CHADEMA Kutumia 5bn/- tu Kwenye Uchaguzi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Kutumia 5bn/- tu Kwenye Uchaguzi!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Buchanan, May 2, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  May 2, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilbrod Slaa ameongea na waandishi wa habari kwamba chama chake kitatumia Tsh bil 5 tu na kuishinda CCM ambayo itatumia bil 50!
  SOURCE: TBC1.
   
 2. M

  Mundu JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  ...Good. Source ya hizo fedha ni nini?
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Bila shaka ataeleza. Kama kaweka wazi matumizi na source si ataeleza? Isitoshe sheria ndivyo yataka.

  Umefanya kuwahi kutawaza mwana kabla hajamaliza shughuli kwenye pot yake
  :caked::peace:
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  May 2, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  It is a reasonable amount, isn't it?
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  .
  .
  Ni michango ya wanachama pamoja na marafiki wa chama wa ndani na nje ya nchi. Chadema ndio waasisi wa michango kwa njia ya simu na ccm waliwaigiliza. Pia inaonyesha ni chama kinachoheshimu utawala wa sheria kwani sheria ya gharama za uchaguzi ndicho kiasi ilichoweka cha juu. Ccm ni nyani ambae kufa kwake kumekaribia na ishara ni kwamba miti yote inateleza. Mwenyekiti wake anasign sheria leo na keshokutwa yake anaivunja maana hakumbuki hata kilichokuwa kwenye sheria aliyosign mwenyewe. Ni mungu aliyemleta m/kiti wa namna ya JK kuweza kufanikisha kuipeleka ccm kaburini maana imekufuru kwa kufikiri kuwa itatawala milele.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,172
  Trophy Points: 280
  CCM ina bilioni 50 halafu CHADEMa ina bilioni 5 tu ambazo ni sawa na 10% ya pesa za CCM uchaguzi huu kweli ni wa haki?
   
 7. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  .
  Hii inatokana na rais aliyepo madarakani kutokujiamini na hivyo kumlazimu kukusanya fungu kubwa la kununua uongozi. Hasikii, haambiliki wala haelewi hata kama kuna wafanyakazi wanataka kuanza mgomo kwa sababu ya cent wanazolipwa na serikali kama mshahara wao wa mwezi. Rais anachowaza ni jinsi tu ya kupata BL50, habari ya mlalahoi kutaka laki tatu na kumi na tano ya mshahara, hilo halimhusu.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,172
  Trophy Points: 280
  Ni lazima kuhakikisha uchaguzi unakuwa halali kwa kuhakikisha pia pesa zinazotumika na vyama katika kampeni za uchaguzi hazina tofauti kubbwa kiasi hicho, vinginevyo kuita uchaguzi ulikuwa "free and fair" ni mazingaombwe maana kamwe haiwezekani chama cha pili kwa umaarufu nchini kitumie 10% ya bajeti ya chama kilicho madarakani katika gharama za kampeni na kisha kuuita uchaguzi huo "free and fair election" Si ajabu vyama vyote vya upinzani bajeti yao ya pamoja ya gharama za kampeni haitafikia hata 15% ya bajeti ya CCM.
   
 9. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2010
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda hiyo. Tatizo bado wananchi wenyewe hawajaweza kufikia hatua ya kufanya mabadiliko kwa sanduku la kura. No wonder watawala wanatamba majukwaani kwamba wao ni chama tawala na kitaendelea kushinda. Kwa mtaji wa Bil 5 kwa 50, opposition have a lot ot do. .
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  As if uchaguzi ni muarobaini..lol

  Sitacomment kwene hiyo bil 5 bcoz it is beyond my reversed logic..
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Umeongea..suala sio wananchi wafanye mabadiliko, suiala hapa ni kila mtu ajue mabadiliko yepi tunayataka kueka kufika nchi ya ahadi. Mambo ya siasa hayatatupeleka kwenye nchi ya ahadi thats a bottom line..tunajitahidi kukwepa hili to own peril.
   
 12. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #12
  May 3, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sijui JK atakuja na kaulimbiu ipi this time, maana alikuja na ile ya MAISHA BORA KWA KILA MTZ, baada ya kuona hajawaletea maisha bora watz akabadili usemi, eti MAISHA BORA HAYAJI KWA KUKAA KIJIWENI!
   
 13. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ivi hizi 50 b ina sifuri ngap?

  Kaazi kwelikweli. tukimaliza uchaguzi tuendelee na uchangishaji wa namna hii, yaani mabilioni kwa kila idara kama afya, elimu, miundo mbinu na nyonginezo, tunaweza kiukweli.
  Ila kwenye siasa mmh!!!
   
 14. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Hivi 5 billion zinatosha kweli????....kwangu mimi naona kama hazitoshi vile...maana wakati wa kampeni chama chahitaji kujitangaza(kwa karibu miezi miwili kama sikosei),kuzunguka Tanzania nzima kuwanadi wagombea wa nafasi za Urais,ubunge na madiwani....Hapa kuna ruzuku kwa wagombea(kama ipo) kuwasaidia katika kampeni,kuchapisha vipeperushi n.k,gharama za helicopter(kama zitakuwepo).......So sijajua itakuwaje(labda nikiona mchanganuo wake) maana kupambana na chama kikubwa kama CCM inahitaji kujipanga hasa(kwa kila kitu)......hii inamaanisha kwamba CCM tayari watatumia zaidi ya Tshs 45 bil kuhakikisha kwamba wanabaki madarakani na wanachukua viti zaidi vya ubunge na madiwani....hata sijui itakuwaje hapa......hesabu zinakataa kabisa.....ni mtazamo tu
   
 15. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  jirani hujui bilion 50 ina sifuri ngapi?

  kwa kila idara haiwezekani hivi jembe nikuulize umewahi kurudisha dawa ya meno kwenye tyubu yake??
   
 16. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unajua nini jirani, namuwazia mtz wa kawaida anaijua hizo bilioni inakuaje? mi sielewi na sina mpango wa kuchangia, labda kuwainua wanyonge ndio ntafanya, mtawala hawezi kumuinua mtawaliwa ili wawe sawa hata siku moja,. Ni sawa na wewe unavyomfanyia dereva tax, au wafanyakazi wako wa chini, usitegemee mtawala wako kukufanyia mema sana. kama sisi tunaweza kujitetea kwa nguvu zenu na pia kutumia viunganisho vyetu kama TUCTA basi ni wakati wetu, tuibadili Tanzania.
   
 17. M

  Magezi JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Tanzania itaweza kuwa na wapiga kura wenye kujua nini wanafanya pale tu wale walianza sekondari za kata watamaliza form iv
   
 18. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,675
  Likes Received: 21,903
  Trophy Points: 280
  Mkuu hujaijua kauli mbiu yake? mbona alishaitoa tayari! "UKITAKA KULA SHURTI ULIWE" Sikumbuki sawasawa aliitolea wapi ila wakuu humu ndani wapo wanaokumbuka
   
 19. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Sometimes tuwe serious...tuache uzushi bana....Kauli mbiu ya uchaguzi wa mwaka 2010 si inakuwepo kwenye ilani bana...bado haijatoka.....Huu ni upotoshaji babaake
   
 20. B

  Bull JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haka kachama kadokgo ka kikabila kidogo na vikanisa fulani Utafananisha na bajeti ya lichama likubwa lisilo na dini wala ukabila kama CCM, nyie watu wachadema kweli mnachekesha!

  Viongozi wenu hawajasoma nanyie wafuasi pia mnaonekana mbumbumbu, Mbowe kafeli darasani, Mchungaji slaa kajisomea kitabu cha nabii paul akafanya mtiani, kweli hawa ndio tuwakabidhi nchi??? You must be jocking guys!!
   
Loading...