Wana jf kwanza niwaombe wale wote ambao labda walijiunga na mtandao huu kwa bahati mbaya basi wausome tu huu uzi wasichangie. wawaachie wale wenye uono mpana wajaribu kutoa maoni yao pamoja kudadavua zaidi ili labda kama nitakuwa nimekosea nipate sababu yakujirekebisha.
Ni kiri kwa uwazi kabisa kwamba wakati wa Uchaguzi mkuu uliopita, nilipiga kura zangu zote tatu kwa CHADEMA. Yaani kura ya Uraisi kwa SLAA, Ubunge pamoja na Udiwani zote niliwapigia CHADEMA. Niliwapa kura zangu nikiamini kabisa nilikuwa napigia kura mabadiliko. Nakumbuka Makala ya Gazeti la Raia Mwema la Alhamisi ya mwisho kabla ya uchaguzi mkuu iliyokuwa na kichwa cha Habari "HERI WATAKAO CHAGUA MABADILIKO" iliyoandikwa na mwandishi Jonson Mbwambo, ilivyonivutia na kunihamisisha kupigia kura mabadiliko.
Nilijitahidi kuhamasisha wengine kuanzia kwenye familia, marafiki, majirani na kila kijiwe nilichoweza kuwepo ili nao wapigie kura mabadiliko, na mabadiliko hayo yalionekana ndani ya CHADEMA. Hatukuishia kupiga kura tu, bali tulihakikisha tunazifuatilia kura zetu. Nakumbuka jioni ile wakati kura zinahesabiwa ndani huku nje vijana tulikuwa na mihemko ya ajabu na kila mara tukiwasiliana na makamanda waliokuwa ndani kama mawakala huku wakitujibu tusiwe na wasiwasi kwani mambo ni mazuri. Kama ni experience ya UKAMANDA basi wakati ule ukamanda wangu ulikuwa wa kiwango cha juu sana.
Lakini CHADEMA kushindwa kuzisimamia AGENDA wanazo zianzisha ndiko kunakonifanya nifikirie upya kuhusu kuwapa tena kura zangu hapo mwakani Mungu akitupa uhai katika uchaguzi Mkuu. Agenda nyingi wanazo zianzisha huwa zinaishia hewani. Mfano wa agenda hizo ni hizi zifuatazo.
1. KUTOKUMTAMBUA RAIS KIKWETE.
Ikumbukwe kwamba, mara baada ya matokeo yote ya Urais kujumlishwa pamoja na kumpa ushindi JK, CHADEMA walitangaza rasmi kutoyatambua matokeo hayo na kutomtambua Raisi JK. Nakumbuka CHADEMA haikushiriki katika hafla ya kutangaza matokeo rasmi ya uraisi, haikushiriki katika sherehe za kuapishwa kwa raisi Kikwete. Na tukio kubwa ni lile la Wabunge wote wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa Bunge mara tu Raisi Kikwete aliposimama ili kulihutubia bunge hilo kwa mara ya kwanza. Lakini mimi sikumbuki ni lini CHADEMA walibadilisha msimamo, na kama kweli waliutangazia umma wa watanzania kwamba wamebadili msimamo na kuanza kumtambua Raisi Kikwete kama Raisi wao pia. Kilichotushangaza ni wao CHADEMA kuukubali mualiko wa kwenda Ikulu kuonana na Raisi JK ili kujadili hatima ya muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba. Kwa wao kukubali kwenda Ikulu kuonana na kujadiliana na kukubaliana mambo kadhaa na Raisi Kikwete, haihitaji akili ya darasani kufahamu kwamba WALISHAAMUA KUBADILISHA MAAMUZI NA KUMTAMBUA RASMI KIKWETE kama Raisi halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nini kilitokea hadi wakaamua kubadili msimamo hakijulikani na wala wanachadema na makamanda watiifu hatujawahi kuelezwa. Agenda hiyo ikaishia hewani.
2. KATIBA MPYA.
Ikumbukwe kwamba suala la katiba mpya lilikuwa ni moja ya agenda za CHADEMA wakati wa uchaguzi mkuu uliopita. Mgombea uraisi wa CHADEMA akaahidi waziwazi kwamba ndani ya siku mia moja za kuwa ofisini, angewapatia wananchi katiba mpya(labda alikuwa anatania). Moja ya sababu kuu za kudai katiba mpya ilikuwa ni kuhakikisha rasilimali za taifa zinalindwa kwa manufaa ya wananchi wote wa taifa hili. Lengo kuu lingine lilikuwa ni kuhakikisha kwamba katiba inaweka miiko imara ya uongozi ili kuminya mianya ya ufisadi. kwakweli hayo mpaka leo bado ndiyo mahitaji makubwa ya wananchi wanyonge wa taifa hili. Na CHADEMA walitegemewa wayatetee iwe kwenye serikali moja, mbili au hata hizo tatu. suala la idadi ya serikali kama ziwe tatu au mbili au moja halikuwepo kabisa wakati ule. Ukweli ni kwamba idadi ngapi za serikali tuwe nazo, ni kwasababu tu ya interest za viongozi(vyeo) na si wananchi. Kwa kuususia mchakato wa katiba kwasababu ya idadi ya serikali, ni sawa na kutupilia mbali interest za wanyonge ambazo mlizibeba wakati ule na kugeukia interest za madaraka ya uongozi. Tunaamini kwamba Rasilimali za wananchi zinaweza kulindwa katika serikali moja, mbili na hata tatu. Maadili ya uongozi yanaweza kupewa makali katika serikali moja, mbili na hata tatu. Usawa wa 50% kwa 50% unaweza kuwepo katika serikali moja, mbili na hata tatu. Maendeleo makubwa ya kiuchumi yana weza kupatikana katika serkali moja, mbili na hata tatu. Sasa iweje mshindwe kusimamia mahitaji muhimu ya wanyonge kwasababu moja tu ya idadi za serikali??? hapo agenda kuu mlioianzisha ya katiba mpya mmeiacha hewani na kuwaacha wanyonge tumeduwaa.
3. MAANDAMANO.
Ikumbukwe pia kwamba Mwenyekiti taifa wa CHADEMA Mh. Mbowe alitangaza maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima ili kupinga kuendelea kwa bunge la katiba. Na akaenda mbele zaidi kwa kusema maandamano hayo ni lazima yafanyike hata kama yatakosa kibali toka kwa jeshi la polisi. Siku ya kuanza maandamano, tunaambiwa Mbowe amesafiri kwenda Afrika ya kusini, Vijana kadhaa wakajikuta peke yao ndio waratibu wa maandamano hayo huku kukiwa na ukimya wa Mwenyekiti na Viongozi wake wa kitaifa. Hadi naandika bandiko hili sijamsikia Mbowe au kiongozi yeyote akisema kama yaliahirishwa au kumetokea nini hadi kushindwa kwa AGENDA hii nayo inayoishia hewani kama nyingine.
Wakuu hiyo ni mifano ninayoikumbuka ambayo ni AGENDA za kitaifa ambazo CHADEMA walizianzisha lakini zikaishia hewani huku wananchi wakiachwa kwenye mataa. Hebu tujadili kuna sababu zipi zinazo wakwamisha?? je, wanaweza kuaminiwa na wananchi wawabebee agenda zao. Jadili!
NB. kwa wale ambao kwao wao kila bandiko lenye changamoto kwa CHADEMA basi limefadhiriwa na Lumumba basi hatuwalaumu, wao ni akili ndogo tutawapuuza)!
thegame