Tulikaa kikazi zaidi, na mkutano wa ndani unaendela. Kama ulidhani neno hukuna kulala ni utani, leo Morogoro imeangukia CDM. Nitaweka picha kesho. Mabomu yamefanya macho yangu yasione vizuri kwa sasa. Lakini Tumepoteza kijana mmoja kwe uzembe wa FFU. Inaonekana kelengwa mu kichwa na risasi ya moto. Na alikuwa anasoma gazeti, na inasemekana alikuwa ni muuza gazeti. Njia niliyotumia kuingilia msamvu ilikuwa front line. FFU wapiga watu bila makosa.
Mkutana ulikuwa nyomi, kwa mujibu wa wenyeji wa Moro haijawahi kutokea, licha ya mbinu chafu cha makada wa CCM kujaribu kutumia polisi kuhujumu mkutano. Mida ya saa kumi shughuli nyingi za Moro zilisimama maana watu wengi walikuwa mkutanoni
Dk wa ukweli na timu yake wamemchana kiuhakika mbunge wa Moro, na Polisi wilaya. Kiasi cha waruguru kutupa hovyo kadi za CCM. Hotuba ilikuwa sio ya kawaida, ilikuwa ya kisayansi.