Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,212
Maandamano na vurugu zinazoendelea Mtwara zimetafsiriwa na baadhi ya viongozi wa serikali kama ni uhaini.
Na baadhi ya watu wamenidokeza kwamba kauli ya Mheshimiwa Nchimbi bungeni kwamba kuna baadhi ya vyama vya upinzani vipo nyuma ya vurugu hizi, ina madhumuni maalumu.
Kuna uwezekano mkubwa kwamba viongozi wa CCM wakayahusisha machafuko haya na CHADEMA, na kuitaka mahakama iamuru CHADEMA ifutwe kutokana na jaribio la uhaini.
Pamoja ya kwamba mimi siungi mkono kile kinachofanywa na wana Mtwara, lakini naamini chama changu CHADEMA kipo upande wa wananchi siku zote. Hata hivyo napendekeza kwamba kauli za kuunga mkono harakati za wana Mtwara, zitolewe kwa umakini mkubwa sana.
Ni angalizo tu!