CHADEMA, kwa mwendo huu 2015 patupu!

CHADEMA, kwa mwendo huu 2015 patupu!

Huyu SELASINI inasemekana ni mzee wa kanisa moja hapa Dar es salaam, sasa sijui kama alikuwa anaongea kama Mchungani au Mbunge? Lakini pia ni mtu wa kusifiwa kama mleta mada ulivyosema kwa sababu hii kasi ya akina LEMA, MSIGWA na WENJE kuongelea udini siyo ya kawaida inaonekana wamejipanga kui hide ili kukilinda chama na aibu, lakini itakuwa vigumu kwa vile hata viongozi wa dini makanisani wamekuwa wakikipigia ndogondogo tena hadharani.
nyinyi na maudini yenu sijui mtahamia chama kipi ccm wakimsimamisha mkristo kugombea urais 2015!!
 
yani mtu aone tatizo alinyamazie,mficha maradhi kifo humuumbua,nyinyi mna matattizo gani?

umesema kweli lakini katika hili la CHADEMA na hoja ya udini inaonekana kabisa limewagusa na jinsi walivyojipanga kulimaliza ndiyo tatizo tena, tatizo shule, MBOWE hawezi kuwa na uelewa wa namna ya kuwafunda wabunge wake waweze kujinasua kisomi.
 
ikitucost si ndo furaha yenu ili 2015 iwe mteremko kwenu?? Huruma juu ya cdm inatoka wapi km si unafki??

Huruma yangu sio kwa Chadema , huruma yangu kwa mwananchi wa kawaida ambaye ameshaweka imani kwa Chadema halafu anakutana na habari za namna hii.
 
eti huyu utakuta ni mbunge au waziri tegemeo la ccm anakuja na huu ushuzi kwa ID fake!hebu tuondolee takataka.

Nyabhingi, siyo kwa vile unalipwa na cdm basi kila mtu atakayeandika kinyume unampinga. kuna hoja ya msingi hapo. wengi tumenufaika, kuwa selasini kumbe alikataa kusaini wakati anakabidhi zile cd kwa kuhofia kuwa zikigundulika ni za kughushi yeye ndiye atakayewajibika
 
Chadema wamejiweka pabaya sana kwa jamii ya Kiislam tasfri ya udini kwao mtu kuwa Muislam.
mtashindana lakini mtashindwa,jiandaeni kuhamia chausta ccm wakimpitisha mkristo kwenye urais,wadini sana nyie.
 
Mkuu unajua hiki chama kimejipanga kwenye vikao vyao vya ndani kuhakikisha hoja ya udini haikiathiri chama, lakini sasa hawakuwapa semina wabunge wao namna ya kutoa hoja zao matokeo yake ndo kila mmoja analipuka na lake na kama unavyojua unapotaka kujitoa katika jambo ambalo ni la kweli usipojipanga lazima uumbuke, tusubiri tu tuone CHADEMA siyo siri sasa itathibitika na chama cha kidini, angalia hata viongozi wa dini wanavyotimika nao wanaropoka hovyo.

hata kama wamepata semina kwa vile wanapata pia maelekezo kutoka kwa viongozi wa kidini ndo maana tunashuhudia watu kama akina selasini. pale yeye alisimama kama mbunge lakini pia kama kiongozi wa dini. selasini ni miongoni mwa wazee wa kanisa moja pale pugu
 
Huo aliotoa ndio msimamo wa CDM wala usihangaike kuwaza,hiki ni chama cha kikatoliki 100% usisahau MTEI waislam wengi kwenye tume ya katiba unadhani alikusudia nini?
Hapa watakushambulia kwa kejeli matusi na kashfa lakini jibu litapatikana 2015 mungu tupe uhai,

Kwa sisi tusio na vyama kiukweli hii CDM inatupa shida sana tena sana hasa ktk masuala haya ya dini ya Kiislam na mitazamo yao. Sehemu yyt ya kazi kiongozi wake akiwa Mwislam wanasema kuna udini ss je kwa hili CDM ina maana ni chama chat kabisa au kipo kutetea maslahi ya Wakristo tu? Bahati mbaya iliyoje members wake hapa Jf badala ya kujibu hoja wanakuja na matusi, dharau, kero ambazo hazijengi bali zinaharibu taswira nzima ya chama! Mfano mwingine halisi WANASEMA RAIS J.M KIKWETE MDINI ss maswali haya ukiwauliza sidhani kama utapata jibu zaidi ya kashfa: Maswali hayo ni:
1. Nini maana ya kusema mtu mdini?
2. Vigezo vipi vinavyothibitisha mtu ni mdini?
3. Ushahidi gani unaothibitisha mtuhumiwa ni mdini?
4. Je kama ni mdini na una concrete evidence kwa nn usimshtaki sehemu husika?
5. Kwa nini ofisi au nafasi anayoshika Mwislam tu ndo kuna udini na Si dini nyingine?
 
Huyu jamaaangu amejileta mwenyewe kwani ni wale jamaa tuliokuwa tunawatafuta wa Kungoa, meno, kope na kukata kucha na kung'oa meno. Hata staili aliyoingia nayo inatufanya tubaki na maswali
 
Mleta mada inaonesha umejaa udini na tena uislam badala ya utaifa.
 
mambo ya udini ni mapya hapa nchini na kuna chama ambacho ni kipya, tujiulize kwanini leo??
 
mtashindana lakini mtashindwa,jiandaeni kuhamia chausta ccm wakimpitisha mkristo kwenye urais,wadini sana nyie.

CCM haina tatizo la udini katika kusimamisha wagombea. walianza na nyerere (mkristo), wakaja na Mwinyi (muislam), akafuatia Mkapa (mkristo) na mwisho Kikwete (muislam). yaani huku wawili na kule wawili. hawa wote kumbuka ndio waliokuwa wenyeviti wa CCM. haya tueleze CHADEMA tangu kimeanzishwa ni muislam gani amewahi kuwa mwenyekiti au katibu mkuu wa chama?
 
Nyabhingi, siyo kwa vile unalipwa na cdm basi kila mtu atakayeandika kinyume unampinga. kuna hoja ya msingi hapo. wengi tumenufaika, kuwa selasini kumbe alikataa kusaini wakati anakabidhi zile cd kwa kuhofia kuwa zikigundulika ni za kughushi yeye ndiye atakayewajibika

it's ok kwako kusema nalipwa lakini mtu anafichua uovu,badala ya kuchunguza nyinyi mnam-condemn yeye and bad enough mnakiingiza na chama,huu sio upuuzi na udini?
 
Kwa sisi tusio na vyama kiukweli hii CDM inatupa shida sana tena sana hasa ktk masuala haya ya dini ya Kiislam na mitazamo yao. Sehemu yyt ya kazi kiongozi wake akiwa Mwislam wanasema kuna udini ss je kwa hili CDM ina maana ni chama chat kabisa au kipo kutetea maslahi ya Wakristo tu? Bahati mbaya iliyoje members wake hapa Jf badala ya kujibu hoja wanakuja na matusi, dharau, kero ambazo hazijengi bali zinaharibu taswira nzima ya chama! Mfano mwingine halisi WANASEMA RAIS J.M KIKWETE MDINI ss maswali haya ukiwauliza sidhani kama utapata jibu zaidi ya kashfa: Maswali hayo ni:
1. Nini maana ya kusema mtu mdini?
2. Vigezo vipi vinavyothibitisha mtu ni mdini?
3. Ushahidi gani unaothibitisha mtuhumiwa ni mdini?
4. Je kama ni mdini na una concrete evidence kwa nn usimshtaki sehemu husika?
5. Kwa nini ofisi au nafasi anayoshika Mwislam tu ndo kuna udini na Si dini nyingine?

Siku za mwizi ni arobaini mkuu, wamejaribu ku-preempty hoja ya udini na kuwabambikiza CCM kuwa wao ndiyo wadini, Mungu siyo athumani bwana yameanza kuwarudi weneywe sasa wanafyatuka tu kwenye majukwaa, bungeni na mwishoe watajitokeza na kusema wapi walikaaa na nani aliandaa mkakati huo wa kuimba habari za udini.
 
mambo ya udini ni mapya hapa nchini na kuna chama ambacho ni kipya, tujiulize kwanini leo??

chama kipya kinakuja na mambo mapya. hayo mambo yanaweza kuwa mazuri au mabaya. kuibuka kwa suala la udini sasa ni wazi kuwa chama kimekuja na mambo mabaya na kwa hiyo chama hicho ni kibaya na hakifai kuwaongoza watanzania
 
CCM haina tatizo la udini katika kusimamisha wagombea. walianza na nyerere (mkristo), wakaja na Mwinyi (muislam), akafuatia Mkapa (mkristo) na mwisho Kikwete (muislam). yaani huku wawili na kule wawili. hawa wote kumbuka ndio waliokuwa wenyeviti wa CCM. haya tueleze CHADEMA tangu kimeanzishwa ni muislam gani amewahi kuwa mwenyekiti au katibu mkuu wa chama?
kwenye red that's holy c.r.ap indeed,yani ccm wanapokezana urais kwa kigezo cha zamu ya dini!
hatutamchagua mtu sababu ya dini yake na hatutaacha kumchagua mtu sababu ya dini yake-jk nyerere
no wonder mmetupa rais jk kikwete.
 
it's ok kwako kusema nalipwa lakini mtu anafichua uovu,badala ya kuchunguza nyinyi mnam-condemn yeye and bad enough mnakiingiza na chama,huu sio upuuzi na udini?

ulipaswa kumsaidia selasini kuondokana na aibu aliyoipata kwa kutueleza ukweli kuhusu zile cd. naona cdm ni hodari sana wa kuandaa cd feki ila mnaumbuliwa kwa cd genuine. selasini angekuwa jasiri angekubali matokeo kwa kusaini kama alivyofanya nchemba kusema kuwa yupo tayari kusema ukweli iwe bungeni, polisi, mahakamani au hata mbinguni
 
Nimemsikiliza Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (CHADEMA) na nahau zake bungeni, nimevutiwa na kauli aliyoitoa kwamba, Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuna udini. Katika matamshi yake anasema, CD alizokuwa nazo zinaonesha namna UDOM kinavyoendeshwa kidini na kwamba kuna wahadhiri ambao wamekuwa wakiwakusanya wanafunzi na kuwapandikiza chuki dhidi ya dini nyingine. Amenukuliwa kwamba, baada ya wanafunzi hao kulishwa maneno ya chuki na wahadhiri hao wa dini fulani, wakahoji
huko nyumbani tunakaa na wanafunzi wa vyuo vingine, tuwafanyeje? Haya si maneno mepesi kama anavyodhani kwa kuwa, kama tumefikia hali hiyo basi tupo mashakani. Ni maneno yanayohitaji utafiti wa kina ili kujiridhisha ingawa yeye mwenyewe anatilia shaka kauli yake.

Makamu wa UDOM ni Prof. Idrisa Kikula ambaye kwa lugha nyepesi tunaweza kusema kwamba, ndiye Mtendaji Mkuu wa UDOM.
Selasini anasema, UDOM kuna udini na anashangaa sababu za polisi kushindwa kuchukua hatua, yeye hakwenda kutoa taarifa
polisi, hajapeleka ushahidi wake polisi na wala hakushughulishwa na walinzi wa amani nje ya bunge, amewapuuza. Amekimbilia bungeni na CD zake akiamini ataonekana ‘live’ na ujumbe wake utafika kwa aliyemkusudia na kuwaridhisha wale walio nyuma ya mchezo huo, kweli tumemuona na ujumbe wake umefika.

Pengine angeenda polisi huenda lile alililokusudia ama dhamira ya wale walio nyuma yake lisingekuwa na matokeo chanya kama alivyokusudia ama walivyokusudia jamaa zake. Amefanikiwa kumwaga machache yaliyo kwenye ulimi wake na kuhifadhi mengi moyoni
mwake. Huyu ni Selasini ndani ya CHADEMA.

Waliomwelewa vizuri Selasini huenda wakawa na mtazamo kama wangu kwamba, tafsiri yake isiyo sahihi ni kuwa, Mtendaji Mkuu
wa UDOM ni mdini ka kwa hivyo anaendesha chuo kidini na kwa kuwa ni Muislamu, maana yake anaendesha chuo Kiislamu. Pengine
Selasini aliona ugumu kutaja Uislamu lakini hakuna tafsiri tofauti na hiyo. Kwa mantiki hiyo, kilio cha Selasini na wale walio nyuma ya mchezo huo ni kutaka Prof. Idrisa awekwe kando kwa kuwa, anaendesha chuo hicho Kiislamu.

Pia kwa tafsiri ni kwamba, Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) kinachoongozwa na Makamu Mkuu wake Gerald Monela kipo salama. Hakina shaka kwa upande wake maana hajakituhumu. Chuo Kikuu cha Mzumbe kilicho chini ya Makamu Mwenyekiti wake Joseph Kuzilwa
kipo salama na hakuna tuhuma zozote za udini. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinachoongozwa na Prof. Mukandara nacho kimeepuka
tuhuma za udini sawia na vyuo vyote vya serikali.

Kwa sasa, kwa bahati mbaya, tuhuma za udini zipo kila sehemu yenye mikusanyiko ya watu wenye dini tofauti, zipo katika kila chuo, zipo sekondari kama ilivyotokea kwenye sekondari ya Bagamoyo na pia zipo Shule za Msingi. Karibu vyuo vyote vya serikali mambo haya yanalalamikiwa lakini kunyooshea chuo kimoja, hapa ndio Selasini alipoleta tafsiri mbaya kwa jamii. Selasini anakosea kitu kimoja, ni dharau kwamba, Watanzania hawawezi kutambua kilicho nyuma ya mpango wake na wale waliomtuma. Anajivika bomu la kutugawa, tena ndani ya muhimili wa dola: Bunge. Lakini pia anaanzisha vita ambayo itammaliza yeye mwenyewe pamoja na chama chake, vita ambayo mwenyekiti wake Freeman Mbowe amekuwa akipambana nayo kwa muda mrefu sasa, anajitahidi kubadilisha fikra za wale wanaoitazama CHADEMA kwa mtazamo hasi wa kidini.

Mbowe anatambua kwamba, wapo wanaoitafsiri CHADEMA kwa mtazamo ‘usio sahihi’. Anapambana na mtazamo huo kwenye
najukwaa na kwenye vikao vidogo lakini anaangushwa na watu kama akina Selasini. CHADEMA inateswa na mambo makuu manne
kwa sasa ikiwa ni pamoja na udini, ukanda, urafiki na mashambulizi kutoka vyama vingine. Inakabiliwa na mtihani mzito kutoka Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kilicho na vijana wake wengi ndani ya chama hicho, kinakabiliwa na Chama cha Wananchi (CUF) kutaka kurudi
katika nafasi yake hiyo, kinakabiliwa na changamoto kutoka NCCR-Mageuzi, lakini yote haya yanapuuzwa na Selasini. Selasini huenda
alionesha hayo nje ya bunge na kuona haitoshi, ameamua kusimama sehemu takatifu na kuwahakikishia walio tofauti na yeye kwamba, yeye ama chama chake kinaendesha mapambano dhidi ya watu wasio na imani yake.

Selasini anadhihirisha chuki yake ana ya chama chake dhidi ya watu walio tofauti na imani yake, Selasini anahitaji kusifiwa ama
kuitwa jasiri kwa kuwa, pale wenzake wanapoficha kauli zinazoashiria mpasuko, yeye anajipiga kifua na kutoka hadharani. Kama chama chake kitaendelea kukaa kimya kutokana na kauli zake zenye kuashiria mapasuko wa kidini, Selasini anaweza kutafsirika kuwa
mawazo yake ndio ya chama chake. Wakati mwingine ni dhambi kusema imani yake ndio chama chake lakini kwa jinsi wanavyopokezana kijiti na wenzake, napata shida kutoamini hivyo.

Selasini anakivuruga chama kwa kukataa kuwa tayari kwa lolote pale alipotakiwa kusaini kwamba, CD zile ni yeye aliyezikabidhi kwa
katibu wa Bunge. Bunge limeshindwa kupokea CD zake kutokana na yeye kutokuwa tayari kwa matokeo yoyote pale uchunguzi na
upembuzi yakinifu utakapofanywa kutokana na CD hizo. Naweza kutafsiri kwamba, Selasini alikuwa na malengo yake hasi ya kuvuruga
Watanzania wanaohaha katika vikao mbalimbali kuhakikisha wanatuliza upepo wa shetani unaovuma kwa sasa. Kwa bahati mbaya,
Selasini ni Mbunge, anasahau kwamba hata walio na imani tofauti na yeye walimchagua kuwa mbunge, anataka kuwadhiahaki kwamba, ni wapuuzi wasiojua walilolifanya.

Sina hakika kama Selasini atagombea tena na kupata kura ya wale anaowadharau, anaowaona hawana hadhi ya kuwa viongozi
wa taasisi kubwa, anaowatuhumu pasina ushahidi wa kweli tena mbele ya Watanzania.

Selasini anapaswa kukumbushwa kwamba, kauli zake na mifano yake anayotaka kuithibitishia jamii inamtesa Mbowe pamoja na Chama chake ambacho mpaka sasa hisia za baadhi ya watu ni hasi hasa kwa upande wa dini. Kauli zake sawia na za rafiki zake, Godbless Lema, Peter Msigwa, Wenje zitaitesa CHADEMA mbele ya safari, zinazidi kutia gazi kwa wale waliokuwa na taswira
hasi dhidi ya chama hicho. Bila shaka matokeo yake ni mwaka 2015.

Tusubiri.

Hivi CHADEMA bila SLAA na MBOWE haiwezekani? mbona naona kama wao ndiyo tatizo hivi sasa ndani ya chama, aidha wameshindwa kuwaandaa wabunge wao au wanafanya makusudi na kwa vile wanasimamia utekeleza wa udini nchini.
 
Mleta mada inaonesha umejaa udini na tena uislam badala ya utaifa.

yaani mtu akimkosoa selasini mnasema mdini. mbona nyie hamkumkemea pale selasini aliposema upuuzi wake bungeni
 
Back
Top Bottom