Una maana gani unaposema usumbufu wa hapa na pale?. Kama usumbufu unaosema maana yake ni misukosuko basi sina budi kukushangaa kwa kauli yako hii.
CHADEMA kiliingia kwenye ulingo wa kisiasa kupambana ili kama kitafanikiwa, basi kiweze kushika madaraka. Sina shaka kabisa, waanzilishi wake walilifahamu hili from day one hata kabla ya kwenda kuchukua form ya usajiri wa muda.
Misukosuko inayoipata CHADEMA ni kitua ambacho hakiwezi kushangaza kwa wale wenye kujua mapambano ya kisiasa hasa kwa nchi zenye demokrasia changa, kwa vile hata katika nchi zilizotuletea hii demokrasia, mapambano ya kisiasa baina ya vyama vikuu huwa ni makali mpaka yanahusisha mud-slinging. Kwa Tanzania inaonekana ni kitu cha ajabu sana kwa vile hii ni mara ya kwanza kwa CCM kupata proper checks & balances katika utendaji wake kisiasa, kiuchumi na kijamii kutoka opposition party. Reaction kama hii ni nornal and natural kwa political shock ambazo vyama vyote vikuu vinaipata.
Usidanganyike kabisa kama CCM haijari madhara yatokanayo na negative reactions ya wananchi kwa matendo yao.
CCM kila mara wanajitathimini kisiasa na ndiyo maana wanafanya mabadiliko katika safu za uongozi kuanzia wajumbe wa nyumba kumi mpaka Taifa ili kujisimika katika nguzo ya kisiasa nchini.
Tatizo ninaloliona ndani ya CCM ni kuendelea kuwa na viongozi ambao mpaka sasa inawawia vigumu kuji-ADJUST na hali halisi ya kisiasa nchini. Kwa mfano, They used to get away with ill-advised comment or action na kibaya kabisa, they are prone to political gaffe. Kwa sasa hiki kitu hakikubaliki kwa sababu wananchi walio wengi kwa sasa nchini wanaweza kuchambua kila neno kwenye sentesi.
Kutokana na kuendelea kuwa na viongozi wa aina hii, inakifanya chama kuonekana kwa kiwango fulani kina mwelekeo au mtazamo hasi katika maswala muhimu kama ukanda, ukabila na udini kwenye macho ya wananchi. Kwa mfano, juzi tumesikia mbunge kupitia CCM akidai mitandao especially, JF idhibitiwe, utaona ni kwa kiasi gani kuna baadhi ya viongozi wasiojua dunia kwa sasa iko wapi.p na inakwenda wapi.