweli kabisa, maana yake ni kwamba wametumia kila aina ya mbinu ambayo
mwenyezi mungu kawajaalia katika kuhakikisha kwamba wana Igunga wanakombolewa, wametumia role models, japo
kwa kuonekana tu jukwaani, kina sugu, zitto, slaa, mbowe, wewe umewaita serikali, wote wameenda kule kuuza sura,
wametumia takwimu zote walizonazo kutoka serikalini na kwenye sources nyingine kuwaonyesha wanaigunga
jinsi ambavyo wanaendeshwa na serikali dhaifu, wamechanganua umasikini wao hata baada ya miaka 50
ya uhuru ukilinganisha na utajiri unaowazunguka, chadema wamewafundisha mpaka jinsi ya kusimamia sheria
wanaigunga kwa kumuadabisha bi fatuma, wametumia kila aina ya mbinu, ni sawa na kusema wametumia
uwezo wao woote.

wewe unakuja unasema watafute mbinu za kudaka watu, jamani, wawadakeje, au unataka na wao, waanze
kugawa wali na kununua vitambulisho.

Nikuulize swali.
Kesho asubuhi DR SLAA akiamuka na kututangazia kwamba mwili wake umekuwa ukishambuliwa
na maradhi kwa muda anaamua kupumzika na hivyo hatashiriki katika active
field politics na hataweza kukitumikia chama katika nafasi ya ukatibu mkuu na hata mpango wake
wa kugombea upresdaa 2015 hauwezekani tena.

wewe utasemaje juu yake
(a) hakufanikiwa kabisa katika kukitangaza chama vijijini?
(b) tunamshukuru sana kwa mchango wake ambapo mpaka sasa amelifikisha taifa katika
mabadiliko ya kisiasa kitaka kiwango cha kuridhisha sana.
 
Fasta fasta

JF-Expert Member
Feb 15, 2011
1,014
613
Kumtambua adui yako ni 50% ya kumshinda, kutambua mbinu ya adui yako ni 75% ya kushinda na ilobaki ni juhudi ili ufanikishe ushindi wako. CDM isikae ikajidanganya na Peoples Power bila kuwa na mbinu za kuitunza na kuiongoza nguvu hiyo. Imani yangu ni kwamba CDM ishaeleweka sana mijini ila vijijini hawajui huyo ndio mnyama gani mkubali msikubali, ipo haja ya kusoma alama za nyakati. CCM kila siku tunasema hawajui kusoma alama za nyakati, ukweli ni kwamba wanajua tena sana kabisa.

Hawa wanazisoma. Sisi CDM tunatakiwa tu kuimarisha chama vijijini. Haya tunayasema. CCM nao wako macho wanajua CDM inataka kuwanyang'anya tonge, hawawezi kukubali kirahisi hivi. Miaka ilobaki ni miatu tu. Je tuko tayari kuingiza wabunge wengi bungeni huku nafasi ya raisi ikibaki na Magamba?

Mzaha mzaha utatumbua usaha soon! Vijana wengi wanajua Peoples Power maana yake maandamano na matumizi ya marungu, fimbo nk bila akili. Kumbe maana yake ni kwamba kwa mujibu wa Katika chokambaya ya Tanzania ibara ya 8, mamlaka ya nchi yako kwa wananchi wenyewe na serikali ipo kama msimamizi tu. Hapa haimanishi mimi Hossan naweza kumwambia ****** 'haloo unajua mimi ndio bosi wako, hifai bwana umekuwa mkwaree sana aisee' ujue utafungwa hadi segerea ibomoke. Dola imeshikwa na CCM na ndio maana hayo mamlaka ya wananchi hakuna, kama yapo iweje sasa kila siku ni kulalama tu vijiweni, upuuzi.

Tatizo sio vijijini tatizo litakalo wakwamisha CDM ni tume ya uchaguzi na katiba. CDM wanatakiwa wajipange kwa nguvu zote kuitafuta katiba ipatikane kabla hata 2013. Lingine wanalotakiwa kulifutilia kwa karibu sana ni tume ya uchaguzi ikiwezekana walitoe nje ya tanzania ili kamati iundwa ya haki bila kuelemea upanda mmoja.

Yaliyotokea hapo Igunga ni mambo ya kipumbavu kabisa ninawaomba CDM mjipange wakati wabunge wanahudumia wananchi. Wekeni mawakili wenye uwezo wa kusoma nyakati. Watu wanakata tamaa ya kupiga kura kwa sababu CCM walisha zoea kutangaza matokeo wanavyotaka wao.Wajitahidi kubadilisha hapo kwenye tume muone kichapo watakachochapwa CCM. Na tume ya uchaguzi ikiwa na watu wenaojali maadili kampeni zitapigwa kwa kufuata sheria.
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Wewe utakuwa na tatizo.
Our reference point kwa sasa ni IGUNGA, Igunga ni Mjini? pale watu hawajui kusoma wala kuandika, hakuna umeme,
wanalala kwenye nyumba za manyata, wanapikia na kunywa maji wanayokunywa ng'ombe. CHADEMA wamepata asilimia
zaidi ya arobaini ya kura zilizopigwa, na hapo kadi za kupigia kura za wataka mageuzi nyingi tu zimenunuliwa. unataka
hawa watu wafanye nini cha kukulidhisha we mwana wa adamu. nyie ndio Magufuri anasema hamna shukurani.

CCM inakataliwa kila sehemu sasa, wewe unasema wako macho, wako macho wanafanya nini, wanakimbia people's power au?
sawa, wanambinu na wanakesha wakipanga mbinu zaidi, kwa ajili ya kuiba kura, kufanya kampeni hatarishi kwa amani ya nchi
yetu, kufisha muamuko wa mabadiriko ya kidemocrasia, kutoa rushwa, kutumia nguvu za dora nk.

Mbinu hizi haziwezi kudumu milele

Sangara Sangara sangara umenigusa leo maneno yako mazito .Uzito wa maneno haya ni kilo nzito za Chuma cha pua lakini pia mtoa mada asikilizwe .Kuna mikoa kama Tanga , Lindi na Mtwara huko bado sanaaaaaaaaa kuanzia mjini hadi kijijini.
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,631
8,443
Guys

KUna ujumbe mzito sana from Hossam, we can choose to ignore or otherwise

To me, there is always to learn badala ya kukaa kujibu kila shambulizi

tuna masikio mawili na mdomo mmoja ili tuweze kusikiliza twice as much as we speak

the onus is on ..........
 
Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,836
1,164
This message has been deleted by Invisible
Reason: Imetoa siri ya Kikwete kuoana na Mama Salma
 
Hossam

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
3,399
1,857
Hossam.
naona tunatofautiana approach 100%. style yangu ni kufocus kwenye kile nachoweza kukifanya
kwa ufanisi, basi, weaknesses zangu naweka pembeni.

CHADEMA wamefanya namna hiyo pia, wametarget vijana (kwa kutumia lugha na maelezo wanayoyaelewa)
sababu kwa swala la matatizo yanayotukabili hayachagui vijana pekee, ni jamii nzima.

Kuna mtu anaitwa FUSO, (Namchukulia ni kichwa zaidi yako wewe Hossam) kaeleza vyema, kwamba mtaji wa
ccm umebaki kuwa wanawake, labda hapa tunaweza kuongea kwamba CHADEMA watumie mbinu gani kuwafumbua
macho wanawake wa kitanzania na sio kulalamika tu, ccm wana mbinu ccm wana mbinu, mbinu zipi, hauelezi, badala
yake una andika andika tu, na kukimbilia kusontea wenzako kidole kwamba wana jazba na majibu mapesi.

Mwisho wake unabaki kujicontradict na hoja zako mwenye, unadai unanielimisha kidogo kwa kusema "HUKO IGUNGA
CHADEMA ILISHINDANA NA SERIKALI SIO CCM INGAWA CHADEMA ILIPELEKA SERIKALI YOTE HUKO" so what?
Unataka CHADEMA wakabiliane vipi na mkakati wa CCM kutumia serikali kwenye kampeni? kuwa wazi kaka, waombe
msaada NATO? au?

Haya, unaendelea oooh! tusiwe mashabiki kuegemea upande mmoja, Huo sio uzalendo. what a point? kuna pande
ngapi katika hili tunalolizungumzia. ONLY TWO. how can you be on both sides, unataka niwe sitaki nataka. unataka
niwe vuguvugu?.

unacomplicate mada kwa kutoa maelezo yasiyoeleweka kabisa, kwamba, "tunachotaka ni kuona na kusikia mabadiliko
ya kisiasa vijijini" hapo ni baada ya kusema "Kufanya mengi mniridhishe mie hakusaidii CDM iwe chama - dola 2015"
anyway, labda mi ni shallow kweli kweli, lakini hapa haueleweki unasimamia nini, Hakuna Mabadiliko ya kisiasa tunayoyataka,
zaidi ya yale yanayowawezesha wananchi kuchagua na kuwa na viongozi wa kisiasa wanaowataka wao, kwa manufaa
yao. Tanzania kuna utitiri wa vyama vya siasa, katika vyama vya upinzani vyoote kimebaki kimoja tu cha kuaminika,
CHADEMA, labda kama unataka kunirudisha nyuma kuangalia kama CUF, SAU, UDP, NSSF nao wamo.

Zaidi ya hapo mabadiliko halisi ya kisiasa ni kuwa na mfumo huru wa uchaguzi na usimamizi wa rasilimali zetu, haya mambo
mjini hayapo, hivyo sitegemei uwe unamaanisha kwamba ndio unataka yapatikane vijijini.

Unaandika in a very vague way, alafu unategemea watu tukusome na tukuache tu, Kwamba "Tanzania ina 80% ya
wakulima ambao wanakunywa maji wanayokunywa ng'ombe wao, hawa wengi wao hawajui hata kusoma wala kuandika,
sasa ni juu ya CDM kuwa na mbinu za kuwadaka na hawa, sio kuwa na jazba bila kutumia akili kaka" unaona,
mbinu zipi, toa mbinu ambazo unataka wazitumie zaidi ya ambazo wamezitumia, zipi? unasema CHADEMA
wamepeleka serikali yao yote Igunga, kweli kabisa, maana yake ni kwamba wametumia kila aina ya mbinu ambayo
mwenyezi mungu kawajaalia katika kuhakikisha kwamba wana Igunga wanakombolewa, wametumia role models, japo
kwa kuonekana tu jukwaani, kina sugu, zitto, slaa, mbowe, wewe umewaita serikali, wote wameenda kule kuuza sura,
wametumia takwimu zote walizonazo kutoka serikalini na kwenye sources nyingine kuwaonyesha wanaigunga
jinsi ambavyo wanaendeshwa na serikali dhaifu, wamechanganua umasikini wao hata baada ya miaka 50
ya uhuru ukilinganisha na utajiri unaowazunguka, chadema wamewafundisha mpaka jinsi ya kusimamia sheria
wanaigunga kwa kumuadabisha bi fatuma, wametumia kila aina ya mbinu, ni sawa na kusema wametumia
uwezo wao woote.

wewe unakuja unasema watafute mbinu za kudaka watu, jamani, wawadakeje, au unataka na wao, waanze
kugawa wali na kununua vitambulisho.

Nikuulize swali.
Kesho asubuhi DR SLAA akiamuka na kututangazia kwamba mwili wake umekuwa ukishambuliwa
na maradhi kwa muda anaamua kupumzika na hivyo hatashiriki katika active
field politics na hataweza kukitumikia chama katika nafasi ya ukatibu mkuu na hata mpango wake
wa kugombea upresdaa 2015 hauwezekani tena.

wewe utasemaje juu yake
(a) hakufanikiwa kabisa katika kukitangaza chama vijijini?
(b) tunamshukuru sana kwa mchango wake ambapo mpaka sasa amelifikisha taifa katika
mabadiliko ya kisiasa kitaka kiwango cha kuridhisha sana.

Sangara.
Ni kweli mkuu tunatofautiana sana kimtazamo lakini ni jukumu langu kukurekebisha maana naona unaanza kuelewa somo yakhe.
CDM kutageti vijana kwenye siasa zao sio vibaya kwa kuwa vijana haimanishi ndio wao pekee wataka mabadiliko nchini hata na wazee wanayataka pia ili wazeeke vema na walipwe NSSF zao bila usumbufu kama ule wa iliyokuwa EAC. Hilo kaka ndio nimesema kwa mjini limefanikiwa, sasa vipi vijijini ambako, labda nikutoe matongotongo sasa, huko ndio CCM wanasema wanao mtaji wao, sasa kwa CDM kuwavurumusha huko CCM watakosa pa kusema wana mhimili, hivyo ndivyo kama ungesoma katikati ya mistari yangu ungegundua maudhui hii ngumu mzee wangu. Mtazamo is nothing to this.

Ona kaka, FUSO kusema CCM mtaji wao ni wanawake halafu na wewe na mvi zako unamsifia umeniskitisha sana, usije kudandia treni kwa mbele, FUSO anakuchota tu ukimsoma vizuri, huyu anatafuta mawazo ya wana JF kuhusiana na kauli za CCM kule Igunga, kumbuka na wao CCM wanafanya tathmini in the meantime, na kaa ukijua uchangiaji mzuri wa mada huonyesha bidii ya mtu kusaka mawazo kwa watu wengi, FUSO hana kichwa kuliko mimi. Sasa kama mtaji wa CCM ni kina mama, mbona jumuiya yao sasa hivi haieleweki na lakini bado CDM haipati nafuu hapo. Ina maana wanawake ndio wana muamko sana na siasa, kaka umeshikwa pabaya naona. Hao 80% wa vijijini wengi wanaohenya kulima na kukamua ng'ombe ni kina mama huku akina baba na watoto wao wakiishia kuoa wanawake lukuki na ulevi kila siku.

Hakuna hata sehemu moja nilipokontradiki hoja zangu ila kwa sababu ya kukurupuka kwako unaona kama nimefanya hivyo. Niliposema CCM walipeleka serikali yao nilimaanisha walimpeleka kila walieona anawafaa kuanzia wa chama chao hadi wa chama-dola-kada wao. Wengine walipanda majukwaani kusema watajenga madaraja mara punda na Lipumba wa CUF ilimradi ni hoja dhaifu zisizo mashiko hata kidogo. Nilisema baada ya CCM kufanya hivyo, na CDM nao walipeleka shehena yao na models ili watu wanaowaonaga kwenye TV sasa walikuwa na fursa ya kushikana nao mikono halafu wanakimbilia ubwabwa wa CCM. Maana yangu kulinganisha 'serikali' hizi mbili haikuwa kuwabeza CDM kwa mbinu zote, ila ilikuwa ni katika kuonyesha ugumu ulivyo pindi unapokosa wazalendo wanaokukubali bila shaka. Hapo ndio nasema kaka sizioni busara zako, unakurupuka sana, jaribu kusoma katikati ya mistari, soma kwa maarifa. CDM ilivyokabiliana na CCM huko Igunga imetoa funzo kwamba hivyo ndivyo inatakiwa kusambaa kwa wamanchi masikini milioni 40 kuanzia leo. Watu wahamasike kama ilivyokuwa Igunga. uwage unaelewa mzee wangu.

NATO ama huko unakosema nikaombe msaada, hawana interest na Tanzania kwa sababu you have absolutely nothing to offer them in return. Nchi iko hoi hadi viongozi wake wanahongwa suti! Hapo nakuona una kaukorofi kidogo. NATO kazi yao ni kupiga tu, so kama unawataka ama una wa admire aisee wewe sio muungwana, bomu la NATO ni Mtanzania gani atalihimili?

Uzalendo ninaoutaka kwako ni kusimamia hoja bila kujali nani atafurahi ama nani utamuudhi. Lakini ukishakuwa bias ujue hufai kasbisa. Huwezi kuja na mamisimamo na mafokasi yako ambayo hayaeleweki halafu unadai oohh sasa unataka niwe vuguvugu? Nani kakwambia hilo, ukiwa vuguvugu tunakufukuza CDM, jaribu uone. Mzalendo wa kweli ni yule anayetetea maslahi ya umma bila kujali msimamo wake kaka. Kama leo hii CCM wataleta unafuu kwa watanzania kwa mfano petroli lita moja ikawa TZS 800, sukari kilo ikarudia TZS 500, mkate ukawa TZS 250 kama zamani, nauli za mikoani kwa mfano Dar - Arusha ikawa TZS 4,000 moro ikawa TZS 1500 Kama zamani, na kadhalika; hapa unatakiwa kukipongeza CCM hata kama wewe ni mpinzani, upinzani maana yake ni kuleta hali tofauti na iliyopo katika kuweka mambo yawe rahisi.

Sifanyi hoja hii iwe ngumu kaka ila niliposema na mabadiliko ya siasa huko vijijini tuyaone maana yake ni kwamba nguvu kamili ya umma itaungana na hapo ndipo ukombozi utakuwa umewadia, 2015 sio mbali kama hali yenyewe ndio hii ujue hilo mapema. Kama wanakijiji watamka kama tulivyo akina sie, tutaona na tutawasaidia waelewe zaidi. Ni sawa kwamba CDM ndio chama pekee kimebaki Tanzania kama mkombozi, lakini unajua yaliyojiri huko NCCR and CUF? Tafakari.

Kuwadaka wale 80% vijijini ni sentensi ndefu na ni pana kuliko unavyodhani. Kuna mbinu nyingi; kwa mfano; Radio kwa vipindi vya elimu ya uraia, Matamasha yenye mwelekeo wa siasa kwa mfano 'piga kura okoa kijiji chako' tamasha kubwa huko Kibondo vijijini watu waelimishwe, kufungua ofisi vijijini kabisa, kushiriki huduma za jamii kama kununua madawa kwa vituo vya afya vijijini, kuchangia madawati mashuleni ambako watoto wetu wanakaa chini huko Kibondo vijijini, yapo mengi ila mwenzangu sijui umelogwa na nani, kwa kufanya haya utawadaka woooote watajua kweli mkombozi kaja. Kuchanganua tu umaskini baada ya miaka 50 ya uhuru hakutoshi kwa kuwa vijana wengi waliokuwepo enzi kabla ya uhuru na miaka michache baada ya uhuru washakufa, vijana hata ungechambua vipi hawakuelewi, na zaidi huko vijijini ndio kabisaaa, kwa sababu toka enzi za ukoloni babu alikuwa analima mahindi huko Kibondo, mwanae akarithi na analima mahindi sasa, akafa akarithi mjukuu nae alima mahindi yaleyale na wanakula ugali kama kawaida, hawa ukiwaambia uhuru wetu hauna maana wataishia kukucheka wewe ukadhani wanakushangilia, waambie hivi, kuna maisha baada ya kilimo hapo watakuwa na shauku ya kutaka kuyajua hayo maisha yakoje, changanya akili aisee.

Kama ikitokea Dr Slaa akafa mimi nitasema CDM na Watanzania tumepoteza mwanamapinduzi daima tutamkumbuka kwa aliyoyafanya. Maana yake alikuwa akitimiza wajibu wake, kama asingefanya angefukuzwa kama Mrema au yule Mbatia alivyo, kama angefanya kwa kusuasua basi angetapikwa awe kama Dovutwa anayejifanya Che Guavara, nchi hii ina vituko aisee.

Msheshimiwa, napenda kutoa hoja.
 
Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,636
Noted Hossam: lakini naomba unisome kwamba CHADEMA hawahitaji kutumia style za CCM kujitangaza labda
kama wanataka kujimaliza.
 
Hossam

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
3,399
1,857
Noted Hossam: lakini naomba unisome kwamba CHADEMA hawahitaji kutumia style za CCM kujitangaza labda
kama wanataka kujimaliza.

Asante Mkuu kwa kufikia tamati, jasho limenitoka lakini Mungu atatusaidia tu. CDM inaaminiwa, sasa ni jukumu lao kujua nguvu kuu iliyo nyuma yao, na kamwe wasiichezee. Asalam Aleykum!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom